KATAVI:Mradi wa nyuki washindwa kuzinduliwa baada ya watu wasiojulikana kuteketeza mizinga kwa moto

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2017 zimeshindwa kuzindua mradi wa ufugaji wa nyuki katika kijiji cha Kaseganyama wilayani Tanganyika mkoani Katavi baada ya mizinga ya nyuki kuteketezwa kwa moto na jiwe la msingi la mradi huo kubomolewa kabisa na watu wasiojulikana.

Mara baada ya kufika katika eneo hilo na kukuta moto ukiendelea kuteketeza mizinga hiyo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amour Ahmed Amour ametaka watu waliofanya kitendo hicho kutafutwa.

Akizungumzia hasara iliyopatikana afisa nyuki wa halmashauri ya Mpanda Bruno Nicolaus amesema halmashauri ilipanga kutoa mizinga 40 yenye thamani ya shilingi milioni tatu laki mbili na ishirini elfu kwa kikundi cha nyuki na mazingira; ambayo imeteketezwa kwa moto na kusalia mizinga mitano ambayo haitafaa kutundikwa kutokana na kuharibika.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Bwana Issa Bida amesema nyuki na mazingira Bida amesema wamegundua moto huo majira ya asubuhi wakati walipofika kusubiri mwenge; ambapo hii ni mara ya pili ambapo mara ya kwanza kuharibiwa kwa kijiwe cha kikundi hicho kulitokea Machi 14 mwaka huu ambapo watu wanne wamefikishwa mahakamani.


Chanzo: ITV
 
Kuna kitu kimefichwa hapa...

Isije kuwa watendaji wa mamlaka za kijiji walikamata eneo la wananchi kwa nguvu na kuweka mradi wa nyuki bila kuwalipa wenyewe fidia.
Au mradi ulikuwa karibu sana na makazi ya watu.
 
Inawezekana wamekula pesa na kuamua kupoteza ushahidi kwa thamani ya mradi na hela iliyotumika.
 
Back
Top Bottom