Katavi ni Katavi - Mkuu wa mkoa, viongozi waingia mkenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katavi ni Katavi - Mkuu wa mkoa, viongozi waingia mkenge

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by bornagain, Aug 20, 2012.

 1. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Viongozi watatu wa ngazi ya juu wa Serikali ya Mkoa wa Katavi wametapeliwa na watu wasiojulikana baada ya kuelezwa kuwa wameshinda promosheni ya Airtel ya Shilingi milioni 50.

  Waliotapeliwa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajabu Rutengwe, Katibu Tawala wa Mkoa, Emmanuel Kalobelo na Mganga Mkuu wa Mkoa, Yahaya Hussein.

  Viongozi hao walitapeliwa kwa nyakati tofauti na watu waliojitambulisha kwao kwa simu kuwa ni watumishi wa Kampuni ya Simu ya Airtel.

  Tukio la kwanza lilikuwa ni la Mkuu wa Mkoa kuambiwa ameshinda zawadi ya Sh. milioni 50 na aliombwa awatumie namba za simu za watu watano aliozungumza nao mara ya mwisho na baada ya kufanya hivyo simu yake ya mkononi ikafungwa na matapeli hao.

  Akieleza mkasa huo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Yahaya alisema yeye baada ya kupigiwa simu na matapeli hao hakuwa na shaka nao kutokana na kauli yao ilivyokuwa ya ustaarabu. Alisema baada ya kuwapa majina ya watu watano alizungumza nao mara ya mwisho kwenye simu yake na kuombwa awatajie namba zake za siri za akaunti ya Benki ya NMB ili wamtumie zawadi ya Sh. milioni 50. Baada ya kuombwa namba yake ya siri, Dkt. Yahaya hakuwa na shaka yoyote na hivyo akawapatia namba hiyo ya siri. Hata hivyo hakuweza kuibiwa fedha zozote kwa vile akaunti yake haikuwa na salio la kutosha.

  Meneja wa Wawi la NMB Wilaya ya Mpanda, Erick Luhanda alisema amepokea malalamiko kutoka kwa viongozi hao. Alisema kiongozi wa mwisho kumpa taarifa alikuwa ni Katibu Tawala wa Moka, Kalobelo. Luanda alisema tayari taratibu za benki zimefanyika hivyo hakutakuwa na hujuma kwenye akaunti za viongozi hao.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alithibitisha kutokea matukio hayo.


   
Loading...