Kassim Majaliwa: Niambieni ni nchi gani duniani Bunge huonyeshwa kwa saa 8?

Big point, Nimeishi marekani miaka zaidi ya mitano sijawahi ona bunge live kama ilivyokua hapa bongo, vyama vingine vimeo kweli kweli nao wameona pakutokea, stupid mind.
Kuish kwako marekani hakujakusaidia
 
Huyu alietoa kauli hii ndio anaitwa waziri mkuu wa Nchi!!! Hata hao wazungu anaowatolea mfano wangeisikia hii wangecheka sana. Hata kwenye kumbi za comedy hii lazima wacheke tu.
Mshaambiwa ccm ni ile ile tukawa wabishi
Haya sasa ndo waziri mkuu wetu huyo
 
Big point, Nimeishi marekani miaka zaidi ya mitano sijawahi ona bunge live kama ilivyokua hapa bongo, vyama vingine vimeo kweli kweli nao wameona pakutokea, stupid mind.
Hujawahi kuliona kwasababu hukutaka tu. Sio kuzuiwa na serikali.
 
Majaliwa ameshachuja.
Ameishiwa pumzi.

Ina maana huyo waziri mkubwa kabisa hajui kwamba kwa sasa bunge linaonyeshwa muda wa kazi.??
Tena asubuhi mpaka sa tano muda mzuri wa wakulima kuwa shambani. Cha ajabu ni kwamba bunge halirushwi muda ule wa saa kumi wakati watu wanakua wameshatoka kazini.
Viongozi wa serikali ni vipofu wasioona kuwa muda wa kazi ni asubuhi mpaka saa tisa na nusu tena bunge la CCM linaonyeshwa nusu ya muda wote wa kazi.
Halafu wanawazuia waandishi wa habari wasifanye kazi. Uchumi wa hii nchi utaporomoka ndani ya miaka michache ijayo kwa kuwa serikali inataka kudhibiti kila kitu kinyume na kanuni la soko huria.
Vyombo huru vinavyolipa kodi vinaangalia soko na maoni ya wateja wao. Kwa nchi yetu bunge lilikua linaheshimika kutokana na watu kulifuatilia kwa kuonyeshwa live.
Hata mpira wa ligi ya Uingereza inapata umaarufu na kupendwa kutokana na kuonyeshwa live.

Wapinzani wako wapi wanze sasa kuzunguka kwenye majimbo yao waliyoshinda na nchi nzima ili waweke bayana hoja zao zinazopotoshwa na wahariri wa bunge la CCM na pia waje kueleza njama hizi za CCM za kuzima jicho la habari linalomulika uovu wa mawaziri na udhaifu wa wabunge wa CCM. Njama zinazofanywa ili tu kuwaaminisha watu kuwa serikali ya awamu ya tano ni ya watu watakatifu kwa wao kuuza sura lakini wabunge wafiche sura zao.
Huku CCM hao hao leo wakijifanya kuwa hawaoni mambo mazuri aliyoyafanya JK awamu ya nne. JK pamoja na udhaifu na wizi uliokuwa unafanywa na mawaziri lakini aliruhusu waandishi wa habari kumulika popote.

Nafasi ya kuuza sura imebaki kwa serikali kwenye matamasha úyao yanayoonyeshwa muda wa kazi. Kuuza sura kumebaki pia kwa mawaziri wakati wa kujibu maswali waliyoulizwa kisanii . Pia waziri mkuu anataka auze sura peke yake kwenye maswali ya papo kwa hapo.

Waziri mkuu kama anataka kuendelea kuheshimika basi afute ule muda wake wa kuuza sura kwenye maswali ya papo kwa hapo siku ya Alihamis usionyeshwe live kwani ni muda wa kazi tena asubuhi wakati watu bado hawajachoka. Na pia zile pesa za kumuonyesha akiuza sura zipelekwe kununua madawa hospitalini.
 
Big point, Nimeishi marekani miaka zaidi ya mitano sijawahi ona bunge live kama ilivyokua hapa bongo, vyama vingine vimeo kweli kweli nao wameona pakutokea, stupid mind.
acha kamba wewe. Marekani gani umekaa hakuna live coverage of congress? Heard of C-Span?

Kwanini tuige nchi nyingine badala ya sisi kuwa mfano duniani na nchi nyingine kutuiga Tanzania?
Brilliant. Kwa nini sisi tusiwe mfano? Umeongezea yaliyosemwa na upinzani February 1st kuhusu kuiga iga mifano potofu. Kuna lightweight mmoja wa C.C.M. alisema mbona Sri Lanka hakuna live coverage!? Sugu, Waziri Kivuli wa habari, akawaambia kwa nini tufananishwe na Sri Lanka? Kwa nini isiwe, kwa mfano, Marekani ambako kuna C-SPAN wanaofanya wall to wall coverage of congressional proceedings?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nawe Nifah: kuwa mkweli, mwenye kutaka kuangalia bunge "live" asifichwe ukweli ni nani katika jamii kama siyo watu wa aina yako ambao hadi mna uwezo wa kuingia kwenye jamvi hili! Kama ni wewe na wa aina yako, muda huo wa "live" bunge mtakuwa kazini. Hata Machinga hawezi kuacha kusaka wateja aangalie bunge.

TUSILALAMIKIE VITU/MAMBO KAMA WATOTO.
Nifah yupo sahihi, kama TV inazuia watu kufanya kazi, TV ya Taifa izimwe hadi saa 2 na kuzimwa tena saa 5 usiku

TV inapokuwa na matangazo usiku kucha nani alilalamika ameshindwa kulala?

Tena population yetu inaongezeka kwa kasi kuliko sehemu nyingi duniani. Hii inaeleza TV si kikwazo kwa watu kutimiza majukumu yao wawe wamachinga au wana familia

Hoja isiyojibiwa ni hii, Nape, Waziri mkuu na Rais walisema tatizo ni gharama.
Je tatizo hilo limekwishaje kiasi cha kutoongelewa tena? Hoja haikuwa muda wa kazi

Serikali haina wajibu wa kusimamia hadi masiha ya kila siku ya mtu.
Wengine asubuhi hatukupata breakfast na wala hatujalalamika kwanini serikali haikutupatia.

Tunajua wajibu wa breakfast ni wa familia. Kama tutaangalia TV mchana kutwa hiyo si kazi ya Nape kwasababu hasimamii maisha yetu binafsi

Kinachoendelea ni kutaka kuficha mambo ambayo tunajua CCM na serikali yake wanayafanya. Hawataki kabisa wananchi waone kinachofanyika au kuzungumzwa nyuma ya pazia kwa hofu moja, kwamba kuna asili ya 'uovu'

Ni uovu kwasababu bungeni ni mkutano wa wazi, nini kinafichwa hapo?

CCM wanamwangusha Magufuli, wakati anajitahidi kutumbua majipu wapo wanaokwenda kinyume wakitaka maovu yafunikwe.

Hawa ndio wasiotaka 'live' ili wananchi walishwe habari wanazotaka wao.

Kama suala ni gharama na muda wa kazi, funga TV ya Taifa kabisa kuliko kutuonyesha Isidingo, Kingwendu n.k.

Ni kichekesho kwa serikali ya #Hapakazi kuchaguliwa watu vipindi vya kuangalia.

Hawana takwimu zozote kwa miaka Zaidi ya 10 ya bunge live kuthibitisha kauli zao.
Nape kaja na Bilioni 4 , wakati bunge linarudisha pesa za ziada bilioni 6.
Mfuko wa wakfu ukasema yupo tayari. Bado wanatafuta sababu tu

Hakuna jingine, ni njama za CCM kuficha uovu, halafu tunaambiwa majipu!!
 
Binafsi nimejiuliza, je kama watanzania hawa walikuwa wanatumia muda wao wote huo kwenye tv kwa kipindi hadi cha miezi mitatu je gharama za kulipia vinga'muzi na umeme walikuwa wakitoa wapi? Maana hawafanyi kazi.
 
Huyo atakuwa anaishi marekani kimagumashi Nadhani atakuwa analala Stoo na hana Tv .

Funza wewe Na hao wabishi wanzako mnapinga tu Kama chama chenu.ukweli Ni kwamba TV stations nyingi hazionyeshi Bunge live isipokuwa C-Span ambayo Ni moja ya chanel za kulipia.chanel za bure hazi onyeshi bunge live Kwa hiyo Google hajakosea
 
Majaliwa ameshachuja.
Ameishiwa pumzi.

Ina maana huyo waziri mkubwa kabisa hajui kwamba kwa sasa bunge linaonyeshwa muda wa kazi.??
Tena asubuhi mpaka sa tano muda mzuri wa wakulima kuwa shambani. Cha ajabu ni kwamba bunge halirushwi muda ule wa saa kumi wakati watu wanakua wameshatoka kazini.
Viongozi wa serikali ni vipofu wasioona kuwa muda wa kazi ni asubuhi mpaka saa tisa na nusu tena bunge la CCM linaonyeshwa nusu ya muda wote wa kazi.
Halafu wanawazuia waandishi wa habari wasifanye kazi. Uchumi wa hii nchi utaporomoka ndani ya miaka michache ijayo kwa kuwa serikali inataka kudhibiti kila kitu kinyume na kanuni la soko huria.
Vyombo huru vinavyolipa kodi vinaangalia soko na maoni ya wateja wao. Kwa nchi yetu bunge lilikua linaheshimika kutokana na watu kulifuatilia kwa kuonyeshwa live.
Hata mpira wa ligi ya Uingereza inapata umaarufu na kupendwa kutokana na kuonyeshwa live.

Wapinzani wako wapi wanze sasa kuzunguka kwenye majimbo yao waliyoshinda na nchi nzima ili waweke bayana hoja zao zinazopotoshwa na wahariri wa bunge la CCM na pia waje kueleza njama hizi za CCM za kuzima jicho la habari linalomulika uovu wa mawaziri na udhaifu wa wabunge wa CCM. Njama zinazofanywa ili tu kuwaaminisha watu kuwa serikali ya awamu ya tano ni ya watu watakatifu kwa wao kuuza sura lakini wabunge wafiche sura zao.
Huku CCM hao hao leo wakijifanya kuwa hawaoni mambo mazuri aliyoyafanya JK awamu ya nne. JK pamoja na udhaifu na wizi uliokuwa unafanywa na mawaziri lakini aliruhusu waandishi wa habari kumulika popote.

Nafasi ya kuuza sura imebaki kwa serikali kwenye matamasha úyao yanayoonyeshwa muda wa kazi. Kuuza sura kumebaki pia kwa mawaziri wakati wa kujibu maswali waliyoulizwa kisanii . Pia waziri mkuu anataka auze sura peke yake kwenye maswali ya papo kwa hapo.

Waziri mkuu kama anataka kuendelea kuheshimika basi afute ule muda wake wa kuuza sura kwenye maswali ya papo kwa hapo siku ya Alihamis usionyeshwe live kwani ni muda wa kazi tena asubuhi wakati watu bado hawajachoka. Na pia zile pesa za kumuonyesha akiuza sura zipelekwe kununua madawa hospitalini.

Sawa DJ Mbowe nimekusikia Na bunge live Hakuna.
 
Hapa ndio unajua uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu.Kwani lazima tufanane na nchi nyingine? nini maana ya kua nchi huru?

Kwani ni lazima tufanane na nchi nyingine katika utendaji wetu kama serikali? Hiyo TBC inatumia kodi zetu na tunayo haki ya kupangia inavyotu mika kwa manufaa yetu.
 
Nilishawahi kusema PM wa sasa hivi simuelewi elewi! Sidhani kama ni mtu makini hata kwenye medani ya siasa! Nadhani ukanda ndio umempa nafasi sio uwezo! Hoja zake hazina mashiko na anashindwa kujenga hoja! Time will tell more! Let's wait....
 
SIyo tu vikao vya Bunge na Senate vinaonyeshwa live. Marekani hawana tume za uchunguzi. Kama likitokea tatizo lolote,linaelekezwa kwenye Kamati ya Bunge husika. Kama ikitokea kashfa polisi,au jeshini,au popote,Kamati za Bunge zinacover kila kitu,kwa hiyo haiundwi tume ya uchunguzi. Tatizo linaelekezwakwenye hiyokamati,na matukio yanatangazwa live on C-Span.
 
Mmeona hilo tu ndo la kuiga ila kufanya maisha ya wananchi wenu yawe kama ya huko ulaya mnaona gumu
Tutayafanyaje maisha ya mtanzania yawe kama ulaya wakati nyie chadema mnatetea mafisadi na waiba mali za umma! Pesa itakaa kweli?
 
Back
Top Bottom