Katambi amepotoka, anahitaji toba

Kama ni kweli kasema hii maneno
Naamini wenye Chama Chao na serikali hawatavumilia hii choko choko
CCM ni Chama cha watu makini
 
Kwa kauli hiyo,alipaswa awajibike kwa kuomba radhi na kujiuzulu.
Mpuuz sana
 
Naibu Waziri anayehusika na mambo ya Ajira sijui na Nini vile, amejitokeza na kuwalaumu vijana wenzake kuwa ni walalamishi na wanachagua Ajira! Sina tatizo na Hilo ila tatizo langu ni wapi zilipo Ajira ambazo vijana walipewa wakazigomea?

Ni ujinga na kujilisha upepo kuona au kuwadharau vijana ambao Leo hii yeye akiondoshwa hapo hatakua na Cha kufanya.

Kuna PhD holder alikua RC Morogoro, alivyotumbuliwa akaanza kulalamika kuwa family nzima inategemea yeye! Sasa huyo ni PhD holder, je hali ikoje kwa vijana? Ni kweli tuna vijana wavivu?

Kuna vijana walikua wanashinda ONLINE wanafanya kazi mbalimbali ONLINE na walikua wanalipwa vizuri tu, akatokea Mpuuzi huko huko CCM akasema hakuna kufanya malipo kwa PayPal sijui na Nini Ile. Vijana wengi Ajira zikafa.

Hawajapona vizuri akatokea kichaa mwingine akaongeza Bei ya bundle kwa 50%. Yaani wakati ulimwengu unapunguza gharama za bundle Tanzania wanaongeza gharama Kisha anatokea mwendawazimu mmoja anawalaumu vijana. Dah!

Usimlaumu Katambi kwani juzi kati Samia alisema Nini kuhusu vijana na ajira?
Mbona hamkumwambia aombe radhi?
 
Kwa nafasi yake anapaswa kuja na mikakati kamambe ya namna gani atawakwamua vijana wenzake na ukosefu wa ajira na sio tofauti na hivyo.
 
Naibu Waziri anayehusika na mambo ya Ajira sijui na Nini vile, amejitokeza na kuwalaumu vijana wenzake kuwa ni walalamishi na wanachagua Ajira! Sina tatizo na Hilo ila tatizo langu ni wapi zilipo Ajira ambazo vijana walipewa wakazigomea?

Ni ujinga na kujilisha upepo kuona au kuwadharau vijana ambao Leo hii yeye akiondoshwa hapo hatakua na Cha kufanya.

Kuna PhD holder alikua RC Morogoro, alivyotumbuliwa akaanza kulalamika kuwa family nzima inategemea yeye! Sasa huyo ni PhD holder, je hali ikoje kwa vijana? Ni kweli tuna vijana wavivu?

Kuna vijana walikua wanashinda ONLINE wanafanya kazi mbalimbali ONLINE na walikua wanalipwa vizuri tu, akatokea Mpuuzi huko huko CCM akasema hakuna kufanya malipo kwa PayPal sijui na Nini Ile. Vijana wengi Ajira zikafa.

Hawajapona vizuri akatokea kichaa mwingine akaongeza Bei ya bundle kwa 50%. Yaani wakati ulimwengu unapunguza gharama za bundle Tanzania wanaongeza gharama Kisha anatokea mwendawazimu mmoja anawalaumu vijana. Dah!

Huyu jamaa nilikuwa namkubali sana kipindi tupo chuo shycom kampeni za uchaguzi mkuu ubunge Kati masele(ccm) vs marehemu shelembi (chadema),ila sasa nimeamini hakuna mkate mgumu mbele ya chair,amekuwa mtu wa kutukejeli vijana kuhusu ajira kweli? Aaa 2025 hatoboi kabisa ndani tu ya ccm humohumo,ovyo kweli,si ageongea mengine tu nasi kutukejeli ase!
 
Katambi Ni msaliti Kama Waitara, Mashinji, Silinde na ma reject wengine Kama covid 19.
Come 2025 mwenye kiti chake Kama hatapata uspika Basi katambi atafute ajira
 
Mojawapo ya Jukumu la Wizara ya Kazi na Ajira ni kuhakikisha kunakuwa na Mazingira wezeshi ya Ajira kwa wote wenye sifa za Ajira,haki na wajibu wa mfanyakazi.

Kwa kuanzia Mh. Naibu Waziri angelisaidia mchakato wa kurasimisha baadhi ya Ajira zisizo rasmi zinazoajiri vijana wengi ili waweze kupata Mikopo ya kujikwamua, kuajili wengine na kukuza mitaji mfano.. Kazi zote za ufundi na viwanda vidogox2.

Mh. Naibu Waziri tunaomba ufanye utafiti wa tatizo la Ajira ili utape uhakika wa hali halisi mtaani,vijana wengi wanahitaji msaada wa elimu ya ujasiriamali,utunzaji wa fedha na namna ya kuanzisha na kukuza mitaji mikubwa ya biashara.

Kama Wizara andaeni semina,warsha,makongamo na watembeleeni Vijana sehemu za kazi ili mpate kutatua changamoto zinawakabili.
 
Yeye hayamhusu hayo
 
Yule jamaa wa salenda atakua role model wa vijana wengi mbeleni!

Nyie kuleni kuku kwa mrija tuu
Ipo siku hayo matumbo yenu

Hapo ndipo wataheshimiana!

Hata kama uprisings nyingi wanazizima kwa nguvu lakini hazitawaacha salama baadae

Be careful with the youth
Kutoa ajira ni Kazi ya Serikali
Serikali lazima itengeneze mazingira wezeshi na lazima muajiri mtake msitake

Jifanyeni tuu mnavaa magold na maujinga mengine mikononi mwenu na kwenye hayo mashingo yenu!

Mataifa yanayojitambua yanaumiza kuwapa raia wake ajira na sometimes wanatengeneza hadi Mazingira wezeshi nje ya nchi zao
Ila huku Kijana mmoja Anaona ana akili sana Hahahahaa!

Sisi tumezeeka sasa
 
Katambi chukua hii usiropoke kuwalaumu vijana hali serikali ndio chanzo cha tatizo la ajira nchini.

Ndani ya miaka 3 jinsi ya kuleta maendeleo na kumaliza tatizo la ajira nchini.

1.Ondoa futa kodi zote za kuingiza magari ya mizigo na abiria nchini kodi yake utaipata mara mbili yake kupitia indirect tax.Kwenye mafuta,leseni za udereva,fine za traffic, parking fee,ushuru wa stand,spare za magari,leseni na vibali mbalimbali.Gari moja uajiri si chini ya vijana 3.

2.Toa ruzuku kwenye viwanda vya kuzalisha matrekta wazalishe matreka mengi waje watuuzie wakulima kwa robo bei trekta moja uajiri zaidi ya watu wanne.

3.Jenga schemes za umwagaliaji KILA kijiji upitapo mto pande zote mbili watu walime mwaka mzima ni aibu sana kwa maji ya mito kumwaga maji yake baharini badala ya mashambani.Soko la mazao nje ya nchi lipo tele

4.Jenga vyuo vya ujuzi kila kata kopesha vijana ujuzi baada ya kumaliza darasa la saba wakapate ujuzi wautakao.

Kukopesha vijana waende chuo kikuu kisha warudi mtaani kuendesha bodaboda na kuwa machinga ni upotevu Mkubwa Sana wa kodi zetu na kuongeza idadi ya masikini nchini.

5.Fungua mipaka watu wauze watakapo nje ya nchi kuna masoko tele.Legeza masharti ya vibali Ili export ikue.

Ni sekta mbili tu zingine takataka hazifikii kilimo na madini kwa kuajiri vijana wote nchini na kuongeza pato la taifa bila kutegemea kukopa na kukamua kodi wananchi.

6.Peleka KILA kijiji mashine za kutengeneza interlocking block na vigae Ili watz wote wajenge nyumba bora kwa gharama nafuu kabisa

Mjerumani kwa miaka 15 alituletea maendeleo makubwa Sana ccm imeshindwa nini.
 
Amekosa hekima hana busara ni ajira zipi alizotoa vijana wakazikataa. Aache kujipendekeza afanyekazi.
 
Back
Top Bottom