Kassim Majaliwa: Navishukuru vyama rafiki CHADEMA, CUF na ACT Wazalendo kwa kunipigia kura ya " Ndiyo" niwe Waziri mkuu!

Maendeleo hayana chama lakini akumbuke alichomfanyia mgombea wa Chadema ili yeye apite bila kupingwa.
 
Kupiga kura ya “hapana” kwa mtu ambaye ni lazima apitishwe iwe jua au mvua ni kupoteza muda tu na kujitafutia uadui na chuki bila sababu za msingi

Walichofanya hao wabunge ni sawa tu.
 
Eti vyama rafiki wakati kwenye kugombea ubunge walikupitisha bila kupingwa!!

Huku ni kujikosha tu kutokana na dhuluma mlizofanyia wapinzani.
PM wa ovyo kabisa huyu..Ruangwa pale wameteka na kutesa mgombea wa chadema ili huyu mshenzi apite bila ya kupingwa..mambo ya ovyo kabisa kufanywa na waziri mkuu.
 
Ni Yeye Majaliwa Kassim Majaliwa waziri mkuu wa Tanzania
Sio Yule wa masaa 72😂😂
 
Eti vyama rafiki wakati kwenye kugombea ubunge walikupitisha bila kupingwa!!

Huku ni kujikosha tu kutokana na dhuluma mlizofanyia wapinzani.
Alitaka kumuua mbunge wa ACT wazalendo baada ya kuchukua fomu.

Hawa jamaa ni wanyama wakali
Poleni sana na tabia yenu ya kudanganya WanaJF kuwa mnachuki kumbe mioyoni mwenu mnapenda na kusifia kazi iliyofanywa na Serikali ya CCM, kwa miaka 5 iliyopita chini ya huyo mnayejidai kumshutumu.

Mnajua fika miaka 5 ijayo Serikali ya CCM, ikisimamiwa na huyo Waziri Mkuu, uchumi wa mtu mmoja mmoja , ikiwa ni pamoja na ninyi, na wa Taifa kwa ujumla utapaa. Na hakuna shska kuwa maendeleo makubwa ya vitu na watu yatapatikana kwa sababu wajenzi wa nyumba ni wamoja ambao hawatakuwa wanagombania fito kama ilivyokuwa na uwepo wa wapinzani.

Kama kweli ninyi Saint Ivuga Salary Slip na kundi lenu humu JF), ni wapinzani wa kweli, ushauri ni kurudi kwenye meza mjipange upya kwa kuwa 2025 vyama vya upinzani vitafutika kabisa kwa kuwa wapiga kura wote wataamini utawala wa chama kimoja kutokana na maendeleo makubwa yatakayokuwa yamepatikana.
 
Eti vyama rafiki wakati kwenye kugombea ubunge walikupitisha bila kupingwa!!

Huku ni kujikosha tu kutokana na dhuluma mlizofanyia wapinzani.

Waziri yupo sahihi kwa kushukuru vyama rafiki (CUF CHADEMA TLP NCCR CHAUMMA UDP) kwa kumpitisha bila kupingwa ubunge kule jimboni. Vyama vyote viliamua kupitisha yaani bila kuwa mbunge mpinzani!
 
Maendeleo hayana vyama (wapinzani walichelewesha maendeleo).

Lakini CCM ndiyo yenye kuleta maendeleo (nileteeni flani ili niwaletee maendeleo, mkichagua upinzani sahauni maendeleo).

Kalaghabao.
Halafu anamalizia kwa kusema " nasema uongo ndugu zangu?"
 
Waziri mkuu mh Kassim Majaliwa amewashukuru wabunge wa vyama rafiki Chadema, Cuf na ACT wazalendo kwa kumpigia kura za "ndio" kwenye ushindi wake wa 100% wa kumthibitisha kushika wadhifa huo.

Mh Majaliwa amesema maendeleo hayana chama hivyo atashirikiana na wabunge wote bila kujali itikadi katika kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi.

Maendeleo hayana vyama!
Hivi wabunge wa vyama rafiki ni kina nani? Nani ana orodha kamili?

Amandla...
 
Waziri mkuu mh Kassim Majaliwa amewashukuru wabunge wa vyama rafiki Chadema, Cuf na ACT wazalendo kwa kumpigia kura za "ndio" kwenye ushindi wake wa 100% wa kumthibitisha kushika wadhifa huo.

Mh Majaliwa amesema maendeleo hayana chama hivyo atashirikiana na wabunge wote bila kujali itikadi katika kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi.

Maendeleo hayana vyama!
Safi sana, haibu kwa Zitto na Lissu
 
Hahah mnamkataa Mbunge wenu tena? Yule ni Mbunge wa CHADEMA na yupo pale kaa ridhaa ya wananchi! Wabunge wengine akiongozwa na Mwenyekiti wenu Mbowe wameshindwa kutetea majimbo yao. Msimkatae mwenzenu kisa yuko peke yake. Ndo demokrasia hiyo vumilieni tu.

Tangu lini haramu ikazaa halali?

Wajifanya hujui matokeo haramu ya uchaguzi huu yalipatikana je?

Jiwe na hata huyu mwenye shukurani uchwara wanajua. Jitendee haki hata kwa kuwasiliana nao kufahamu kwa non ilibidi kupata huduma ya wakora. Kwani vinginevyo mbombo ilikuwa nkafu!
 
FB_IMG_1605339581808.jpg
 
Back
Top Bottom