Kasi ya Wanafunzi shule ya msingi kukatishwa masomo kisa michango inaongezeka kila kukicha

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,787
4,424
Salaam Wakuu

Kumeibuka tabia za waalimu wa shule za msingi kuwarejesha watoto majumbani kisa hawajatoa michango mbalimbali ikiwamo ya mitihani, ulinzi na michango mingine.

Kutokana na hali hii watoto wamekuwa wakitoka shule wanazunguka mitaani bila kuwa na shughuli maalumu ya kufanya.

Nafikiri jambo hili sio sawa kwa sababu linawanyima watoto hawa haki ya msingi ya kupata elimu. Pia jambo hili ni baya kimaadili na kiusalama kwa sababu kuondoka shuleni muda usio sahihi unaweza kumshawishi apitie katika mazingira mabaya.

Nashauri walimu watafute mbinu nyingine ya kuwabana wanafunzi kutoa michango kuliko kuwaondoa shuleni au kuwakatisha masomo.

Sambamba na hili, Wazazi pia tuwe wawajibikaji kwa kulipa michango inayotakiwa ili tusifanye kazi ya waalimu kuwa ngumu. Elimu ni bure lakini michango midogo midogo tujitahidi ili mambo yaende.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom