Katanga amemuongezea CAG watumishi 104 ili zoezi la ukaguzi wa fedha za Uviko likamilike haraka!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,550
141,358
KMK mh Hussen Katanga amemuongezea CAG watumishi 104 ili kuongeza kasi ya ukaguzi wa fedha za Uviko katika maeneo mbalimbali .

Naye CAG mh Charles Kicheere amesema wanafanya ukaguzi makini kwa kila shilingi iliyotumika na hakuna sehemu hata moja ambayo haitaguswa na ukaguzi huo maalumu kabisa.

Source: Eatv

Maendeleo hayana vyama!
 
Zamani kidogo wale wakurugenzi wajanja wajanja ndio walionekana watendaji wazuri kwa kuwa ndio walikuwa wanakubalika sana kwa Madiwani kwa kuwa wanawapa zabuni kinyume cha utaratibu, Anapata mafungu makubwa na kwa wakati kwa kuwa anajiongeza kwa wagawaji na wakija wakaguzi anawasaidia kuandaa Hati safi kwa Halamshauri yake

Wale wazalendo anawakomalia Madiwani nao wanamuanzishia zengwe…kule Serikali kuu hajiongezi matokeo yake miradi inakwama kwa kukosa fedha na wakija Wakaguzi wanamchapa hati chafu na ikija ile Kamati ya LAAC ya Bunge inamlipua

Tumetoka mbali sana kwa kweli

Unaweza ukaja ukaguzi wa kumkagua CAG kama alivyofanya Spika Ndugai by then!
 
Nilicho na hakika nacho ni kuwa Tanzania imepata Rais ambaye sio na hana hulka ya wizi. Kilele cha mafanikio yake aliyojiwekea kimepitiliza hivyo hana sababu ya kutoandaa hatima yake kwa Mungu. Hili Jambo mlielewe vizuri sana watanzania.
 
KMK mh Hussen Katanga amemuongezea CAG watumishi 104 ili kuongeza kasi ya ukaguzi wa fedha za Uviko katika maeneo mbalimbali .

Naye CAG mh Charles Kicheere amesema wanafanya ukaguzi makini kwa kila shilingi iliyotumika na hakuna sehemu hata moja ambayo haitaguswa na ukaguzi huo maalumu kabisa.

Source: Eatv

Maendeleo hayana vyama!
Maigizo yale yale ya miaka yote
 
Wakaguzi waliofika Buchosa DC walikuwa wanakagua document tu field walikuwa wanafika dakika 5 wanasepa.

Majengo hayajakamilika vioo havijawekwa meza na viti vingine vimeanza kuvunjika kwani vimechomelewa kimagumashi.

Rangi za kuta zimepakwa kimagumashi kama kupaka shoe polish kwenye kiatu. Bank statement za mashule mengine zanaonyesha pesa ilikuwa inatokea account binafsi za wakuu wa shule na sio wazabuni.

Mbaya zaidi ni wakaguzi wamekwenda kuonana na wakuu wa shule kingali kamati za ujenzi hawakuziona na hao ndo wanajua wakurugenzi na wakuu wa shule walivyotafuna pesa. Hii nchi inaliwa sana.
 
Hao watumishi 104 watalipwa tena? Au wanajitolea
 
Hapo watu wanapiga perdiem wakitoka wanapitia kwa DT maisha yanaenda
 
Back
Top Bottom