Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 106,835
- 189,753
Akizungumza kwenye Oparesheni ya chama chake inayoitwa 255 ambayo sasa iko Mkoa wa Katavi Tundu Lissu, amedai kwamba amepewa Taarifa ya kupelekwa Muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa Bungeni, kwenye vikao vinavyoendelea huku akidai kwamba Muswada huo una nia ovu.
Mbele ya Maelfu ya Wananchi Lissu amedai kwamba lengo la Muswada huo ni kumpatia Rais Mamlaka ya moja kwa moja ya kuendesha shughuli za Usalama wa Taifa na kuondoa mamlaka hayo kwa Waziri wa Utawala Bora kama ilivyo sheria ya sasa ambayo ilitungwa wakati wa uongozi wa Benjamin Mkapa, ambako Mawaziri waliowahi kuhudumu walikuwa Mkuchika na Masilingi.
Lissu amesema kifungu cha 5:2(b) cha sheria hiyo ya mwaka 1996 kinakataza maofisa wa Usalama wa Taifa kufanya kazi za Polisi, jambo ambalo kwenye muswada huu wa sasa linaenda kuondolewa.
Anasema ndani ya Muswada huo hata wale walinzi wa Wagombea wa Urais wakati wa Uchaguzi, wale waliokuwa Polisi na waliratibiwa na IGP sasa wanatakiwa waondolewe na Wawekwe maofisa wa Usalama wa Taifa ambao wataripoti moja kwa moja kwa Rais ambaye naye atakuwa Mgombea, maana usalama wa Taifa ni kitengo kitakachokuwa chini yake moja kwa moja.
Toa Maoni yako.
Pia soma: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa unaoifanya iwe chini ya Usimamizi wa Rais watua Bungeni