Kassim Majaliwa: Madaktari na manesi wanalipwa mshahara mkubwa kwa sababu wamesoma muda mrefu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kassim Majaliwa: Madaktari na manesi wanalipwa mshahara mkubwa kwa sababu wamesoma muda mrefu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thereitis, Jun 29, 2012.

 1. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Naibu waziri Tamisemi anayeshughulikia elimu aliyasema hayo leo asubuhi kupitia kipindi cha jambo Tanzania kinachorushwa na TBC1. Amesema walimu na watumishi wa kada nyingine ambao wamesoma chuo kwa muda mfupi ukilinganisha na madaktari wanastahili mshahara huo.

  Kwa mtazamo wangu naibu waziri Majaliwa hayupo sahihi. Nafikiri si sawa kumlipa mtumishi mshahara mkubwa au mdogo eti kwa kuangalia kigezo cha muda aliotumia alipokuwa chuoni. Watumishi wote wa serikali wanafanya kazi ya kuwatumikia watanzania kwa kutumia taaluma zao; wote wanamahitaji ya kibinadamu yanayolingana; wote wanaishi katika nchi moja yenye mfumuko mkubwa wa bei ya bidhaa.

  Naomba michango yenu wakuu.
   
 2. m

  moseskwaslema Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Achana na wanasiasa wachovu kama hao,yeye amesomea unaibu waziri miaka mingapi?,nani ana taaluma ya ubunge au unaibu waziri? kwanini wanalipwa viwango vikubwa vya mishahara wile hakuna taaluma ya namna hiyo. Hawa viongozi wanashindwa kuelewa alama za nyakati,watanzania tunahasiri na wao bado wanaendelea kuropoka tu.

  Ngoja na walimu tuanze kugoma ili waropoke zaidi.
  Naomba nichukue fursa hii kuwashawishi walimu na wakufunzi wa vyuo kuwa mgomo wetu uwe pale endapo serikali haitatulipa madeni yetu pamoja na nyongeza ya mishahara katika bajeti ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi.
   
Loading...