Katavi: Baba mdogo adaiwa kumuua mtoto baada ya mtoto huyo kupoteza ng’ombe aliokuwa akiwachunga

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,372
Mtoto aitwaye Lusambaja Bundala(7) Mkazi wa Kitongoji cha Luhafwe Kata ya Ntongwe Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi ameuawa kwa kupigwa kichwani na kukatwa na kitu chenye ncha kali na anayedaiwa kuwa baba yake mdogo baada ya mtoto huyo kupoteza ng'ombe aliokuwa akiwachunga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Benjamin Kuzaga alisema kuwa tukio hilo limetokea Septemba 16,2019 majira ya saa nne asubuhi katika kitongoji cha Luhafwe wilaya ya Tanganyika.

Alieleza kuwa wakati wa uhai wake, marehemu alikuwa akiishi nyumbani kwa baba yake mdogo aitwaye Juma Lusambaje (28) ambaye ndiyo mtuhumiwa wa mauaji hayo.

"Kabla ya kuuawa kwa mtoto huyo,Septemba 12,2019 marehemu akiwa na mtoto mwenzake aitwaye Ibrahimu Lusambaja(13) walitumwa na mtuhumiwa kwenda kuchunga ng'ombe. Tangu siku hiyo hakuonekana hadi hapo jana majira ya saa nne asubuhi alipokutwa akiwa amefariki dunia kwa kuuawa kwa kupingwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kuchomwa na kisu chini ya kidevu",ameeleza Kamanda Kuzaga.

Kamanda Kuzaga amesema chanzo cha mauaji ya mtoto huyo ni hasira za mtuhumiwa baba yake mdogo Juma Lusambaja kuchukia baada ya marehemu kupotelewa na ng'ombe aliokuwa anachunga.

"Baada ya marehemu kupoteza ng'ombe ndipo mtuhumiwa alipoamua kuchukua sheria mikononi na kuamua kumpiga mtoto kwa kutumia chuma chenye ncha kali na kumchoma na kisu hadi kumuua na hakutoa taarifa kwa mtu yeyoye",ameongeza.

Amesema Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani ili akajibu tuhuma zinazo mkabili

Mwili wa marehemu umekabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajiri ya mazishi baada ya kuwa umefanyiwa uchunguzi wa kidaktari.
 
utaratibu wa ku exchange binadam na ngombe umezipandisha hadhi mno ng'ombe
 
Back
Top Bottom