Katavi: Tundu Lissu apinga Muswada wa Sheria ya Usalama wa Taifa kuwasilishwa bungeni, adai utaleta Ukiritimba

Kama rais ataendelea kuwa juu ya sheria, mambo mengi yataendelea kutekelezwa kwa utashi wa rais na sio kwa sheria. Tukitaka sheria wangalau ziwe na meno, kinga ya kutoshtakiwa ya rais iondolewe. Na haya hayawezi kupatikana kwa katiba hii. Na ili ipatikane katiba ya kumdhibiti rais ni aidha yatokee machafuko, au serikali kupinduliwa. Kinyume na hapo, hiyo katiba ya maridhiano italeta mabadiliko mepesi tu.
 
Hayo marekebisho ndio sahihi na yanaleta uhalisia. Utawala bora ilikuwa kivuli tu bora ijulikane direct Rais yuko responsible.

Hofu ya kuondolewa Polisi kwa wagombea itabadili nini wakiwa usalama? Bado Rais ni amri jeshi mkuu akitaka taarifa atazipata tu.

Issue ya Usalama kukatazwa kufanya kazi za Polisi nafikiri iliwafunga mikono Usalama na wakati mwingine kuhatarisha kuharibu operation zao. Ijulikane tu aina ya makosa watayo deal nayo direct bila kupitia Polisi.
Loh! Siwezi kusema sana. Ebu jipe muda kutafuta elimu na maarifa namna idara hizi zinavyotakiwa kufanya kazi.

Inayozungumziwa hapa ni idara ya usalama wa Taifa siyo idara ya usalama wa Rais. Hii inatakiwa kulitazama Taifa na siyo Rais. Rais akionekana kuhatarusha maslahi ya Taifa, idara hii hutakiwa kuchukua hatua za wazi na za siri kwa dhamira ya kuliokoa Taifa.
 
Taasisi ya usalama wa Taifa nayo unaenda kuwekwa kwenye kapu la kutoweza kushtakiwa lakini pia inaenda kupewa mamlaka ya kukamata Rais😏😏 . CCM oyee,dalili ya anguko lako inazidi kutamalaki.
 
No hapa kachemka. Hata polisi wako chini ya rais kiufupi rais alitaka taarifa yoyote anapata. Hata alitaka jue Jana umelala na Malaya Gani atajua tu
Wewe unaona hiyo ndio Kazi ya Rais? Nchi gani nyingine yenyeutaratibu Huo na ilifanikiwa kimaendeleo?
 
Kama rais ataendelea kuwa juu ya sheria, mambo mengi yataendelea kutekelezwa kwa utashi wa rais na sio kwa sheria. Tukitaka sheria wangalau ziwe na meno, kinga ya kutoshtakiwa ya rais iondolewe. Na haya hayawezi kupatikana kwa katiba hii. Na ili ipatikane katiba ya kumdhibiti rais ni aidha yatokee machafuko, au serikali kupinduliwa. Kinyume na hapo, hiyo katiba ya maridhiano italeta mabadiliko mepesi tu.
Aiseeee !!

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Akizungumza kwenye Oparesheni ya chama chake inayoitwa 255 ambayo sasa iko Mkoa wa Katavi , Tundu Lissu amedai kwamba amepewa Taarifa ya kupelekwa Muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa Bungeni , kwenye vikao vinavyoendelea , Huku akidai kwamba Muswada huo una nia ovu .

Mbele ya Maelfu ya Wananchi Lissu amedai kwamba lengo la Muswada huo ni kumpatia Rais Mamlaka ya moja kwa moja ya kuendesha shughuli za Usalama wa Taifa na kuondoa mamlaka hayo kwa Waziri wa Utawala Bora kama ilivyo sheria ya sasa ambayo ilitungwa wakati wa uongozi wa Benjamin Mkapa , ambako Mawaziri waliowahi kuhudumu walikuwa Mkuchika na Masilingi .

Lissu amesema kifungu cha 5:2(b) cha sheria hiyo ya mwaka 1996 kinakataza maofisa wa Usalama wa Taifa kufanya kazi za Polisi , jambo ambalo kwenye muswada huu wa sasa linaenda kuondolewa .

Anasema ndani ya Muswada huo hata wale walinzi wa Wagombea wa Urais wakati wa Uchaguzi , wale waliokuwa Polisi na waliratibiwa na IGP , sasa wanatakiwa waondolewe na Wawekwe maofisa wa Usalama wa Taifa ambao wataripoti moja kwa moja kwa Rais , ambaye naye atakuwa Mgombea , maana usalama wa Taifa ni kitengo kitakachokuwa chini yake moja kwa moja.

Toa Maoni yako .
Hizi sheria zinatungwa kwa siri? Wananchi hawapaswi kamwe kushirikishwa kwa namna moja au nyingine tokea huko mwanzo, au kwa vile kuna mbunge waliyempata kwa uteuzi wa chama kimoja?

Yale "maridhiano" ya Mbowe na Samia, bado yapo hai, au sasa Mbowe anaonyeshwa mazingaombwe aliyohusishwa nayo!
 
Mchakato wa Maridhiano unaendelea

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Usalama wa Taifa nachojua wana ripoti moja kwa moja kwa Mh. Rais, na iko chini ya Mh. Rais, nadhani hiyo sheria eti Usalama wa Taifa iwe chini ya Waziri wa Utawala Bora ni kosa.

Kiutekelezaji hata sasa, Usalama wa Taifa wana ripoti kwa Mh. Rais, hivyo sheria ikibadilishwa na waripoti kwa Mh Rais, itakuwa bora, sbb kiutendaji hata sasa iko hivyo.

Tundu Lissu anaropoka hovyo, hajui kitu
 
Kama ni kweli basi ccm ni janga, na inatengeneza jang kubwa.

Mamlaka makubwa anayopewa raisi yatakuja kumgharimu baadae.
 
Back
Top Bottom