Kasi ya wakuu wa mikoa ni stahiki?

phillipinne

New Member
Jun 27, 2016
4
7
Ndugu zangu ni miezi kadhaa imepita tangu kuteuliwa wakuu wa mikoa kuhudumu ktk serikali ya awamu ya tano. Hata hivyo tayari baadhi ya wakuu wa mikoa wameachishwa nyadhifa baada ya kufurushwa kwa sababu mb alimbali ikiwemo udanganyifu juu ya watumishi hewa. Swali la kuujiuliza Mimi na wewe, je ni kweli hawa wakuu wa mikoa kwa ujumla wao wemekidhi mahitaji ya wale wanao waongoza kwa katika utatuzi wa changamoto mbalimbali?

Nikilinganisha aina na mbinu za wakuu wa mikoa waliopita na wa sasa naona hakuna tofauti kubwa kwani ubunifu na uwajibikaji juu ya kutatua kero za wananchi uko chini sana,wengi wao wanakosa creativity na abilities ya kuexplore potentials ktk mikoa Yao na kuconvert into solutions kwa matatizo ya wananchi wao hasa ajira. Ndiyo maana hakuna mkuu wa mkoa mwenye plan pana ya kutatua tatizo la ajira ktk mkoa wake kwa kutumia mazingira asilia ndani ya mkoa wake.

Huduma za jamii bado zinakabiliwa na changamoto kubwa kwa namna zinavyopatikana na kutolewa huku wakuu wa mikoa hawa kutokuwa na mbinu madhubuti juu ya hili.

Migogoro ya aridhi bado ni changamoto kubwa kwani bado wananchi wananyang'anywa aridhi hata na viongozi wa serikali za mitaa na vijiji.
Mfano mkazi wa kijiji cha ring'wani kata ya ring'wani wilaya ya Serengeti mkoani mara jina lake Emmanuel Mataro ananyang'wa aridhi yake na mwekiti wa kijiji mwenye jina la Masese, mtu hajawahi kupata msaada.
 
Back
Top Bottom