Katavi: Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imesababisha madhara makubwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,823
2,000
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imesababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kujeruhi watu Saba na kubomoa nyumba 59 katika kijiji cha KIBAONI na ILALA – NGULU mkoani KATAVI.

Mkuu wa Wilaya ya MLELE, RACHIEL KASANDA amethibitisha kubomoka na kuezuliwa paa kwa nyumba hizo na kuwatahadharisha wakazi wa wilaya ya MLELE kuwa makini na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kakuni amesema shule hiyo imeathiriwa na Mvua hizo.
 

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,793
2,000
ina maana hizi mvua zina mpango gani na sie mwaka huu, hazitaki kunyesha, zikinyesha hazina ustaarabu, hazitaki tulime chakula
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom