Kata ya Nanjara-Reha; "Mchanga ni mwingi kuliko mawe", hongera CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kata ya Nanjara-Reha; "Mchanga ni mwingi kuliko mawe", hongera CDM

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Tuko, Oct 29, 2012.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kama kuna sehemu Tanzania hii ambapo nguvu ya pesa hutumika kuibeba CCM, ni katika tarafa ya Tarakea, ilimo kata ya Nanjara - Reha.
  Msemo "Mchanga ni mwingi kuliko mawe" ni msemo maarufu katika kata hii kwenye ishu za siasa. Baada ya kuona upepo umeanza kuwaendea vibaya, CCM ilianza kuwatumia matajiri wake wa Tarakea, wakiwemo akina Michael Shirima (mwanzilishi na biggest shareholder wa precision air na akimiliki biashara nyngine ndani na nje ya nchi), Bw Waha, anayemiliki biashara kadhaa Dar (ikiwemo Rombo green view Hotel-shekilango), Bw Maulid Swai (fogo wa Tarakea), na wengine wengi wa Dar, Moshi Arusha na kwingineko ambao ni wazawa wa Tarakea. Kinachonifurahisha katika kata hii ni kuwa wananchi wa kipato cha chini, wakijifananisha na mchanga, wameamua kuwaumbua matajiri wakubwa (wakiwafananisha na mawe) na ndio chimbuko la huo msemo Waache wao waje na hela zao, lakini siku ya kura tutaona 'mchanga na mawe kipi kingi'...

  Kata ya Nanjara-Reha ilibaki wazi baada ya diwani aliyekuwapo (Bw Mnene), kushindwa kukubali kuwa degraded kutoka kuwa jiwe, hadi kuwa chembe ya mchanga. Huyu jamaa (ambaye kwa kiasi fulani ana vijihela), baada ya kushinda udiwani 2010, alishuhudia hujuma kubwa katika biashara zake, ambapo ndani ya mda mfupi alijikuta gari zake zote za mizigo zimepaki polisi zikikamatwa kwa makosa ya ajabu ajabu, pamoja na kuhujumiwa kwa biashara zingine, then akaona anauelekea umasikini, akaamua aandike barua ya kujivua udiwani kwa hiari yake. CCM walidhani akiingia hapo 'chembe ya mchanga' hataweza kupambana na 'mawe' akashinda, but wamekuwa surprized. Poleni sana kina Mramba, na kina Mchomba na mafisadi papa wengine...
   
 2. M

  Magesi JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa mkuu lakini umemsahau fisad na fyatu mzinz anazin mpaka na watoto wke wa kuzaa diwan wa Keryo Flavian Marandu
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mkuu, fogo maana yake nini ??
  kuna umbali kati ya tarakea na nanjara nakumbuka niliwahi kupita barabara ya rombo vumbi lilikuwa lakuua mtu.
   
 4. josefast

  josefast JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  nanjara ni mitaa yote ya kbaoni P/s + nanjara sec + namfua sec. Pale kuna mzee Eliuta Silayo aka Mbuya yule mzee naye alikwepo mangiii
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Fogo ni jina la mtaani Rombo likimaanisha Tajiri.

  Wafanyabiashara wa magendo wako close na CCM huku wakinyanyasa hovyo vijana

  Jeshi la polisi Rombo limewekwa mfukoni mwa matajiri

  Soon tutakomesha hii cartel
   
 6. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  tarakea ni chachu ya mabadiliko kwa rombo nzima...... Vijana, wazee .... Wengi ni chadema.

  Ushindi wa mbunge selasini ulitoka tarafa ya tarakea.

  Kesho j4 bwana vasco da gama anaenda kuzindua barabara ya lami pale tarakea.

  Vijana na wazee wanamsubiri wasikie ana waambia nini
   
 7. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Jana ulishuhudia JK mwenyewe akizindua lami, eti? Kinachonifurahisha ni kuwa lami imejengwa kwa 'wapinzani' kwa kutumia ela za walipa kodi wa Tanzania, wakiwemo 'chama tawala' wengi huko Ifakara, Matombo, Ileje, Kilindi, makambako, Nachingwea na kwingineko ambako bado wanakula vumbi... Kweli 'upinzani' unalipa...
   
Loading...