Kassim Majaliwa: Wanasiasa waeleze yale watakayoyafanya kwenye kampeni na sio kubeza yaliyofanywa na wengine

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,524
9,325
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu mara kampeni za uchaguzi mkuu zitakapofunguliwa ili kuepuka vurugu zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

Akizungumza katika ibada ya siku kuu Eid Al Adha Jijini Dar es Salaam, Majaliwa amesema kuwa ni muhimu kwa wanasiasa kueleza yale waliyopanga kuwasaidia wananchi kuliko kubeza yale yaliyofanywa na wengine na kukashfu.

“Tujiepushe na lugha za uchochezi, tujiepushe na lugha za bezo, tujiepushe na lugha za kashfa kazungumze kile ambacho utawatendea wananchi” amesema Majaliwa

Waziri Mkuu pia amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuimarisha amani na mshikamano nchini kwa kutoa mawaidha mazuri yenye lengo la kujenga jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa Taifa.

Akielezea kuhusu hayati Benjamini Mkapa ,amesema kuwa waislamu watamkumbuka kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha waislamu kwa kutoa majengo ya Serikali na kukabidhi kwa waislamu na hivyo kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho kilichopo mjini Morogoro.

Ippmedia.com
 
Nakazia hapo,maana imekuwa kama watu wanawadharau wapiga kura,na kudhani hawaoni.
 
Mm nitabeza Sana tu. Naanza na ununuzi wa madege yasiyokuwa na faida. Popo tu ndiyo wanafaidika kwa kupata sehemu nzuri ya kuzalia.

Nitabeza kauli potofu za mwenyekiti wa ccm zinazoligawa taifa. Unaogopa nn kwan wewe Majaliwa ikiwa mnatamba kwamba serikali hii imefanya maajabu mengi?
 
Asipangie watu cha kuongea kwenye kampeni. Kila siku tunasikia rais wetu akibeza mambo ya hovyo yaliyofanyika awamu zilizopita, ni kwanini yeye awazuie watu wengine kuyasema ya hovyo ya awamu hii? Inaonekana awamu hii inataka kampeni zifanyike kwa utashi wa rais aliye madarakani.
 
Tumekuwa tunawaambia sana kwenye vikao vyetu kuwa tusiishi kwa uongo kwani tutaaibika wakati ukifika wa kuweka mezani hesabu!

Sasa ona tunahangaika kubembeleza wasitukashifu na kubeza? Kampeni gani hiyo ya kupangiana maneno ya kuongea?
Kanuni zipo na zinakataza matusi tuu sio kupigana vijembe kama tumechemsha.

Miaka mitano tumeongea peke yetu sasa mbona tuna hofu?
 
Kanuni zipo na zinakataza matusi tuu sio kupigana vijembe kama tumechemsha. Miaka mitano tumeongea peke yetu sasa mbona tuna hofu?
Hahahaha
 
Mm nitabeza Sana tu. Naanza na ununuzi wa madege yasiyokuwa na faida. Popo tu ndiyo wanafaidika kwa kupata sehemu nzuri ya kuzalia.

Nitabeza kauli potofu za mwenyekiti wa ccm zinazoligawa taifa. Unaogopa nn kwan wewe Majaliwa ikiwa mnatamba kwamba serikali hii imefanya maajabu mengi?
kwan ndani ya nyumba yako au chumba chako kuna vingne umenunua lakini hujawahi kuvitumia..kwahiyo kuwa na ndege sio lazima upande ww tu hamna wenye mawe watapanda mkuu...kila kitu kwenye nchi kinahtajika ili kuimarisha ustawi wa taifa kwa ujumla
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu mara kampeni za uchaguzi mkuu zitakapofunguliwa ili kuepuka vurugu zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

Akizungumza katika ibada ya siku kuu Eid Al Adha Jijini Dar es Salaam, Majaliwa amesema kuwa ni muhimu kwa wanasiasa kueleza yale waliyopanga kuwasaidia wananchi kuliko kubeza yale yaliyofanywa na wengine na kukashfu.

“Tujiepushe na lugha za uchochezi, tujiepushe na lugha za bezo, tujiepushe na lugha za kashfa kazungumze kile ambacho utawatendea wananchi” amesema Majaliwa

Waziri Mkuu pia amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuimarisha amani na mshikamano nchini kwa kutoa mawaidha mazuri yenye lengo la kujenga jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa Taifa.

Akielezea kuhusu hayati Benjamini Mkapa ,amesema kuwa waislamu watamkumbuka kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha waislamu kwa kutoa majengo ya Serikali na kukabidhi kwa waislamu na hivyo kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho kilichopo mjini Morogoro.

Ippmedia.com
unampiga dongo "mzee baba?" ha ha ha ha
 
Tumekuwa tunawaambia sana kwenye vikao vyetu kuwa tusiishi kwa uongo kwani tutaaibika wakati ukifika wa kuweka mezani hesabu!

Sasa ona tunahangaika kubembeleza wasitukashifu na kubeza? Kampeni gani hiyo ya kupangiana maneno ya kuongea?
Kanuni zipo na zinakataza matusi tuu sio kupigana vijembe kama tumechemsha.

Miaka mitano tumeongea peke yetu sasa mbona tuna hofu?
Payback time man
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu mara kampeni za uchaguzi mkuu zitakapofunguliwa ili kuepuka vurugu zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

Akizungumza katika ibada ya siku kuu Eid Al Adha Jijini Dar es Salaam, Majaliwa amesema kuwa ni muhimu kwa wanasiasa kueleza yale waliyopanga kuwasaidia wananchi kuliko kubeza yale yaliyofanywa na wengine na kukashfu.

“Tujiepushe na lugha za uchochezi, tujiepushe na lugha za bezo, tujiepushe na lugha za kashfa kazungumze kile ambacho utawatendea wananchi” amesema Majaliwa

Waziri Mkuu pia amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuimarisha amani na mshikamano nchini kwa kutoa mawaidha mazuri yenye lengo la kujenga jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa Taifa.

Akielezea kuhusu hayati Benjamini Mkapa ,amesema kuwa waislamu watamkumbuka kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha waislamu kwa kutoa majengo ya Serikali na kukabidhi kwa waislamu na hivyo kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho kilichopo mjini Morogoro.

Ippmedia.com
Anajishtukia huyo.
 
Back
Top Bottom