Katani A. Katani anawatumia baadhi ya watumishi wa Serikali kuja Tandahimba kuwatishia na kuwasumbua wananchi

Ndendende

Member
Oct 8, 2016
57
39
Katani A. Katani ni miongoni mwa vijana waliowahi kuwa na dhamana ya ubunge katika jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara.

Miongoni mwa wananchi wamekuwa na kauli kwamba muda umefika wa kufanya maamuzi ya kumuondoa Katani A. Katani ambaye alikuwa miongoni mwa wabunge wavivu wa kufikiri na wavivu wa kufikisha changamoto za wananchi kwa njia sahihi.

Katani A. Katani anawatumia baadhi ya watumishi wa serikali kuja Tandahimba kuwatishia na kuwasumbua wananchi ambao wanashughuli zao kwa kuwaonesha kwamba yeye ndiye alistahili kuongoza kura za maoni.

Katani Katani alikuwa anaamini yeye ndiye anastahili kuwa mbunge wa milele kwa jimbo la Tandahimba na ndio maana akaamua kuihama CUF huku akisema amehakikishiwa ushindi na viongozi wa juu wa CCM kitu ambacho sio kweli.

Katani Katani anashirikiana kwa karibu na Mhesh. Chilota ambaye ameongoza kura za maoni jimbo la Nanyamba. Tangu awali uhusiano huu ilifika hatua Katani Katani anawasafirisha Makatibu wa kata za Tandahimba kuwapeleka Nanyamba kufanya vikao vya mikakati ya namna katani anavyotakiwa kuwa mshindi katika kura za maoni.

Katani Katani haungwi mkono na wananchi wa Tandabimba hata kura alizozipata zilitengenezwa kwa njia ya kupanga vijana 10 maalumu wa kusaidia wasiojua kusoma na kuandika ambao ni wapiva kura wengi hawajui kusoma na kuandika. Vijana hao waliandaliwa na Mwenezi wa Wilaya ambaye ni mtiifu wa Katani hata kipindi katani yupo upinzani alikuwa anampa siri za vikao vya sekretariet na kamati ya siasa.

Mamlaka zifuatilie kwa ukaribu hawa wananchi ambao wanatishiwa maisha na huyu aliyewahi kuwa Mbunge wa Tandahimba ambaye kwa sasa amepoteza mvuto.

Pia nashauri mgombea aliyeongoza kura za maoni alichukue hili na alifanyie kazi kuona namna ambavyo wananchi wa jimbo lake wasiishi kwa hofu kwaajili ya kumuhofia mtu mdogo ambaye alikuwa anauishi ubunge kwa masilahi yake.

Naomba kwa leo niweke mezani.
 

Attachments

  • IMG-20200730-WA0042.jpg
    IMG-20200730-WA0042.jpg
    95.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom