SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,805
- 1,874
Tabia aliyoiacha ya kuwafanya watanzania wawe waoga kumuondoa mkubwa yeyote tangu Waziri Mkuu ilimgharimu hata mwenyewe.
Kwanza ilikuwa ni vigumu kukibadili chama chake akalazimisha yeye binafsi mjadala wa vyama vingi uingie mtaani.
Pili katika vikao vya chama alikasirika jinsi walivyobabaisha katika hoja ya kuukubali utanganyika. Hapa aliona Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa chama wanapaswa kujiuzuru nafasi zao.
Hakutokea hata mmoja serkialini kuwaambia, yeye akaamua kuwaambia na ukumbuke wakati huo yeye hana madaraka yoyote.
Hata wakati amewaambia Malecela na Kolimba kujiuzuru, bado kichinichini walikataa na kuliza "Kwani Nyerere ndiye nani".
Hawakujiuru.
Hatimaye akaandika kitabu akakisambaza mitaani ndipi Malecela akaondolewa kwenye Uwaziri Mkuu.
Hapa tunajifunza nini?
Ukwlei ni kwamba Mwalimu Nyerere hakuacha msingi mzito wa Waziri Mkuu kuwajibishwa inapotakiwa kufanya hivyo.
Alichofanya Nyerere ni kuandika kitabu kama raia wa kawaida, jambo ambalo hata wewe unaweza.
Lakini tofauti yako na Nyerere ni kwamba hakuna ambaye alithubutu kumuweka mahabusu kwa kuandika kitabu kile. Kingekuw akimeandikwa na mimi au wewe inawezekana ungefia mahabusu ingawa kesi ungeshinda mahakamani.
Hivyo, katika maksa makubwa ya Mwalimu Nyerere ni pamoja na kutoacha utaratibu wa kumwajibisha mkubwa kuanzia Waziri Mkuu na utaratibu huo ukawaacha salama walioanzisha hilo jambo.
Utaratibu wa kutunga kitabu hauna usalama wowote kwa mtu ambaye hajawahi kukalia kiti cha urais kama Julius Nyerere.
Hivyo naona kuwa hili ombwe ni kubwa aliloacha Mwl. Nyerere.
Jadili kwa hoja inayojenga, tunaleta hoja za kujenga nchi yetu. Penye kosa tuseme kosa ili tuone jinsi ya kulirekebisha na si kuleta kejeli