Kasulu, Kigoma: Watu wanne wa familia moja wauawa kwa kukatwa na panga

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Watu wanne wa familia moja ambao ni wakazi wa Mtaa wa Katandala Kata ya Msambara Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma, wameuwawa kwa kukatwa katwa na mapanga na watu wasiofahamika pamoja na kubomolewa nyumba yao.

Ni majonzi na simanzi kubwa kwa wana familia ya Petro ambayo imepoteza wazazi na ndugu zao ambao wamepatwa na mkasa mzito wa kukatwakatwa na mapanga hadi kusababisha vifo vya baba wa familia Petro Segarika anayekisiwa kuwa na umri wa miaka 70 na mkewe Suzana Mkuka (55) pamoja na watoto wao wawili Alphonce Petro anayekisiwa kuwa na umri wa miaka 28 na Aniza Petro (35) ambaye yeye alikuwa ni mjamzito.

Wakizungumzia mauaji hayo Isaya Petro na Daudi Petro ambao ni watoto wa marehemu mzee Petro Segarika wanaeleza kuhusu tukio hilo.

Mara baada ya tukio hilo kutokea polisi waliwasili na walichukua miili ya marehemu kwa uchunguzi na baada ya hapo walikabidhi miili hiyo kwa wanafamilia kwa ajili ya mazishi, ambapo licha ya uchunguzi huo bado chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika, huku baadhi wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

Diwani wa Kata ya Msambara Evans Lucas, amesema familia ya marehemu na wananchi wengine wanasubiri kuona vyombo vya dola vikifanya kazi yake, huku Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Simon Anange, akithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
 
Hiyo nyumba ilikuea mbali Sana na wakazi Wengine kiasi kuwa Hadi inabomolewa hakuna jirani aliyeongoza au kusikia walau apige yowe?

Upelelezi uanzie kwa majirani.Je aliishine na hao majirani?

Pili kubomoa nyumba hakuna uhusiano wowote na mgogoro wa Ardhi hapo au popote Kati ya marehemu na mtu yeyote?

Tatu marehemu shughuli zake hasa zilikuwa zipi na alikuwa akizifanyia wapi Hakuna tatizo lolote kwenye shughuli zake na mtu yeyote? Kuwa labda kulikuwa kudhulumia nk?

Nne je labda aliwahi kuwa na kesi na yeyote?

Tano hao Wengine nao je hawajawahi kiwa na kesi ,uhasama nk na yeyote?
 
Mwongozo mzuri. Maana polisi / jamii wanaweza kuishia kusema ni imani za kishirikina tu bila upelelezi wa kina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom