Kasi ya Zanzibar kujiletea maendeleo yaongezeka, sasa inajenga bandari kubwa ya kisasa. Hongera Rais Mwinyi na Maalim Seif!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,796
141,694
Zanzibar imetiliana saini na serikali ya Oman katika ujenzi wa bandari kubwa na ya kisasa zaidi Afrika ya mashariki.

Bandari hiyo mpya itakuwa na gati nyingi zikiwemo za container, mafuta, gesi, uvuvi, utalii wa bahari nk.

Utiaji sainu mkataba wa ujenzi bandari hiyo ya kipekee Afrika ya Mashariki umeshuhudiwa na viongozi wote wakuu wa serikali wakiongonzwa na Rais Mwinyi na makamu wake Maalim Seif.

Nimuombe Mbowe wa Tanganyika akajifunze kwa Maalim Seif.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hahahaa! Hapo angetangazwa mshindi yule anaeshinda kwa kura za wananchi halafu akafanya hili la kutiliana saini na watu wa Oman mngesema anaanza leta ndugu zake!
 
Kwanini watiliane saini na wakoloni, ina maana hawana fedha za ndani kutekeleza mradi huo, wanakwama wapi aisee...?
 
... kwa saizi ya Zanzibar na geographical location yake inahitaji kuwa na bandari kubwa kihivyo? Kama mfanyabiashara wa bara au nchi jirani kwanini nipitishe mzigo Zanzibar badala ya bandari ambayo baada ya hapo unaingia nchi kavu moja kwa moja? Sipati logic.
 
Utapata logic bandari ikikamilika!
 
... kwa saizi ya Zanzibar na geographical location yake inahitaji kuwa na bandari kubwa kihivyo? Kama mfanyabiashara wa bara au nchi jirani kwanini nipitishe mzigo Zanzibar badala ya bandari ambayo baada ya hapo unaingia nchi kavu moja kwa moja? Sipati logic.
Mkuu una taaluma ya usafirishaji au? Hii itakuwa strategic port kwa ajili ya transhipments ( kama ilivyo Dubai port, au Singapore), pia yaweza kuwa "free port" Hivyo kupunguza safari za kwenda china kufuata bidhaa kwa watu wanaotoka landlocked countries badala yake wanaenda hapo Zanzibar! Hili wazo lilikuwepo hapa bara ndilo liliolopelekea bomoabomoa ya Kurasini!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom