Katambi: Serikali imetenga Milioni 100 kuwalipa watoa taarifa za uhalifu nchini

Nimeisha toa tarifa na malalamiko sasa yapata mwaka ila akuna hatua za kisheria wanazo chukulia walifu licha ya kulalamila raia wa kigeni wana shirikiana na wazawa kuiba ardhi ya taifa ila wapi ni udhuni sana kwa taifa anitafte mimi nimpe ushaidi A.z sijapata haki yangu nikidai haki nakandamizwa washitakiwa kwa kuonga wako vema nisha sambaza barua kila ofisi sikapewa majibu wal haki
Mkuu pole sana 🙏
 
Majizi, mafisadi, Mahujumu uchumi yapo huko huko, lakini kwa sababu tunawaona Watanzania kama Nguchiro ndo maana eti tunawaomba walete taarifa. Taarifa gani kama hata waliotajwa na CAG ambao wanafahamika kabisa hawajachuliwa hatua?

Mungu si Athumani, ipo siku tutaelewana.
Hawa jamaa huwa wanatuona sisi ni mapoyoyo
 
Hivi unasifu nini hapo kama siyo ushabiki usio na macho? Hili tangazo la milioni 100 ni usanii mwingine wa kusahaulisha watu ukweli uliopo. Unampongeza waziri anayeahidi fedha, huku serikali hiyohiyo ikitishia kuwapoteza watoa taarifa mitaani?
Tukiongelea uhalifu na amani ya nchi, mbona serikali haidhibiti wezi wa mabilioni ya umma wanaotajwa kila kukicha kwenye ripoti za CAG? Ripoti za CAG zinatoka, ufisadi wa kutisha unaonyeshwa wazi, lakini hakuna hatua yoyote kwa sababu hata Rais mwenyewe alishabariki uhalifu huu wa kalamu kwa kauli yake ya 'kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake'! Huu ni ushahidi wa wazi kuwa wakubwa wameruhusiwa kupiga mabilioni wanavyotaka, kisha wanakuja kutuzuga wananchi na maigizo ya kugawa zawadi. Katambi kama Waziri wa Mambo ya Ndani atwambie hadi leo nani alihusika na mauaji ya Oktoba 29? Watanzania sasa hivi tumeshashtuka, tunajua ipi ni sinema na upi ni ukweli!
Mkuu uko enlightenment thinkers sana 🙏 ✅.

Kuelekea u,u tutaona mengi
 
Acha
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Serikali imetenga Shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuwazawadia wananchi watakaotoa taarifa sahihi zitakazosaidia kubaini na kuzuia vitendo vya uvunjifu wa amani nchini. Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama katika kulinda amani, usalama na utulivu wa nchi.

Aidha, Katambi amesema taarifa zitakazotolewa zitahifadhiwa kwa usiri mkubwa, huku watoa taarifa wakilindwa kwa mujibu wa sheria za ulinzi binafsi na sheria za kulinda watoa taarifa. Amefafanua kuwa kiwango cha zawadi kitategemea uzito na umuhimu wa taarifa husika, ambapo taarifa itakayothibitika kuwa ya kweli itastahili malipo yasiyopungua Shilingi milioni tano.

Acha utani na mambo serious......usalama na ulinzi wake .....weka bil 3 hivi mambo ni mengi sanaaa
 
Kwa sababu ya ugumu wa maisha uliopo mtaani kwa sasa, kuna hatari kubwa ya watu kutengeneza taarifa za uongo au "kuwasingizia" maadui zao wa kibiashara au kisiasa ili tu wapate hiyo Shilingi milioni kadhaa.
Ndio maana mimi nasisitiza kuwa taarifa lazima zithibitike kuwa za kweli badala ya kuwa propaganda za kisiasa.
Umesema kweli kabisa mkuu MKANGAFFU, naunga mkono hoja yako kwa 100%.
Mazingira ya ugumu wa maisha yakichanganyikana na njaa, yanatengeneza hatari kubwa sana mtaani. Hawa wasaka tonge na watu wasio na uaminifu watatumia fursa yoyote ya zawadi za fedha kuwasingizia na kuwazushia majungu maadui zao wa kibiashara au kisiasa ili tu wapate hizo shilingi milioni kadhaa. Ndio maana nasisitiza sana kuwa taarifa lazima zithibitike kwa ushahidi thabiti badala ya kuendekeza propaganda za kisiasa na kutafuta kiki za kijinga.

Kama mfano hai wa hili ninachokisema, hebu tuangalie kule Pakistan kwenye sheria yao ya blasphemy. Kule watu wengi sana wamepoteza maisha, kushambuliwa, au hata kuhukumiwa kunyongwa mahakamani kwa ushahidi wa uongo wa maneno tu. Mtu anakutuhumu tu kwa visasi vyake binafsi au vya kibiashara, unakamatwa na kusulubiwa bila uchunguzi makini wa kisayansi.

Huu ndio uhalisia kwamba mifumo ikikosa umakini, inakuwa silaha ya kuangamiza wasio na hatia. Hawa mawaziri wetu wa kuokoteza wanaopenda kupiga denda na sifa za kijinga za kisiasa lazima serikali ijiangalie sana nao. Wasikurupuke kuweka mifumo itakayowapa watu mwanya wa kulipiza visasi na kutengeneza majungu mtaani kwa sababu ya njaa zao. Lazima kuwepo na uchunguzi thabiti na huru (vetting) kabla ya kuchukua hatua yoyote.

Mwisho kabisa, bado nahoji sana umakini wa uchunguzi wao. Kama serikali hii hii tangu mwaka 2017 haijawapata waliompiga risasi Mhe. Tundu Lissu, na wale wauaji wa Oktoba 29, ndiyo tuiamini leo kama itafanya uchunguzi kwa uwazi? Ama mfumo huu utakuja kuwa silaha tu ya kuwafunga wapinzani kisiasa kwa kuwatumia machawa na vikosi vya propaganda kutuhumu watu ovyo mtaani?
 
Acha

Acha utani na mambo serious......usalama na ulinzi wake .....weka bil 3 hivi mambo ni mengi sanaaa
Uko sahihi kabisa mkuu Lambardi. Masuala ya usalama yanahitaji hiyo bilioni 3, lakini tukubali kuwa kuna uzembe mkubwa sana kwenye wizara ya Waziri Katambi. Haya matukio ya mauaji na watu kupotea hovyo yamekithiri, na serikali inajua fika kuwa imesimama ukutani. Hatua hii ya sasa ni mkakati wa makusudi kabisa wa kuhamisha ajenda ili kuwapoza wananchi na kukwepa lawama za jumuiya za kimataifa. Wanataka kututoa kwenye reli, lakini safari hii tunahoji uwajibikaji!
 
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Umenena vyema CHIEF PRIEST! Kwenye nchi ambayo msemo wa 'kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake' umegeuka kuwa utaratibu wa kijumla, kila taasisi inajiongoza yenyewe. Huu uzembe unajidhihirisha zaidi kwenye wizara ya Katambi, ambako mauaji na watu kupotea hovyo vimekuwa jambo la kawaida, huku wakijaribu kila mbinu kuhamisha mjadala wa umma. Kibaya zaidi, mfumo huu unatumia njaa kama silaha; watu wanapewa vipesa kidogo wanashangilia, na sitashangaa kuona hata wachache kati ya wale 'Critical Thinkers' wa JamiiForums wakiangukia huko kwa ulafi wa matumbo yao. Kiukweli, kuunga mkono CCM kwa sasa inahitaji akili ya mwenda wazimu! 🤷‍♂️
 
Nakubaliana sana mkuu ....uko sahihi sana....Waziri alietolewa Simbachawene hakutaka huu upuuzi.....alicheza nje mfumo.....ina maana serikali lao moja...
 
Tajeni waliouza twiga UAE mpewe pesa
 
Umenena vyema CHIEF PRIEST! Kwenye nchi ambayo msemo wa 'kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake' umegeuka kuwa utaratibu wa kijumla, kila taasisi inajiongoza yenyewe. Huu uzembe unajidhihirisha zaidi kwenye wizara ya Katambi, ambako mauaji na watu kupotea hovyo vimekuwa jambo la kawaida, huku wakijaribu kila mbinu kuhamisha mjadala wa umma. Kibaya zaidi, mfumo huu unatumia njaa kama silaha; watu wanapewa vipesa kidogo wanashangilia, na sitashangaa kuona hata wachache kati ya wale 'Critical Thinkers' wa JamiiForums wakiangukia huko kwa ulafi wa matumbo yao. Kiukweli, kuunga mkono CCM kwa sasa inahitaji akili ya mwenda wazimu! 🤷‍♂️
Mtaji wa CCM ni Ujinga na umasikini wa walio wengi ndiyo maana wakipewa vijisenti kidogo tu wanakuwa machawa wakiamini hivyo vijisenti ndiyo vitamaliza umasikini wao.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Serikali imetenga Shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuwazawadia wananchi watakaotoa taarifa sahihi zitakazosaidia kubaini na kuzuia vitendo vya uvunjifu wa amani nchini. Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama katika kulinda amani, usalama na utulivu wa nchi.

Aidha, Katambi amesema taarifa zitakazotolewa zitahifadhiwa kwa usiri mkubwa, huku watoa taarifa wakilindwa kwa mujibu wa sheria za ulinzi binafsi na sheria za kulinda watoa taarifa. Amefafanua kuwa kiwango cha zawadi kitategemea uzito na umuhimu wa taarifa husika, ambapo taarifa itakayothibitika kuwa ya kweli itastahili malipo yasiyopungua Shilingi milioni tano.

Haya Lucas Mwashambwa na viroboto wenzako kuna fungu huko changamkieni.
 
Tajeni waliouza twiga UAE mpewe pesa
Kifo cha utata cha marehemu Stan Katabalo baada ya kulipua kashfa ya Loliondo kinathibitisha nguvu ya mtandao huu. Mbaya zaidi, tangu Katabalo aondoke, tasnia imeingiliwa na njaa. Waandishi wa sasa wamekimbilia uchambuzi wa mpira kwa woga, na wale waliobaki kwenye siasa kazi yao ni kuwa wasifiaji wa CCM na serikali yake. Labda ukimtoa mzee wetu Pascal Mayalla mwana JF mwenzetu kwa ujasiri wake wa kutega viongozi kwa maswali ya akili. Hawa waandishi wa michezo, ukiona wanavyokaza mishipa ya shingo kuwawajibisha kina Mangungu na Hersi utadhani ni mashujaa wa habari, kumbe ni paka tu waliojivisha manywele ya simba. Wanapiga kelele kwenye soka kwa sababu wanajua hakuna risasi wala utekaji, lakini kwenye siasa zote zinalala! 🧠
 
Takataka kama Balile ni aibu kubwa kwa tasnia hii .
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Serikali imetenga Shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuwazawadia wananchi watakaotoa taarifa sahihi zitakazosaidia kubaini na kuzuia vitendo vya uvunjifu wa amani nchini. Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama katika kulinda amani, usalama na utulivu wa nchi.

Aidha, Katambi amesema taarifa zitakazotolewa zitahifadhiwa kwa usiri mkubwa, huku watoa taarifa wakilindwa kwa mujibu wa sheria za ulinzi binafsi na sheria za kulinda watoa taarifa. Amefafanua kuwa kiwango cha zawadi kitategemea uzito na umuhimu wa taarifa husika, ambapo taarifa itakayothibitika kuwa ya kweli itastahili malipo yasiyopungua Shilingi milioni tano.

Kwanini mnatumia Kodi za wananchi vibaya kwa kiwango hiki? Shame on you!
 
Nyie WAHUNI sana mbona ndogo sana!!!

Yaani per diem yenu principal officer per day 390,000 ,halafu watoa taarifa milioni 100
 
Uhalifu wa kwanza ni kutenga million mia kulipa wakuda bila sababu za msingi. Taarifa za uhalifu dhidi ya jamhuri kupitia wabadhirifu wa mali za umma anazosoma CAG kila siku zimefanyiwa lini kazi na wapi?
 
Back
Top Bottom