KATAVI: Masheikh watano wajiuzulu uongozi ndani ya BAKWATA kwa kuchoshwa na baadhi ya mambo

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,605
2,000
Masheikh watano akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), mkoani Katavi, Sheikh Shaban Bakari wamejiuzulu uongozi wakidai kuwepo kwa migogoro ya uongozi na ukiukwaji wa Katiba ya Bakwata.

Halmashauri ya baraza hilo inaundwa na viongozi sita ambao ni Masheikh, watano kati yao ndio waliotangaza kujiuzulu ambao ni Mwenyekiti wao Sheikh Bakari, Sheikh Mashaka Kakulukulu, Sheikh Hassan Mbaruku, Sheikh Said Haruna Omary na Sheikh Mohamed Sigulu.

Wakitangaza uamuzi huo jana mjini Katavi mbele ya waandishi wa habari, Sheikh Kakulukulu alisema haoni sababu ya kuendelea kuwa kiongozi wa halmashauri ya baraza hilo akidai kumekuwepo na baadhi ya mambo ya hayaendi sawa.

"Hata Katiba ya Bakwata imekuwa ikikiukwa na kusababisha migongano ya kimaslahi, hata utekelezaji wa miradi ya maendeleo umekwama kutokana na msuguano wa kiuongozi", alisema Sheikh Kakulukulu.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Masheikh wengine, huku Sheikh Sigulu akidai kuwa msuguano uliopo wa kiuongozi ndani ya Bakwata umesababishwa na mwalimu wa madrasa katika Msikiti Mkuu mjini Mpanda kuamua kuacha kazi ya kufundisha hivi karibuni.

Chanzo: HabariLeo
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,605
2,000
Wasingefanya hivyo, hayo mambo ya kujiuzulu wawaachie wanasiasa

Walitakiwa wapambane wawe sehemu ya mabadiliko ambayo yanahitajika
 

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,755
2,000
Unakuta nao wanataka tu nafasi ili wapate ka hela ka kuoa wake wengine na wengine

shikamoo baba J embu wanyooshe hawa mashekhe ili wakienda haja kubwa chooni waitoe wakiwa wamesimama wasiweze kupinda
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
19,703
2,000
Huku kujiuzulu hakuhusiani na kutolipwa mshahara kwa muda wa miezi kumi na moja?
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,605
2,000
Unakuta nao wanataka tu nafasi ili wapate ka hela ka kuoa wake wengine na wengine

shikamoo baba J embu wanyooshe hawa mashekhe ili wakienda haja kubwa chooni waitoe wakiwa wamesimama wasiweze kupinda
Ebu jiheshimu....acha kejeli haisadii kitu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom