Katavi: Aliyejenga madirisha katika kituo cha Afya cha Katumba ayavunja baada ya Halmashauri kutomlipa

Ndio tatizo la mswahili..huwa hatuna uvumilivu...utafkiri hayo malipo watamdhulumu.
Ni sehemu chache sana nchi hii mafundi wamelipwa na halmashauri, kila anakopita Rais, waziri mkuu malalamiko ni hayohayo, au majengo hayatengewi bajeti ya madirisha?
 
Mkandarasi aliyefahamika kwa jina la Boniface Exavery, ambaye alitengeneza madirisha ya Almunium na katika Kituo cha Afya cha Katumba, Halmashauri ya Nsimbo ya mkoani Katavi, ameyavunja madirisha hayo, kwa kile alichokidai kutokamilishiwa malipo yake na ofisi ya Halmashauri huku akiwaameshamaliza kazi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, amedai mradi huo ulikuwa umekiuka taratibu mbalimbali za kisheria, ikiwemo upatikanaji wa tenda hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, mwenyewe ameeleza kushtushwa na hatua ya Mkandarasi huyo, na kueleza taarifa za awali walizipata kutoka kwa wananchi, na kulitaka Jeshi la Polisi kumshikiria Mkandarasi huyo, huku akikiri Halmashauri kutomlipa malipo yake.

Mmoja wa Wakandarasi ambaye anajulikana kama Bulaya Mushi, ambaye na yeye anaidai Halmashauri hiyo kwenye mradi huo wa Kituo cha Afya, amemuomba Mkuu wa Mkoa kuangalia madai yao ili waweze kulipwa na Halmashauri hiyo.
HAKUNA KAZI NGUMU KAMA UHAKIMU. SIJUI ITATOLEWA HUKUMU GANI HAPO. JAMAA ANADAI KWELI. LAKINI KAHARIBU ANACHOKIDAI !!! DUH SIPATI PICHA NA ANATAKIWA KUISAIDIA PORIS, KAZI IPO.
 
Jina lenyewe lina gundu 100% Mchanyiko tata kabisa wa wasiotakiwa!
Hata yule polisi aliyesimamishwa kazi na kushushwa cheo kule Sumbawanga anaitwa ACP Urio. Angekuwa Masalu au Mabula kungekuwa na leniency sana, trust me. Mambo haya yanafanana dunia nzima, angalia ile kesi ya Amber Guyger yule binti polisi mzungu aliyeua mwafrika, hata mkosaji anapambwa kadri iwezekanavyo!
Awamu hii ukijiona unaitwa Mushi, Macha, Urio, Chami, Massawe na mengine kama hayo play safe and keep a very low profile, yatapita haya halafu maisha yako yataendelea.
 
HAKUNA KAZI NGUMU KAMA UHAKIMU. SIJUI ITATOLEWA HUKUMU GANI HAPO. JAMAA ANADAI KWELI. LAKINI KAHARIBU ANACHOKIDAI !!! DUH SIPATI PICHA NA ANATAKIWA KUISAIDIA PORIS, KAZI IPO.
Huenda wakati anaenda kuyang'oa madirisha yake akiyozulumiwa ndio uharibifu ukatokea kwenye madirisha yake hapo mwenye hatia ni Mkurugenzi.
 
1570626071989.png
 
Ndio tatizo la mswahili..huwa hatuna uvumilivu...utafkiri hayo malipo watamdhulumu.
Nina uhakika kabisa kwamba haujawahi kufanya kazi na hizi halmashauri....hata ukibisha huo ndio ukweli kwamba haujawahi.
Je unajua Kuna wazabuni mbalimbali wamefanya kazi na hizi halmashauri na wameishafuatilia miaka mingi wakizungushwa hadi wakaamua kuacha hizo fedha?
Wapo wengi sana sana na hata hapa wapo wanasoma hili tukio ni mashahidi.
Sisi wenyewewe tuliishaacha 70+ milioni Jiji la Mwanza, na takribani 15m huko Nyasa DC. Sio hapo, tumeacha takribani 30m Tume ya Madini Dodoma.
Orodha ni ndefu na nimesahau kiwango tulichoacha temeke DC.
kwahiyo rodha ni ndefu halafu sasa unakuta umechukua mkopo benki, na wafanyakazi wanadai ila ukienda halmashauri wanakuzungusha na kukwambia pesa imetumika kwenye dharura na mambo mengine. Halafu kitu kibaya ni kwamba kazi yako ndio wanajisifu nayo kwenye vyombo vya habari.
Namuunga mkono huyu fundi, na ujumbe umewafikia
 
Pole sana kamanda...inasikitisha kwakweli
 
Ndio tatizo la mswahili..huwa hatuna uvumilivu...utafkiri hayo malipo watamdhulumu.
Yaani ufanyiwe kazi halafu usinilipe kwa wakati,sasa pesa itaninufaishaje ukinipa muda ambao haihitajiki?Wewe yawezekana ni mmoja wa wale ambao wakikopa anakuja kulipa baada ya muda wa makubaliano kupita.
 
Kama angeacha ingekuwa alama wazi ya udhalimu aliofanyiwa na kwa vile amevunja hapo ndipo uhujumu unapoanzia na ile mali haikuwa yake na hapo kosa linakuja kuharibu mali ya umma!! Hana uvumilivu
Action and reaction are equal but opposite in direction
 
Back
Top Bottom