Kassim Majaliwa: Makontena ya Makinikia yanayosafirishwa nje ya nchi ni halali

Maswali muhimu ambayo majibu yake yataweka mambo sawa vichwani mwa wenye akili;

1. Usafirishaji wa makinikia uliruhusiwa lini tena baada ya kuzuiwa kwa madai ya udanganyifu?
2. Nini tofauti ya bei ya sasa na ile ya zamani?
Nimedokezwa ukweli huu mchungu hadi nikatamani kuzimia:

1. Makontena yameanza kusafirishwa nje ya nchi tangu mwendazake yuko hai.

2. Hakuna kilichobadilika kutoka mfumo uliokuwa unatumiwa na Serikali ya JK kupitia TMAA kusafirisha makinikia hayo nje. Utaratibu huo ulikuwa ni: sampuli kuchukuliwa na kupimwa, thamani ya awali ya madini husika kukokotolewa, mrabaha wa awali kulipwa, makontena kusafirishwa na kusafishwa nje ya nchi kwa vibali maalum, baada ya makinikia hayo kuchakatwa huko nje na thamani yake halisi kujulikana, kama thamani ya awali itakuwa ndogo wawekezaji wanalipa serikalini mrabaha wa mwisho na kama itakuwa chini wanarejeshewa na serikali hela iliyozidi kwenye malipo ya awali. Narudia tena, hakuna kilichobadilika.

3. Madini yanayolipiwa kodi na mrabaha bado ni yaleyale, hakuna kilichoongezeka - ni dhahabu, shaba na fedha.

Nampongeza sana mama yetu SSH kwa kupambana kufufua uchumi wetu na kukataa propaganda za kisiasa ambazo zilichangia sana kuvuruga uchumi wa nchi yetu hususan sekta ya madini. Ingekuwa dunia ya kwanza, wahusika wangeomba msamaha kwa uongo walioupiga kwa umma kuhusu wizi kwenye makinikia wakati mambo yalikuwa under control. KAZI IENDELEE.

Wanaopinga taarifa hii waje na maelezo yafuatayo:
1. Je, yale makontena yaliyozuiliwa kipindi cha mwendazake si tayari yalishapelekwa nje, tuelezwe aina ya madini yaliyopatikana baada ya kusafishwa huko nje na kama kuna utofauti na kile TMAA walichokuwa wamekikadiria kupitia sampuli zilizopimwa.
2. Je, Utaratibu wa sasa wa kusafirisha makontena hayo unaotumika hivi sasa una tofauti gani na ule wa kipindi cha nyuma.
3. Je, tumevuna kiasi gani cha fedha hivi sasa kupitia makinikia na je inatofauti gani na mapato ya awali.
4. Je, sheria yetu ya kuzuia makinikia kusafirishwa nje tumeifuta au bado ipo. Kama ipo yanasafirishwa nje kwa sheria ipi?
PROPAGANDA SAWA LAKINI TUMUOGOPE MUNGU JAMANI.
 
Tumesema sana hapa jukwaani wakati wa dhalimu kuwa makinikia yaliyokamatwa yalishaondoka, na yanaendelea kwenda nje. Na ushahidi wa tulivyosema umo humu humu jukwaani. Unabakiza maneno ili kulinda heshima ya PM, kuna jizi lolote la kura lenye heshima?
Hahaha unajiona mtakatifuuu.
 
Utaratibu wa kusafirisha makinikia haujawa kubadilika tangu ensi za Mkapa. Mwendazake alikuja na mbwembwe nyingi za kutafuta simple popularity kutoka kwa wajinga.

Mineral concentrates zinafirishwa toka Duniani kote, yeye akaja kuwadanganya Watanzania wajinga kuwa tunaibiwa, na kuwa makonteina yale 90% ni dhahabu tupu. Wajinga wakamshangilia kutokana ja ujinga bila ya kujiuliza, utabebaji container 20ft container load lenye 90% gold, ni lorry gani litakuwa na uwezo (gold has SG 19.30) - wakabaki wanakenua meno kuwa eti wamepata mkombozi ilihali ile report nzima ya Mruma na Uroso zilikuwa good for the fools.
Ndio ile “professorial …”?
 
Anatuona sisi mambulula, kwanini hiyo michanga isifanyiwe kazi hapa hapa ili kuleta ajira nyingi. Asifikiri woote nywele zetu zipo upande km yeye.
 
Wamesema wameyapima na kuchukua kodi
Hata mwanzo ndio ilikuwa hivyo, sisi tumeuza mchanga, wamepima mchanga, na kutulipa kodi ya mchanga!. Tulipoyazuia, tuliyazuia kwa kuhisi tunaibiwa kwa vile hutujui kilichomo. Tukapima kilichomo, tukathibitisha tulikuwa tunaibiwa na tukapiga hesabu ikaja US $ 190.B . Tukaamua lazima tuyachenjue ili tujue kinachopatikana. Sasa kama tumeamua kuruhusu bila kujua kilichomo, why did we stop them mwanzo na kuja kuruhusu sasa?. What is the diference betwen export before ban, and now?.
P
 
Hata mwanzo ndio ilikuwa hivyo, sisi tumeuza mchanga, wamepima mchanga, na kutulipa kodi ya mchanga!. Tulipoyazuia, tuliyazuia kwa kuhisi tunaibiwa kwa vile hutujui kilichomo. Tukapima kilichomo, tukathibitisha tulikuwa tunaibiwa na tukapiga hesabu ikaja US $ 190.B . Tukaamua lazima tuyachenjue ili tujue kinachopatikana. Sasa kama tumeamua kuruhusu bila kujua kilichomo, why did we stop them mwanzo na kuja kuruhusu sasa?. What is the diference betwen export before ban, and now?.
P
Hayajaruhusiwa leo yameanza kabla ya 17/03/2021
 
Serikali iwe makini na hili suala
Wao wenyewe wanaona haijawahi tokea Waziri Mkuu kujibu swali bungeni halafu na Ofisi yake itoe barua ya taarifa kwa Umma kwa kile alichosema bungeni.!
Ngoma nzito sana hii Hayati kaiacha..!
 
PM anaingizwa chaka baya bila kujua. Ameulizwa general question, na alipaswa kama mtendaji mkuu wa serikali, kupress for more specific details, na wala siyo kuhangaika haraka kuwasilisha maelezo mengi kwa lengo tu la kuwapooza Watanzania.

Hoja ya msingi: ^Kontena zileeeeeee zinaenda tena^

PM angeomba ushahidi specific na kuahidi kufuatilia. Suala la madini ni nyeti sana na limetugharimu mengi huko nyuma na hata wakati wa kurekebisha sheria za madini. Pia linamendewa usiku kucha na wapigaji wa ndani na nje ya nchi. So, halipaswi kujibiwa na kupita kijuujuu tu hivi.

PM zile nguvu zako za weledi na uzalendo halisi ziko wapi!??? Ama ziliishia ileeee tarehe 17 Machi 2021!??? Nawe umekuwa kama Bi Mkubwa na Dkt Plan wake ambao wamewekeza vipaumbele vyao kwenye empty hotuba tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!???
ndiyo maana alitoa maelezo marefu ili watu kama wewe wagumukuelewa muelewe kwahiyo ulitaka aunde tume kuchunguza kitu ambacho anataarifa nacho anakijuwa kinavyofanyika?
 


Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewatoa hofu Watanzania kuhusiana na kuwepo kwa makontena yenye makinikia ambayo yameonekana yakisafirishwa kwenda nje ya nchi kuwa makontena hayo yanasafirishwa kihalali.

Waziri Mkuu amesema hayo bungeni Mkoani Dodoma wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu kitendo ambacho hufanyika kila siku ya alhamisi iwapo waziri mkuu anakuwepo bungeni.

Amesema makontena hayo yanasafirishwa chini ya utaratibu maalum ambao umewekwa na Serikali kupitia kampuni ya umma ya madini ya Twiga kwa kushirikiana na wachimbaji wakubwa wa madini.

Waziri Mkuu amesema kinachofanywa sasa na serikali kwa kilichopo ndani ya makontena hayo kukaguliwa na kupimwa kisha serikali kulipwa inachotakiwa kupata na baada ya hapo wahusika wa makontena hayo yenye makinikia kupewa nyaraka za kuwadhibitisha ambazo hutakiwa kuzionyesha mara zinapohitajika.

Mwaka 2017 hadi mwaka 2018 Serikali tume maalum ya kuchunguza jinsi ambavyo Tanzania inavyonufaika au la na Sekta ya madini ambapo ilibainika uwa sekta hiyo imegubikwa na udanganyifu.
View attachment 1807221

View attachment 1806771

This is a stupid argument. Kwani zamani hayakulipiwa? Hoja ilikuwa ni uhakiki wa kilichomo ndani ya makinikia. KWa nini madini yasiondolewe hapa hapa na thamani ijulikane? tusiambiwe yamelipiwa. Kwa vigezo gani?
 
Hata mwanzo ndio ilikuwa hivyo, sisi tumeuza mchanga, wamepima mchanga, na kutulipa kodi ya mchanga!. Tulipoyazuia, tuliyazuia kwa kuhisi tunaibiwa kwa vile hutujui kilichomo. Tukapima kilichomo, tukathibitisha tulikuwa tunaibiwa na tukapiga hesabu ikaja US $ 190.B . Tukaamua lazima tuyachenjue ili tujue kinachopatikana. Sasa kama tumeamua kuruhusu bila kujua kilichomo, why did we stop them mwanzo na kuja kuruhusu sasa?. What is the diference betwen export before ban, and now?.
P
Ndugu, Yale yalikuwa maigizo ya 'mzarendo' Jiwe & co.
Hakuna mtz yoyote nje ya kikundi chao aliyeruhusiwa kuongea wala kutoa wowote kuhusu chochote au lolote, chini ya usimamizi/ulinzi wa nguvu kubwa ya wasiojulikana.

Kwa kweli sijui HASA wewe ulitegemea nini wakati mchakato mzima tangu upimaji wa makinikia, mazungumzo yao na mikataba HALISI iliyojiri, pamoja na majisifu mengi kwao ulikuwa na umeishia kuwa siri YAO kubwa.

Kama ulikuwa wasoma 'body language' ungewaona hata MABEBERU hawakuonekana kujali wala kutishika na matamshi/madai vichekesho ya Mhe Kabundi. Yalikuwa ni ya kuwachota tu watz.

Sasa hivi PM anatia huruma sana kwa tabu kubwa anayopata aweze kufunika uvundo ambao hakuhusika, vilevile kama ilivyokuwa kwenye korosho. Kosa lake kubwa ambalo litaendelea KUMLA, ni kukosa ujasiri wa kujiuzulu wakati uleule.

Ndugu yangu, MUDA ndio utakaokuja kusema UKWELI vizuri zaidi na kwa sauti zaidi. AMEN
 
Acha kupotosha watu wewe Mbweha uliekengeuka na kukosa busara. Twiga minerals ilipoundwa ndio habari ya kusafirisha makinikia ikaanza kupata baraka.
Usipanic dogo, tuliuliza yalipo macontainer ya makinikia kabla ya hiyo sijui Twiga hakukuwa na majibu. Jitahidi kuvumilia ukweli.
 
Naomba niweke wazi kuwa mimi taaluma hii ya madini naifahamu maana nimesoma mambo haya ya mawe. Unaposema kuwa pesa imelipwa basi useme pia ni kiasi gani?

Tunataka muweke wazi taarifa za kijiolojia na kichemia juu ya kiasi cha madini yaliyomo kwa kila tani moja ya mchanga. Na kwanini hamkuutangazia umma juu ya makubaliano ya kuendelea kusafirisha nje mchanga huo wenye madini?
 
Back
Top Bottom