KASULU, KIGOMA: Polisi yakamata risasi 408 zikimilikiwa na mtu mmoja

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
776
1,330
JESHI la polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kukamata risasi 408 za bunduki zilizokuwa zikimilikiwa na Mtu mmoja ambaye jina lake halikutajwa mkazi wa Kijiji cha Makere Wilayani kasulu Mkoani Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake leo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma, DCP Fredinand Mtui alisema mnamo tarehe 5 Desemba majira ya 08:20 huko maeneo ya makere Center katika kijiji cha Makere askari wakiwa doria walipokea taarifa kutoka kwa raia wema wanaochukia uhalifu kuwa kuna mtu wana wasiwasi nae kuwa ana mzigo usio kuwa wa kawaida.

Mtui alisema Askari walianza ufuataliaji na kufanikiwa kukamata mtuhumiwa mmoja ambaye jina lake limehifashiwa kwa shughuli za kiusalama, alipo fanyiwa upekuzi mtuhumiwa huyo katika Sanduku lake alilokuwa amebeba alikutwa akiwa na risasi 408 za bunduki aina ya SMG/SAR alizokuwa amezifunga ndani ya nguo zake.

Aidha Mtui alisema upelelezi bado unaendelea, Mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria pindi upelelezi utakapo kamilika ilikutoa fundisho kwa wananchi wengine wanao nunua silaha kwa lengo la kufanyia uhalifu.

"Nichukue fursa hii kuwaasa wahalifu wanaojihusisha na biashara ya kuuza na kununua risasi na silaha nyingine waache biashara hiyo, wafanye kazi nyingine ambazo zinatambulika kisheria vyombo vya ulinzi na usalama viko imara kuwatafuta wahalifu hao na kuwachukulia hatua za kisheria,"alisema Mtui.

WhatsApp Image 2016-12-07 at 03.12.27.jpeg

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma,DCP Fredinand Mtui akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusiana na tukio hilo la kukamatwa risasi za moto 408,zilizokuwa zikimilikiwa na mtu mmoja mkoani humo.
WhatsApp Image 2016-12-07 at 03.12.25.jpeg

Risasi 408 za bunduki zilizo kuwa zikimilikiwa na Mtu mmoja ambaye jina lake halikutajwa, mkazi wa Kijiji cha Makere Wilayani kasulu Mkoani Kigoma.
 
Mwacheniii bana hioonifursaa napengine ziemkamatwa 600+ zingine wametumia fursa
 
Back
Top Bottom