Kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jul 11, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha
  Imeandikwa na Anna Makange, Muheza; Tarehe: 11th July 2011

  TANZANIA itakumbwa na ongezeko la watu maradufu katika kipindi cha miaka 25 ijayo, kutokana na kufikia kiwango cha asilimia 2.9 cha ukuaji wa idadi ya watu ambacho ni cha juu ikilinganishwa na kiwango cha asilimia 1.8 katika nchi zinazoendelea.

  Ongezeko hilo linatokana na kiwango kikubwa cha uzazi ambapo kwa wastani mwanamke wa Kitanzania huzaa watoto sita ikilinganishwa na wastani wa watoto watatu kwa kila mwanamke duniani, kiashiria hicho kinachochewa na idadi ndogo ya Watanzania wanaotumia huduma za kisasa za uzazi wa mpango.

  Hayo yamebainishwa jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza katika Mkoa wa Tanga.

  Ni asilimia 27 tu ya kinamama wa Kitanzania ndio wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango ikilinganishwa na nchi nyingine zinazoendelea kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Kenya ambayo imepiga hatua kubwa kwa kufikia asilimia 46 kwa takwimu za 2009.

  Akizungumza katika sherehe hizo, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Florence Mwanri alisema, ni ukweli ulio wazi kuwa rasilimali watu ndiyo nguzo muhimu katika maendeleo, lakini ni dhahiri kwamba idadi kubwa isiyoendana na ukuaji wa uchumi ni changamoto katika harakati za kufikia maendeleo.

  "Makisio ya idadi ya watu inaonesha Tanzania ilikuwa na watu milioni 43 mwaka 2010 na inatarajiwa kufikia milioni 63.5 mwaka 2025 kutokana na kiwango cha sasa cha ukuaji wa idadi ya watu cha asilimia 2.9 kwa mwaka kuwa juu hasa ikilinganishwa na cha asilimia 1.8 kwenye nchi zinazoendelea na kwa kuzingatia kwamba asilimia 50 ya watu hao ni vijana ikilinganishwa asilimia 30 ya vijana kwenye nchi zinazoendelea.

  "Hii inaonesha kuwa juhudi za makusudi zinahitajika ili kutumia rasilimaji ya vijana katika kukuza uzalishaji wenye tija na kuongeza pato," alisema Mwanri ambaye ofisi yake ndiyo inayoandaa sherehe hizo.

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Kalembo aliwataka wananchi kushiriki kwa vitendo kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau wengine wa maendeleo kutekeleza mikakati itakayosaidia kukabili changamoto zinazotokana na kasi ya ongezeko la idadi ya watu kwa kuchukua hatua ya kuanza kupanga uzazi na kupunguza idadi ya watoto.

  "Kasi hii ya ongezeko la idadi ya watu mara mbili ni changamoto kubwa sio tu kwa Serikali ambayo inatakiwa kuwekeza zaidi kwenye huduma za elimu na afya ili kuharakisha maendeleo, bali pia kwa familia ambayo inayo wajibu wa kutumia nguvu na ujuzi wao katika kuongeza uzalishaji ili kukuza kipato kitakachowezesha kuondokana na umasikini.

   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu kuna haja kubwa ya Viongozi wa dini zetu kubwa mbili kushirikishwa katika kampeni za uzazi wa majira.

  Vinginevyo jitihada/kampeni za kupunguza kasi ya kuzaliana hazitakuwa na mafanikio yoyote. Bado kuna Watanzania wengi wanaoamini kwamba, "Kila mtoto huja na riziki yake." kitu ambacho hakina ukweli wowote.

  Imefikia wakati wa Watanzania kuwa na familia kutokana na uwezo wao wa kuwapa watoto wao malezi bora ikiwemo elimu toka wanapozaliwa hadi watakapoweza kujitegemea, vinginevyo ndio nchi yetu itazidi kuwa nchi ya walalahoi na hivyo kubaki nyuma sana kimaendeleo ukilinganisha na nchi nyingine duniani.
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu huwezi kula sweet ikiwa na karatasi. lol

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Hahahahahah lol! unaweza kula bila karatasi na matokeo yake yasionekane baada ya miezi 9...Ni uamuzi tu Mkuu...Mwalimu alisema kupanga ni kuchagua :)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 841
  Trophy Points: 280
  Ni tatizo lililopo hasa vijijini maana mtoto anarithi kilimo, ufugaji au uvuvi na sio elimu
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu unashauri kuwa Tupange Uzazi au Tuzuie Uzazi, kipi unapendekeza ili tujadili. Maana yote yanajadilika.

  Maana ukisema uzazi wa majira ina maana kila msimu watu wazae au? Yaani Kiangazi mtoto, Masika mtoto, Vuli Mtoto, majira ya kuchipua Mtoto au...?
   
 7. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Tanzania bado ina eneo kubwa, ardhi nzuri na mali asili nyingi tu. Watuu waendelee kuzaliana ni poa tu. In terms of eneo Tanzania iko sawa na Nigeria. Nigeria wako zaidi ya 110 Milioni na sisi bado 40mil. Watu wengi soko kubwa kama China na India. Tukizaliana hadi tufike 100+ million akili zitafunguka, zilizoganda zitayeyuka.
   
 8. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,313
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  jumlisha na mikoa ya Arusha na Iringa ambayo huwa na vipindi vya kutafuta wake ambapo idadi kubwa lazima iongezeke kwenye miezi ya feb, march hadi june.
   
 9. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Sasa tufanyeje? haya mauzazi ya mpango yametuletea majanga mengi sana wanawake, kansa za kizazi zimeongezeka sana walisema na hili, wasitudanganye na haya mauzazi yao ya mpango ya misaada, yanazidi kutuangamiza, acha tu tuzae au bora tutumie njia za asili tu...mauvimbe yamekuwa mengi, kila wanawake wanne ukikaa nao wawili au mmoja ana uvimbe kwenye kizazi
   
 10. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Point ni kwamba wazazi wazae iwapo tu wanauwezo wa kuwatunza na kuwasomesha watoto wao.., sio wewe uzae uachie jamii ikulelee mtoto
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Mkuu inabidi kuangalia mfuko wako unaruhusu kuwa na watoto wangapi ambao utaweza kuwapa malezi mazuri ikiwemo elimu ya uhakika tangu wanapozaliwa mpaka wanapoweza kujitegemea badala ya kuwa na watoto 10 wakati uwezo wa wazazi hao labda ni watoto wawili tu. Bado kuna Watanzania wengi wanaamini misemo iliyopitwa na wakati kama vile, "Kila mtoto huja na rizki yake" au "Tajiri na mali yake na maskini na wanawe" misemo hii haina maana yoyote ile kwani mtoto anapozaliwa haingii duniani na kitita chake cha pesa kwa ajili ya malezi yake mpaka pale atakapoweza kujitegemea.

  Hayo ya masika mtoto, Vuli mtoto sijui na kiangazi mtoto ndiyo yanasababisha familia za walalahoi maana Wazazi wengi hawawezi kumudu gharama kubwa za maisha ya kila siku na hatimaye watoto hawali vizuri na wala hawapati elimu nzuri na ukichanganya na ujira mdogo wanaoupata Watanzania wengi hali ndio inazidi kuwa mbaya katika kuendelea kuwa Taifa la walala hoi
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Tujipe hongera
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dada yangu hii allegation imefanyiwa utafiti?? na how come kama hali iko hivyo halafu tena uzao unaongezeka kwa kasi? Au ndiyo yale yale kwamba ukivaa nguo nyekundu wakati wa mvua unakaribishwa kucharazwa na radi!
   
 14. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #14
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Tuzae na tujaze Tanzania
  ..

  Wekeni kwanza idadi ya wanao fariki kwa
  Mwaka..... tulinganishe...

  Kama ziko similar tuacheni tuzae tu....
   
 15. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Tunawapa sana shida watoto tunaowazaa bila mpangilio, mtu unakuta anazaa watoto halafu anawabebesha machungwa au ndizi kwenda kuuza huku jua kali likimpiga kichwani. Nina dada yangu binamu utamsikia nazaa bwana nisipozaa huyu bwana hela anaenda kuhonga, halafu hata kibanda cha kuweka mbavu hana na yeyeye mwenyewe hana kazi, huwa sipati picha mumewe akifa sijui itakuaje.

  Halafu watu kama hawa bubu hawaelewi hata uongelee nini. Mi nadhani pia na malezi yanachangia unakuta mtu wamezaliwa kumi na yeye anafuata hivyo hivyo. So wazazi wa sasa tukizaa kwa mpango naamini hata watoto wetu watafuata nyayo zetu huko mbele.
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mimi huwa nachanganyikiwa mtu anaposema watu wazae kwa mpango, huo uzazi wa mpango ndio upi, kwani mimi naamini kuwa kila mwenye kuamua kuzaa, iwe mtoto mmoja, wawili au hata watoto kumi ndio mpango wake huo, yaani alisha amua kuzaa idadi hiyo ya watoto, ndio kesha panga hivyo.

  Sasa mimi sioni tatizo, kinachotakiwa ni serikali kuondoa maradhi yanayo wakumba watoto wadogo, kama vile Kifaduro, Pepopunda, Ndui, Maleria na yale magonjwa yote yanayo waandama watoto. Wakisha fanikiwa ilo sasa ndio waingie kwenye kampeni za hizo zinazo itwa uzazi wa mpango.
   
 17. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia, mkatawale ndege, wanyama na samaki.
  Sasa tatizo liko wapi? As long as unao uwezo wa kulea ruksa!!
   
 18. DIUNATION

  DIUNATION JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2014
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,878
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Katika taarifa ya habari ya channel 10 usiku huu imeripotiwa kua watoto 101 wamezaliwa katika mkesha wa chrismas pekee katika hospiitali za Amana Temeke na Mwananyamala.Sasa kwa nchi nzima nzima wamezaliwa watoto wangapi na je kwa mwaka mzima?
   
 19. Lateni

  Lateni JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2014
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 685
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  soon tutakua kama Nigeria. Mnaigeria asipozaa watoto kuanzia saba na kuendelea anaona kama hajazaa.
   
 20. cooper

  cooper JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2014
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 394
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Mtajaa Kariakoo labda. Hii nchi nice kubwa mno. Safiri kwenda mwanza, tbr, Mbeya uone mapori yalivyo makubwa. Nyie ishoeni kugombea tuviwanja vya mjini.
   
Loading...