Kasulu, Kigoma: Mbunge Josephine Ngezabuke (CCM) apata ajali mbaya, gari lake laua mtoto

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mbunge viti maalumu mkoa wa Kigoma Josephine Ngezabuke (CCM) amepata ajali mbaya ya gari akitokea Kakonko katika kijiji cha Mvugwe wilayani Kasulu mkoani Kigoma Jana majira ya saa kumi na moja jioni.

Hali ya mbunge huyo inaripotiwa sio nzuri, hata hivyo katika ajali hiyo aligongwa mtoto mdogo ambaye ni mwanafunzi na alifariki papo hapo.

Majeruhi wengine ni Dereva wa CCM Wilaya ya Kasulu (Mzee Saidi) na Diwani mmoja wa viti maalum.

Mbunge huyo amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kasulu, inaelezwa kuwa atakuwa ameathirika zaidi Mgongoni na kwamba hawezi hata kukaa.

Hata hivyo kesho Ofisi ya bunge inamtumia ndege maalum kwaajili kumsafirisha Hospitali kuu ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
 
Mwenyezi Mungu ampiganie na apate matibabu haraka ili aweze kupona na pia pole sana kwa Familia ya huyo Mtoto aliyepoteza maisha na Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
 
Hawa wabunge wa ccm wamekutwa na masahibu gani ajali za karibukaribu na vifo vya watoto kwenye ajali hizo!?
 
mbona hii habari ni ya tangu wiki jana, naona umeipost kama imetokea leo
 
Back
Top Bottom