Kasi ya uzazi mzigo mkubwa kwa uchumi wa Tanzania, Sheria itungwe

Lububi

JF-Expert Member
May 3, 2013
2,121
3,732
Familyplanning-640x350.jpg

LENGO la kupunguza nusu ya watu wanaoishi katika umaskini na njaa nchini Tanzania na kuwafanya wawe katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 linaweza kuhatarishwa na ongezeko la idadi ya watu, zaidi katika maeneo ya vijijini.

Hali hiyo, ambayo ni pigo kwa mikakati ya Taifa ya kupunguza umaskini kama inavyoainishwa kwenye Awamu ya Pili ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II) pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo kuelekea mwaka 2025, inatokana na kasi kubwa ya ongezeko la watu nchini ambayo haiendani na mipango mingine ya maendeleo.

Miongoni mwa mambo ambayo yamesisitizwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ni kuhakikisha kwamba, kufikia mwaka 2025 Tanzania lazima ibadilike kufikia kwenye uchumi wa kati na wa viwanda na kuboresha kipato cha mwananchi mmoja mmoja.

“Kuboresha maisha kwa wote na kuhakikisha elimu ya msingi inatolewa kwa wote pamoja na afya ya msingi, kuhadumisha utawala bora na wa sheria, pamoja na kujenga utamaduni wa uwajibikaji,” inaeleza Dira hiyo.

Baada ya mkutano wa Septemba 2000, nchi zote 189 za Umoja wa Mataifa, ikiwemo Tanzania, zilipitisha Malengo 7 ya Maendeleo ya Milenia (MDG) na kuahidi kuyafikia ifikapo mwaka 2015.

Malengo hayo ni pamoja na asilimia 50 ya kupunguza umaskini uliokitihiri na njaa; elimu ya msingi kwa wote; kukuza usawa wa kijinsia; kupunguza mbili ya tatu ya vifo vya watoto wachanga; kupunguza vifo vya mama wajawazito kwa robo tatu; kukabiliana na kuenea kwa VVU/UKIMWI, malaria na magonjwa mengine hatari; kuhakikisha mazingira ni endelevu; na kuendeleza ushirikiano kati ya Kaskazini na Kusini kwa ajili ya kuchochea maendeleo.

MKUKUTA pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Milenia.

Hata hivyo, mpaka kupitishwa tena kwa Malengo Endelevu ya Dunia mwaka 2015, utekelezaji wa malengo ya awali – ambayo yamehusishwa pia katika malengo mapya – ulidhoofishwa na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa misaada ya maendeleo na mtikisiko wa uchumi duniani.

Aprili 5, 2013 aliyekuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizindua ripoti ya idadi ya watu katika ngazi ya taifa, wilaya, kata na shehia jijini Dar es Salaam, aliwataka Watanzania kuzingatia matumizi ya uzazi wa mpango ili kukabiliana na ongezeko la watu ambalo linatarajiwa kufikia milioni 90 mwaka 2050.

Pinda alisema ni vyema kuzingatia uzazi wa mpango kama ilivyoainishwa katika sera ya watu ya mwaka 2006.

“Sera ya idadi ya watu inatutaka tuzae watoto ambao tunaweza kuwahudumia katika maendeleo yao ya baadaye na Taifa kwa jumla, tuachane na dhana potofu ya kwamba kuzaa watoto wengi ni umaarufu na utajiri,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Licha ya Serikali kuahidi kushirikiana na wananchi kuhimiza matumizi ya uzazi wa mpango kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na ongezeko la idadi ya watu, lakini utekelezaji wake umekuwa mgumu kutokana na wananchi wengi kutofikiwa na elimu pamoja na huduma hizo za uzazi wa mpango.

Hata hivyo, mjumbe wa Taasisi ya kutetea idadi ya watu na uzazi wa mpango Tanzania (Tanzanian Coalition for Demographic Awareness and Action – TCDAA), Halima Shariff, anasema idadi ya watu nchini Tanzania inaweza kufikia milioni 130 hadi 140 ifikapo mwaka 2050, kasi ambayo inatokana na kiwango cha kuzaliana ambacho ni wastani wa watoto watano kwa kila mwanamke nchini humo.

Takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba, kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya watu nchini Tanzania kufikia milioni 60 ifikapo mwaka 2025 kutoka idadi ya watu milioni 45 ya sasa kutokana na ongezeko la uzazi la asilimia 2.7 kila mwaka.

Kwa mujibu wa Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, katika kipindi cha miaka 10 (2002 hadi 2012) idadi ya watu iliongezeka kwa 10,485,320, hali ambayo inaonyesha kwamba, kuna uwezekano wa ongezeko la watu 1,215,000 kila mwaka.

Kutokana na kasi hiyo, kuna wasiwasi kwamba, hadi kufikia mwaka 2025 Dar es Salaam itakuwa na watu milioni 8.5 kutoka idadi ya sasa ya watu milioni 5 kutokana na ukuaji wa asilimia 5.6, hali ambayo itaongeza changamoto kubwa ya maisha jijini humo kuliko ilivyo sasa.

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 1967 hadi 2012 idadi ya watu nchini Tanzania imekua mara nne zaidi kutoka watu 12,313,469 wakati wa Sensa ya baada ya Uhuru hadi kufikia takriban milioni 45 mwaka 2012.

Zaidi ya asilimia 80 ya watu iko vijijini ambako huduma muhimu za kijamii kama afya, elimu na maji safi na salama zinapatikana kwa shida huku kipato cha wananchi wanaotegemea zaidi kilimo kama njia kuu ya uchumi kikiwa duni.

Taasisi ya TCDAA inaeleza kwamba, kutokuwepo kwa mikakati madhubuti pamoja na elimu kuhusu suala la uzazi wa mpango ndiyo chanzo kikubwa cha ongezeko hilo halina uwiano na nguvukazi ya taifa inayoweza kuchangia uchumi ili kuwafanya wananchi wafikie uchumi wa kati.

Tanzania inakabiliwa na wimbi la watu wasiozalisha kwani wengi wao ni tegemezi huku asilimia 54 ya watu wote wakiwa na umri wa chini ya miaka 20.

“Kwa takwimu hizi ni vigumu kufikia malengo ya kukuza uchumi na kuwafanya Watanzania wawe na uchumi wa kati, kwa sababu idadi kubwa ya wananchi kwa sasa ni tegemezi,” anasema Leo Bryant kutoka TCDAA.

TCDAA inaeleza kwamba, chanzo kikubwa cha ongezeko hilo la watu bila mpangilio ni kutokuwepo kwa mipango madhubuti ya elimu ya uzazi wa mpango kuanzia ngazi ya chini itakayoendana na mikakati ya serikali katika kukuza uchumi.

“Kama tunavyosema katika malengo yetu, serikali, wanasiasa na jamii kwa ujumla kwanza inapaswa kutambua kasi hii ilivyo, lakini mikakati ya taifa katika kukuza uchumi inapaswa kuendana na kasi hiyo pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango kwa sababu ongezeko hili linaathiri mipango yote ya wizara na idara zake,” imeeleza TCDAA.

Kutopatikana kwa elimu ya kutosha ya uzazi wa mpango kunachangia mimba zisizopangiliwa zikiwemo mimba za utotoni, ambapo inaelezwa kwamba asilimia 44 ya wanaopata mimba ni wasichana wenye umri wa miaka 19, ambao licha ya wao wenyewe kuwa tegemezi, lakini hawana hata elimu ya malezi.

“Watoto hawana elimu ya uzazi wa mpango na uhusiani kuanzia ngazi ya chini hadi chuo kikuu, matokeo yake ni mimba zisizopangiliwa, ongezeko la utoaji wa mimba huku asilimia karibu 42 ya watoto wakikabiliwa na tatizo la kudumaa kwa kukosa matunzo sahihi,” anaongeza Bi. Halima Shariff.

Utumiaji wa njia za uzazi wa mpango nchini Tanzania hauna kasi kubwa ambapo kwa mujibu wa takwimu za TCDAA, ni asilimia 27 tu ya Watanzania wanaotumia njia hizo.

Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Malima Lubeleje, anazungumzia ongezeko hilo la watu nchini Tanzania kama changamoto kubwa inayoweza kukwamisha maendeleo kutokana na kutojipanga kwa serikali na jamii kwa ujumla katika kukabiliana nalo.

“Ongezeko la watu linamaanisha kuongezeka kwa changamoto ya ukosefu wa ajira, kwa sababu kutakuwepo na idadi kubwa ya vijana wasio na kazi huku huduma nyingine muhimu zikikwama kutokana na bajeti ya serikali kutokidhi malengo,” anasema Lubeleje.

Mbunge huyo anasema kwamba, serikali italazimika kutenga bajeti kubwa kukidhi mahitaji ya wananchi, lakini kufikiwa kwa bajeti hiyo kunaweza kuwa changamoto nyingine kwani mapato yanaweza kuwa kidogo kutokana na wananchi wengi kutokuwa na uwezo wa kuzalisha.

“Athari za ongezeko la watu ni kubwa sana, hasa kama hakuna mipango madhubuti, maana yake hata bajeti za sekta nyingine zinazotoa huduma kama afya, elimu, maji, nishati na kadhalika nazo zitayumba kwa kuelemewa na idadi ya watu,” anaongeza.

Mchungaji William Mwamalanga anaelezea ongezeko la watu kama ni janga lingine ambalo siyo tu litayumbisha uchumi, lakini pia litaongeza migogoro mbalimbali ya kijamii, hususan ya ardhi.

“Tayari Tanzania imeshuhudia migogoro mingi ya ardhi ambapo wakulima na wafugaji wanauana wakigombea ardhi – wakulima wanataka ardhi yenye rutuba na wafugaji wanataka sehemu ya malisho kwa sababu ardhi iliyokuwa ikitumiwa zamani haina rutuba kutokana na kukosekana kwa mvua pamoja na mabadiliko ya tabianchi,” anafafanua.

Anaongeza: “Pamoja na mabadiliko hayo ya tabianchi, lakini ni jambo lililo dhahiri kwamba hivi sasa Watanzania tumeongezeka wakati ardhi yetu haiongezeki, hata kama ardhi iliyopo haijatumiwa yote, lakini lazima tuelewe kwamba siyo ardhi yote ya Tanzania inafaa kwa kilimo na shughuli nyingine za maendeleo, sehemu nyingine ni hifadhi na misitu.”

Mchungaji Mwamalanga anasema hata hivyo kwamba, njia pekee inayoweza kuinusuru Tanzania katika janga hilo ni kuhimiza elimu ya uzazi wa mpango pamoja na kuongeza bajeti ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango.

Kiongozi huyo wa kiroho ameiasa jamii kuachana na utamaduni wa kuzaa bila mpangilio kwa kuona sifa kuwa na watoto wengi wakati uwezo ni mdogo.

“Zamani ardhi ilikuwa na rutuba, ilitosha kutokana na idadi ya watu iliyokuwepo, lakini pia hata mifugo ilikuwa na malisho mengi, watu waliona fahari kuwa na watoto wengi kwa sababu walishiriki kwenye uchumi na kuleta tija, leo hii kilimo kimeyumba, hakuna mvua za kutosha na vijana wengi wanakimbilia mijini, sasa kuna faida gani ya kuwa na watoto wengi wakati wanakabiliwa na changamoto ya kiuchumi,” alihoji.

Kwa upande mwingine, Mchungaji huyo anasema kuna hatari ya uchumi wa Tanzania kuyumba hata kwa miaka 10 licha ya rasilimali zilizopo kutokana na kukosekana nguvukazi hasa kwa kuchukulia kwamba, hivi sasa asilimia 54 ya wananchi wana umri wa chini ya miaka 20.

“Hawa wote wanatakiwa kulishwa, ni tegemezi, sasa mpaka miaka 10 itakapopita ndipo tunategemea kizazi hiki kitakuwa kwenye uzalishaji, hapa hujapigia hesabu ya wazee ambao nao ni tegemezi kwa jamii,” amesema.

Mchungaji Mwamalanga anasema ni vyema serikali ikaweka msisitizo wa elimu ya uzazi wa mpango katika Mpango wa Miaka Mitano na kuongeza bajeti ili kurahisisha upatikanaji wa elimu na huduma za afya ya uzazi wa mpango na kuliokoa taifa.

Mwaka 2009, Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) lilisema kwamba, idadi kubwa ya watu ilitegemea kuongezeka na kufika bilioni 7 mwaka 2011, mwaka mmoja mapema zaidi ya ilivyotarajiwa, ambapo asilimia 95 ikiwa katika nchi zinazoendelea.

"Idadi ya watu itafika bilioni saba katika nusu ya pili ya mwaka 2011, hii ina maana kutakuwa na ongezeko katika uwekezaji wa jamii kufukuzana na ongezeko la idadi ya watu, na kusababisha kuwepo kwa fursa chache za kuongeza ubora wa huduma hasa elimu na afya, ambazo zinapaswa kuleta mabadiliko yanayohitajika kufikia Malengo ya Milenia,” alisema Jose Miguel Guzman, mkuu wa Tawi la Idadi ya Watu na Maendeleo katika Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA).

Lakini takwimu za mwaka 2013 zinaonyesha kwamba, idadi ya watu duniani tayari imekwishafikia bilioni 7.125 na inakadiriwa itafikia watu bilioni 7.4 mwaka huu 2016.

Chanzo: Kasi ya uzazi mzigo mkubwa kwa uchumi wa Tanzania | Fikra Pevu
 
Mi naona itungwe sheria rasmi. Ikibid iwepo chanjo ya kudhibiti uzaaji holela. Kwa maana hali hii ikiachwa hivi itageuka 'timing bom'. Mambo mengne yasiyoweza kurekebishwa hali ikishatokea ni bora yawe yanapewa strict attention. Au kwa vile si siasa.
 
wacha tuzae bna,nchi lote hili!..tzaane lipatikane soko na ubunifu
 
U
Mi naona itungwe sheria rasmi. Ikibid iwepo chanjo ya kudhibiti uzaaji holela. Kwa maana hali hii ikiachwa hivi itageuka 'timing bom'. Mambo mengne yasiyoweza kurekebishwa hali ikishatokea ni bora yawe yanapewa strict attention. Au kwa vile si siasa.
Ndio maana jukwaa hili lina wapiga CHABO wengi kuliko WACHANGIAJI hii inatokana na PUMBA kama hizi.UZAZI WA MPANGO NI DHAMBI.
 
kuna wakat inabid utenganishe dini/iman yako na mambo ya maendeleo ya nchi. La sivyo utafkia mahala utasema jeshi na vyombo vya ulinzi na bajet yake vifutwe kwa sababu kuna iman ya 'ukipigwa shavu la kulia geukia la kushoto!' Maendeleo ni sayansi. Na hesabu zimo. Tofautisha law v/s morality. Jikite kwenye nini kifanyike kwa hakika. Je, ningeongeza na pendekezo la watu waruhusiwe ku abort kwa hiari si utaomba wani ban! Hiyo minyororo ya kidini haitu grantee jamii kuendelea hapo mbelen. Dunia haipanuki ujue. Labda kama neno 'utafiti' kwako ni nadharia tu.
 
Ukimwi,ebola,chikungunya,vita vya wenyewe kwa wenyewe, vinatutosha sisi waafrika.
 
Itikadi kama hii ilikuwepo China. China imeitekeleza hii sera kwa kipindi kirefu sana na yenyewe imeona hiyo sera haiwasaidii bali inawafifisha. Sasa hivi wamegundua kwamba watu ni nguvukazi na soko, hivyo ukiwa na idadi kubwa ya watu unatengeneza nguvukazi na pia unakuwa na soko kubwa la kuuza bidhaa zako.
 
Jamani mnawapa taarifa Illuminati tena kwamba mbinu zao zote za kutuua kwa visukari.magonjwa yasiyotibika kama Ebola,Zika,Cholera, Ukimwi,vita,vyandarua vilivyotiwa sumu,njaa,vidonge na mbinu zingine za uzazi wa mpango,chanjo nk.havijafanikiwa kutuua!Ninyi vipi?Ngoja sasa waongeze dozi, mtakoma.
Mi naona itungwe sheria rasmi. Ikibid iwepo chanjo ya kudhibiti uzaaji holela. Kwa maana hali hii ikiachwa hivi itageuka 'timing bom'. Mambo mengne yasiyoweza kurekebishwa hali ikishatokea ni bora yawe yanapewa strict attention. Au kwa vile si siasa.
Mi naona itungwe sheria rasmi. Ikibid iwepo chanjo ya kudhibiti uzaaji holela. Kwa maana hali hii ikiachwa hivi itageuka 'timing bom'. Mambo mengne yasiyoweza kurekebishwa hali ikishatokea ni bora yawe yanapewa strict attention. Au kwa vile si siasa.
 
Siku hizi mabinti wadogo kabisa wanawatoto. Wengine wawili hadi watatu. Halafu wote wanaishi kwa bibi. Wanaume wanaowapa ujauzito nao tegemezi tu. Elimu inahitajika zaidi idadi ya watu iongezeke kwa uwiano sawa na humuda zilizopo. Bila hivi....tutegemee kaya masikini kuzidi kudidimia katika ufukara huku familia tajiri zikipaa kwa kipato na hali bora ya maisha.
 
Kwa sasa ukiwahoji kwa karibu wenye watoto wengi hasa mabinti wengi hata wao sio hesabu zao ila ni matokeo. Nadhan hata nguvu nying zielekezwe kwa wanaobebesha mimba bila hata wao kuwahitaj pengine. Kuwaelimisha wanawake tu haitasaidia. Mana hata wasomi wapo uzaz wa mpango umewashinda. Hapa ziletwe mbinu za kisasa zaid zenye side effects kidogo sio kama hizi wanatishiana madhara kibao. Pia zikubalike hata njia mbadala baada ya mimba kutungwa. Kifup mimba nyingi ni za ajari hasa hizi kaya maskini.. (Tajiri na mali zake , maskini na watoto wake).
 
Familyplanning-640x350.jpg

LENGO la kupunguza nusu ya watu wanaoishi katika umaskini na njaa nchini Tanzania na kuwafanya wawe katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 linaweza kuhatarishwa na ongezeko la idadi ya watu, zaidi katika maeneo ya vijijini.

Hali hiyo, ambayo ni pigo kwa mikakati ya Taifa ya kupunguza umaskini kama inavyoainishwa kwenye Awamu ya Pili ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II) pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo kuelekea mwaka 2025, inatokana na kasi kubwa ya ongezeko la watu nchini ambayo haiendani na mipango mingine ya maendeleo.

Miongoni mwa mambo ambayo yamesisitizwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ni kuhakikisha kwamba, kufikia mwaka 2025 Tanzania lazima ibadilike kufikia kwenye uchumi wa kati na wa viwanda na kuboresha kipato cha mwananchi mmoja mmoja.

“Kuboresha maisha kwa wote na kuhakikisha elimu ya msingi inatolewa kwa wote pamoja na afya ya msingi, kuhadumisha utawala bora na wa sheria, pamoja na kujenga utamaduni wa uwajibikaji,” inaeleza Dira hiyo.

Baada ya mkutano wa Septemba 2000, nchi zote 189 za Umoja wa Mataifa, ikiwemo Tanzania, zilipitisha Malengo 7 ya Maendeleo ya Milenia (MDG) na kuahidi kuyafikia ifikapo mwaka 2015.

Malengo hayo ni pamoja na asilimia 50 ya kupunguza umaskini uliokitihiri na njaa; elimu ya msingi kwa wote; kukuza usawa wa kijinsia; kupunguza mbili ya tatu ya vifo vya watoto wachanga; kupunguza vifo vya mama wajawazito kwa robo tatu; kukabiliana na kuenea kwa VVU/UKIMWI, malaria na magonjwa mengine hatari; kuhakikisha mazingira ni endelevu; na kuendeleza ushirikiano kati ya Kaskazini na Kusini kwa ajili ya kuchochea maendeleo.

MKUKUTA pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Milenia.

Hata hivyo, mpaka kupitishwa tena kwa Malengo Endelevu ya Dunia mwaka 2015, utekelezaji wa malengo ya awali – ambayo yamehusishwa pia katika malengo mapya – ulidhoofishwa na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa misaada ya maendeleo na mtikisiko wa uchumi duniani.

Aprili 5, 2013 aliyekuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizindua ripoti ya idadi ya watu katika ngazi ya taifa, wilaya, kata na shehia jijini Dar es Salaam, aliwataka Watanzania kuzingatia matumizi ya uzazi wa mpango ili kukabiliana na ongezeko la watu ambalo linatarajiwa kufikia milioni 90 mwaka 2050.

Pinda alisema ni vyema kuzingatia uzazi wa mpango kama ilivyoainishwa katika sera ya watu ya mwaka 2006.

“Sera ya idadi ya watu inatutaka tuzae watoto ambao tunaweza kuwahudumia katika maendeleo yao ya baadaye na Taifa kwa jumla, tuachane na dhana potofu ya kwamba kuzaa watoto wengi ni umaarufu na utajiri,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Licha ya Serikali kuahidi kushirikiana na wananchi kuhimiza matumizi ya uzazi wa mpango kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na ongezeko la idadi ya watu, lakini utekelezaji wake umekuwa mgumu kutokana na wananchi wengi kutofikiwa na elimu pamoja na huduma hizo za uzazi wa mpango.

Hata hivyo, mjumbe wa Taasisi ya kutetea idadi ya watu na uzazi wa mpango Tanzania (Tanzanian Coalition for Demographic Awareness and Action – TCDAA), Halima Shariff, anasema idadi ya watu nchini Tanzania inaweza kufikia milioni 130 hadi 140 ifikapo mwaka 2050, kasi ambayo inatokana na kiwango cha kuzaliana ambacho ni wastani wa watoto watano kwa kila mwanamke nchini humo.

Takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba, kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya watu nchini Tanzania kufikia milioni 60 ifikapo mwaka 2025 kutoka idadi ya watu milioni 45 ya sasa kutokana na ongezeko la uzazi la asilimia 2.7 kila mwaka.

Kwa mujibu wa Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, katika kipindi cha miaka 10 (2002 hadi 2012) idadi ya watu iliongezeka kwa 10,485,320, hali ambayo inaonyesha kwamba, kuna uwezekano wa ongezeko la watu 1,215,000 kila mwaka.

Kutokana na kasi hiyo, kuna wasiwasi kwamba, hadi kufikia mwaka 2025 Dar es Salaam itakuwa na watu milioni 8.5 kutoka idadi ya sasa ya watu milioni 5 kutokana na ukuaji wa asilimia 5.6, hali ambayo itaongeza changamoto kubwa ya maisha jijini humo kuliko ilivyo sasa.

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 1967 hadi 2012 idadi ya watu nchini Tanzania imekua mara nne zaidi kutoka watu 12,313,469 wakati wa Sensa ya baada ya Uhuru hadi kufikia takriban milioni 45 mwaka 2012.

Zaidi ya asilimia 80 ya watu iko vijijini ambako huduma muhimu za kijamii kama afya, elimu na maji safi na salama zinapatikana kwa shida huku kipato cha wananchi wanaotegemea zaidi kilimo kama njia kuu ya uchumi kikiwa duni.

Taasisi ya TCDAA inaeleza kwamba, kutokuwepo kwa mikakati madhubuti pamoja na elimu kuhusu suala la uzazi wa mpango ndiyo chanzo kikubwa cha ongezeko hilo halina uwiano na nguvukazi ya taifa inayoweza kuchangia uchumi ili kuwafanya wananchi wafikie uchumi wa kati.

Tanzania inakabiliwa na wimbi la watu wasiozalisha kwani wengi wao ni tegemezi huku asilimia 54 ya watu wote wakiwa na umri wa chini ya miaka 20.

“Kwa takwimu hizi ni vigumu kufikia malengo ya kukuza uchumi na kuwafanya Watanzania wawe na uchumi wa kati, kwa sababu idadi kubwa ya wananchi kwa sasa ni tegemezi,” anasema Leo Bryant kutoka TCDAA.

TCDAA inaeleza kwamba, chanzo kikubwa cha ongezeko hilo la watu bila mpangilio ni kutokuwepo kwa mipango madhubuti ya elimu ya uzazi wa mpango kuanzia ngazi ya chini itakayoendana na mikakati ya serikali katika kukuza uchumi.

“Kama tunavyosema katika malengo yetu, serikali, wanasiasa na jamii kwa ujumla kwanza inapaswa kutambua kasi hii ilivyo, lakini mikakati ya taifa katika kukuza uchumi inapaswa kuendana na kasi hiyo pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango kwa sababu ongezeko hili linaathiri mipango yote ya wizara na idara zake,” imeeleza TCDAA.

Kutopatikana kwa elimu ya kutosha ya uzazi wa mpango kunachangia mimba zisizopangiliwa zikiwemo mimba za utotoni, ambapo inaelezwa kwamba asilimia 44 ya wanaopata mimba ni wasichana wenye umri wa miaka 19, ambao licha ya wao wenyewe kuwa tegemezi, lakini hawana hata elimu ya malezi.

“Watoto hawana elimu ya uzazi wa mpango na uhusiani kuanzia ngazi ya chini hadi chuo kikuu, matokeo yake ni mimba zisizopangiliwa, ongezeko la utoaji wa mimba huku asilimia karibu 42 ya watoto wakikabiliwa na tatizo la kudumaa kwa kukosa matunzo sahihi,” anaongeza Bi. Halima Shariff.

Utumiaji wa njia za uzazi wa mpango nchini Tanzania hauna kasi kubwa ambapo kwa mujibu wa takwimu za TCDAA, ni asilimia 27 tu ya Watanzania wanaotumia njia hizo.

Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Malima Lubeleje, anazungumzia ongezeko hilo la watu nchini Tanzania kama changamoto kubwa inayoweza kukwamisha maendeleo kutokana na kutojipanga kwa serikali na jamii kwa ujumla katika kukabiliana nalo.

“Ongezeko la watu linamaanisha kuongezeka kwa changamoto ya ukosefu wa ajira, kwa sababu kutakuwepo na idadi kubwa ya vijana wasio na kazi huku huduma nyingine muhimu zikikwama kutokana na bajeti ya serikali kutokidhi malengo,” anasema Lubeleje.

Mbunge huyo anasema kwamba, serikali italazimika kutenga bajeti kubwa kukidhi mahitaji ya wananchi, lakini kufikiwa kwa bajeti hiyo kunaweza kuwa changamoto nyingine kwani mapato yanaweza kuwa kidogo kutokana na wananchi wengi kutokuwa na uwezo wa kuzalisha.

“Athari za ongezeko la watu ni kubwa sana, hasa kama hakuna mipango madhubuti, maana yake hata bajeti za sekta nyingine zinazotoa huduma kama afya, elimu, maji, nishati na kadhalika nazo zitayumba kwa kuelemewa na idadi ya watu,” anaongeza.

Mchungaji William Mwamalanga anaelezea ongezeko la watu kama ni janga lingine ambalo siyo tu litayumbisha uchumi, lakini pia litaongeza migogoro mbalimbali ya kijamii, hususan ya ardhi.

“Tayari Tanzania imeshuhudia migogoro mingi ya ardhi ambapo wakulima na wafugaji wanauana wakigombea ardhi – wakulima wanataka ardhi yenye rutuba na wafugaji wanataka sehemu ya malisho kwa sababu ardhi iliyokuwa ikitumiwa zamani haina rutuba kutokana na kukosekana kwa mvua pamoja na mabadiliko ya tabianchi,” anafafanua.

Anaongeza: “Pamoja na mabadiliko hayo ya tabianchi, lakini ni jambo lililo dhahiri kwamba hivi sasa Watanzania tumeongezeka wakati ardhi yetu haiongezeki, hata kama ardhi iliyopo haijatumiwa yote, lakini lazima tuelewe kwamba siyo ardhi yote ya Tanzania inafaa kwa kilimo na shughuli nyingine za maendeleo, sehemu nyingine ni hifadhi na misitu.”

Mchungaji Mwamalanga anasema hata hivyo kwamba, njia pekee inayoweza kuinusuru Tanzania katika janga hilo ni kuhimiza elimu ya uzazi wa mpango pamoja na kuongeza bajeti ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango.

Kiongozi huyo wa kiroho ameiasa jamii kuachana na utamaduni wa kuzaa bila mpangilio kwa kuona sifa kuwa na watoto wengi wakati uwezo ni mdogo.

“Zamani ardhi ilikuwa na rutuba, ilitosha kutokana na idadi ya watu iliyokuwepo, lakini pia hata mifugo ilikuwa na malisho mengi, watu waliona fahari kuwa na watoto wengi kwa sababu walishiriki kwenye uchumi na kuleta tija, leo hii kilimo kimeyumba, hakuna mvua za kutosha na vijana wengi wanakimbilia mijini, sasa kuna faida gani ya kuwa na watoto wengi wakati wanakabiliwa na changamoto ya kiuchumi,” alihoji.

Kwa upande mwingine, Mchungaji huyo anasema kuna hatari ya uchumi wa Tanzania kuyumba hata kwa miaka 10 licha ya rasilimali zilizopo kutokana na kukosekana nguvukazi hasa kwa kuchukulia kwamba, hivi sasa asilimia 54 ya wananchi wana umri wa chini ya miaka 20.

“Hawa wote wanatakiwa kulishwa, ni tegemezi, sasa mpaka miaka 10 itakapopita ndipo tunategemea kizazi hiki kitakuwa kwenye uzalishaji, hapa hujapigia hesabu ya wazee ambao nao ni tegemezi kwa jamii,” amesema.

Mchungaji Mwamalanga anasema ni vyema serikali ikaweka msisitizo wa elimu ya uzazi wa mpango katika Mpango wa Miaka Mitano na kuongeza bajeti ili kurahisisha upatikanaji wa elimu na huduma za afya ya uzazi wa mpango na kuliokoa taifa.

Mwaka 2009, Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) lilisema kwamba, idadi kubwa ya watu ilitegemea kuongezeka na kufika bilioni 7 mwaka 2011, mwaka mmoja mapema zaidi ya ilivyotarajiwa, ambapo asilimia 95 ikiwa katika nchi zinazoendelea.

"Idadi ya watu itafika bilioni saba katika nusu ya pili ya mwaka 2011, hii ina maana kutakuwa na ongezeko katika uwekezaji wa jamii kufukuzana na ongezeko la idadi ya watu, na kusababisha kuwepo kwa fursa chache za kuongeza ubora wa huduma hasa elimu na afya, ambazo zinapaswa kuleta mabadiliko yanayohitajika kufikia Malengo ya Milenia,” alisema Jose Miguel Guzman, mkuu wa Tawi la Idadi ya Watu na Maendeleo katika Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA).

Lakini takwimu za mwaka 2013 zinaonyesha kwamba, idadi ya watu duniani tayari imekwishafikia bilioni 7.125 na inakadiriwa itafikia watu bilioni 7.4 mwaka huu 2016.

Chanzo: Kasi ya uzazi mzigo mkubwa kwa uchumi wa Tanzania | Fikra Pevu
Mawazo ya kipuuzi sana hayo, pamoja na data uchwara ulizoweka hapa.

Kuna wakati Tanzania imewahi kuwa na population kubwa zaidi ya China, Nigeria, Indonesia, brazil au Malasia?

Hizo zimeendelea kukua kiuchumi kwa sababu ya population kubwa.

Population inaleta faida chanya zifuatazo ndugu;

Moja; Ubunifu (creativity), mkiwa wachache let's say 70% ya wasomi wote wameajiriwa (Serikalini au private), nani atashughulika na ubunifu? Population huleta changamoto za vichwani na kuwafanya watu kuwa critical thinkers and innovators!

Mbili, Population ni factor kubwa na pekee (nasema ni silaha kuu ya Taifa). Unapoona hao mashoga wa ulaya na marekani wanafinance program za birth control siyo kwamba wanakupenda kivile mzee baba, wanajua mkiwa wachache watawacontrol kirahisi kwa kadiri ya matakwa yao!

Tatu, angalia Taifa kama ujerumani au hata Canada, kinachowakuta hivi sasa baada ya kucontrol population? Hawana nguvu kazi ya Taifa as a result wameruhusu uhamiaji maradufu ili wapate nguvu kazi. (Uko tayari tayari kwa hilo kama Taifa na unajua madhara yake in the long run).

Nne, kwa kuwa na population kubwa maana yake Taifa linajihakikishia "enough and competent cheep labour ". Hili ndo limewapaisha China, India na Brazil! Ulaya yote na marekani production kubwa wanafanya "outsourcing China au India " kwa sababu kuna cheep labour lakini ambao ni competent. Ndiyo unaona product imeandikwa (made or assembled in China for Apple).

Note: Kwakuwa hatutaki kufikiri kwa vichwa vyetu kama Taifa, Acha wenye vichwa watusaidie kufikiri na kuamua.
 
Familyplanning-640x350.jpg

LENGO la kupunguza nusu ya watu wanaoishi katika umaskini na njaa nchini Tanzania na kuwafanya wawe katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 linaweza kuhatarishwa na ongezeko la idadi ya watu, zaidi katika maeneo ya vijijini.

Hali hiyo, ambayo ni pigo kwa mikakati ya Taifa ya kupunguza umaskini kama inavyoainishwa kwenye Awamu ya Pili ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II) pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo kuelekea mwaka 2025, inatokana na kasi kubwa ya ongezeko la watu nchini ambayo haiendani na mipango mingine ya maendeleo.

Miongoni mwa mambo ambayo yamesisitizwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ni kuhakikisha kwamba, kufikia mwaka 2025 Tanzania lazima ibadilike kufikia kwenye uchumi wa kati na wa viwanda na kuboresha kipato cha mwananchi mmoja mmoja.

“Kuboresha maisha kwa wote na kuhakikisha elimu ya msingi inatolewa kwa wote pamoja na afya ya msingi, kuhadumisha utawala bora na wa sheria, pamoja na kujenga utamaduni wa uwajibikaji,” inaeleza Dira hiyo.

Baada ya mkutano wa Septemba 2000, nchi zote 189 za Umoja wa Mataifa, ikiwemo Tanzania, zilipitisha Malengo 7 ya Maendeleo ya Milenia (MDG) na kuahidi kuyafikia ifikapo mwaka 2015.

Malengo hayo ni pamoja na asilimia 50 ya kupunguza umaskini uliokitihiri na njaa; elimu ya msingi kwa wote; kukuza usawa wa kijinsia; kupunguza mbili ya tatu ya vifo vya watoto wachanga; kupunguza vifo vya mama wajawazito kwa robo tatu; kukabiliana na kuenea kwa VVU/UKIMWI, malaria na magonjwa mengine hatari; kuhakikisha mazingira ni endelevu; na kuendeleza ushirikiano kati ya Kaskazini na Kusini kwa ajili ya kuchochea maendeleo.

MKUKUTA pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Milenia.

Hata hivyo, mpaka kupitishwa tena kwa Malengo Endelevu ya Dunia mwaka 2015, utekelezaji wa malengo ya awali – ambayo yamehusishwa pia katika malengo mapya – ulidhoofishwa na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa misaada ya maendeleo na mtikisiko wa uchumi duniani.

Aprili 5, 2013 aliyekuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizindua ripoti ya idadi ya watu katika ngazi ya taifa, wilaya, kata na shehia jijini Dar es Salaam, aliwataka Watanzania kuzingatia matumizi ya uzazi wa mpango ili kukabiliana na ongezeko la watu ambalo linatarajiwa kufikia milioni 90 mwaka 2050.

Pinda alisema ni vyema kuzingatia uzazi wa mpango kama ilivyoainishwa katika sera ya watu ya mwaka 2006.

“Sera ya idadi ya watu inatutaka tuzae watoto ambao tunaweza kuwahudumia katika maendeleo yao ya baadaye na Taifa kwa jumla, tuachane na dhana potofu ya kwamba kuzaa watoto wengi ni umaarufu na utajiri,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Licha ya Serikali kuahidi kushirikiana na wananchi kuhimiza matumizi ya uzazi wa mpango kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na ongezeko la idadi ya watu, lakini utekelezaji wake umekuwa mgumu kutokana na wananchi wengi kutofikiwa na elimu pamoja na huduma hizo za uzazi wa mpango.

Hata hivyo, mjumbe wa Taasisi ya kutetea idadi ya watu na uzazi wa mpango Tanzania (Tanzanian Coalition for Demographic Awareness and Action – TCDAA), Halima Shariff, anasema idadi ya watu nchini Tanzania inaweza kufikia milioni 130 hadi 140 ifikapo mwaka 2050, kasi ambayo inatokana na kiwango cha kuzaliana ambacho ni wastani wa watoto watano kwa kila mwanamke nchini humo.

Takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba, kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya watu nchini Tanzania kufikia milioni 60 ifikapo mwaka 2025 kutoka idadi ya watu milioni 45 ya sasa kutokana na ongezeko la uzazi la asilimia 2.7 kila mwaka.

Kwa mujibu wa Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, katika kipindi cha miaka 10 (2002 hadi 2012) idadi ya watu iliongezeka kwa 10,485,320, hali ambayo inaonyesha kwamba, kuna uwezekano wa ongezeko la watu 1,215,000 kila mwaka.

Kutokana na kasi hiyo, kuna wasiwasi kwamba, hadi kufikia mwaka 2025 Dar es Salaam itakuwa na watu milioni 8.5 kutoka idadi ya sasa ya watu milioni 5 kutokana na ukuaji wa asilimia 5.6, hali ambayo itaongeza changamoto kubwa ya maisha jijini humo kuliko ilivyo sasa.

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 1967 hadi 2012 idadi ya watu nchini Tanzania imekua mara nne zaidi kutoka watu 12,313,469 wakati wa Sensa ya baada ya Uhuru hadi kufikia takriban milioni 45 mwaka 2012.

Zaidi ya asilimia 80 ya watu iko vijijini ambako huduma muhimu za kijamii kama afya, elimu na maji safi na salama zinapatikana kwa shida huku kipato cha wananchi wanaotegemea zaidi kilimo kama njia kuu ya uchumi kikiwa duni.

Taasisi ya TCDAA inaeleza kwamba, kutokuwepo kwa mikakati madhubuti pamoja na elimu kuhusu suala la uzazi wa mpango ndiyo chanzo kikubwa cha ongezeko hilo halina uwiano na nguvukazi ya taifa inayoweza kuchangia uchumi ili kuwafanya wananchi wafikie uchumi wa kati.

Tanzania inakabiliwa na wimbi la watu wasiozalisha kwani wengi wao ni tegemezi huku asilimia 54 ya watu wote wakiwa na umri wa chini ya miaka 20.

“Kwa takwimu hizi ni vigumu kufikia malengo ya kukuza uchumi na kuwafanya Watanzania wawe na uchumi wa kati, kwa sababu idadi kubwa ya wananchi kwa sasa ni tegemezi,” anasema Leo Bryant kutoka TCDAA.

TCDAA inaeleza kwamba, chanzo kikubwa cha ongezeko hilo la watu bila mpangilio ni kutokuwepo kwa mipango madhubuti ya elimu ya uzazi wa mpango kuanzia ngazi ya chini itakayoendana na mikakati ya serikali katika kukuza uchumi.

“Kama tunavyosema katika malengo yetu, serikali, wanasiasa na jamii kwa ujumla kwanza inapaswa kutambua kasi hii ilivyo, lakini mikakati ya taifa katika kukuza uchumi inapaswa kuendana na kasi hiyo pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango kwa sababu ongezeko hili linaathiri mipango yote ya wizara na idara zake,” imeeleza TCDAA.

Kutopatikana kwa elimu ya kutosha ya uzazi wa mpango kunachangia mimba zisizopangiliwa zikiwemo mimba za utotoni, ambapo inaelezwa kwamba asilimia 44 ya wanaopata mimba ni wasichana wenye umri wa miaka 19, ambao licha ya wao wenyewe kuwa tegemezi, lakini hawana hata elimu ya malezi.

“Watoto hawana elimu ya uzazi wa mpango na uhusiani kuanzia ngazi ya chini hadi chuo kikuu, matokeo yake ni mimba zisizopangiliwa, ongezeko la utoaji wa mimba huku asilimia karibu 42 ya watoto wakikabiliwa na tatizo la kudumaa kwa kukosa matunzo sahihi,” anaongeza Bi. Halima Shariff.

Utumiaji wa njia za uzazi wa mpango nchini Tanzania hauna kasi kubwa ambapo kwa mujibu wa takwimu za TCDAA, ni asilimia 27 tu ya Watanzania wanaotumia njia hizo.

Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Malima Lubeleje, anazungumzia ongezeko hilo la watu nchini Tanzania kama changamoto kubwa inayoweza kukwamisha maendeleo kutokana na kutojipanga kwa serikali na jamii kwa ujumla katika kukabiliana nalo.

“Ongezeko la watu linamaanisha kuongezeka kwa changamoto ya ukosefu wa ajira, kwa sababu kutakuwepo na idadi kubwa ya vijana wasio na kazi huku huduma nyingine muhimu zikikwama kutokana na bajeti ya serikali kutokidhi malengo,” anasema Lubeleje.

Mbunge huyo anasema kwamba, serikali italazimika kutenga bajeti kubwa kukidhi mahitaji ya wananchi, lakini kufikiwa kwa bajeti hiyo kunaweza kuwa changamoto nyingine kwani mapato yanaweza kuwa kidogo kutokana na wananchi wengi kutokuwa na uwezo wa kuzalisha.

“Athari za ongezeko la watu ni kubwa sana, hasa kama hakuna mipango madhubuti, maana yake hata bajeti za sekta nyingine zinazotoa huduma kama afya, elimu, maji, nishati na kadhalika nazo zitayumba kwa kuelemewa na idadi ya watu,” anaongeza.

Mchungaji William Mwamalanga anaelezea ongezeko la watu kama ni janga lingine ambalo siyo tu litayumbisha uchumi, lakini pia litaongeza migogoro mbalimbali ya kijamii, hususan ya ardhi.

“Tayari Tanzania imeshuhudia migogoro mingi ya ardhi ambapo wakulima na wafugaji wanauana wakigombea ardhi – wakulima wanataka ardhi yenye rutuba na wafugaji wanataka sehemu ya malisho kwa sababu ardhi iliyokuwa ikitumiwa zamani haina rutuba kutokana na kukosekana kwa mvua pamoja na mabadiliko ya tabianchi,” anafafanua.

Anaongeza: “Pamoja na mabadiliko hayo ya tabianchi, lakini ni jambo lililo dhahiri kwamba hivi sasa Watanzania tumeongezeka wakati ardhi yetu haiongezeki, hata kama ardhi iliyopo haijatumiwa yote, lakini lazima tuelewe kwamba siyo ardhi yote ya Tanzania inafaa kwa kilimo na shughuli nyingine za maendeleo, sehemu nyingine ni hifadhi na misitu.”

Mchungaji Mwamalanga anasema hata hivyo kwamba, njia pekee inayoweza kuinusuru Tanzania katika janga hilo ni kuhimiza elimu ya uzazi wa mpango pamoja na kuongeza bajeti ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango.

Kiongozi huyo wa kiroho ameiasa jamii kuachana na utamaduni wa kuzaa bila mpangilio kwa kuona sifa kuwa na watoto wengi wakati uwezo ni mdogo.

“Zamani ardhi ilikuwa na rutuba, ilitosha kutokana na idadi ya watu iliyokuwepo, lakini pia hata mifugo ilikuwa na malisho mengi, watu waliona fahari kuwa na watoto wengi kwa sababu walishiriki kwenye uchumi na kuleta tija, leo hii kilimo kimeyumba, hakuna mvua za kutosha na vijana wengi wanakimbilia mijini, sasa kuna faida gani ya kuwa na watoto wengi wakati wanakabiliwa na changamoto ya kiuchumi,” alihoji.

Kwa upande mwingine, Mchungaji huyo anasema kuna hatari ya uchumi wa Tanzania kuyumba hata kwa miaka 10 licha ya rasilimali zilizopo kutokana na kukosekana nguvukazi hasa kwa kuchukulia kwamba, hivi sasa asilimia 54 ya wananchi wana umri wa chini ya miaka 20.

“Hawa wote wanatakiwa kulishwa, ni tegemezi, sasa mpaka miaka 10 itakapopita ndipo tunategemea kizazi hiki kitakuwa kwenye uzalishaji, hapa hujapigia hesabu ya wazee ambao nao ni tegemezi kwa jamii,” amesema.

Mchungaji Mwamalanga anasema ni vyema serikali ikaweka msisitizo wa elimu ya uzazi wa mpango katika Mpango wa Miaka Mitano na kuongeza bajeti ili kurahisisha upatikanaji wa elimu na huduma za afya ya uzazi wa mpango na kuliokoa taifa.

Mwaka 2009, Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) lilisema kwamba, idadi kubwa ya watu ilitegemea kuongezeka na kufika bilioni 7 mwaka 2011, mwaka mmoja mapema zaidi ya ilivyotarajiwa, ambapo asilimia 95 ikiwa katika nchi zinazoendelea.

"Idadi ya watu itafika bilioni saba katika nusu ya pili ya mwaka 2011, hii ina maana kutakuwa na ongezeko katika uwekezaji wa jamii kufukuzana na ongezeko la idadi ya watu, na kusababisha kuwepo kwa fursa chache za kuongeza ubora wa huduma hasa elimu na afya, ambazo zinapaswa kuleta mabadiliko yanayohitajika kufikia Malengo ya Milenia,” alisema Jose Miguel Guzman, mkuu wa Tawi la Idadi ya Watu na Maendeleo katika Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA).

Lakini takwimu za mwaka 2013 zinaonyesha kwamba, idadi ya watu duniani tayari imekwishafikia bilioni 7.125 na inakadiriwa itafikia watu bilioni 7.4 mwaka huu 2016.

Chanzo: Kasi ya uzazi mzigo mkubwa kwa uchumi wa Tanzania | Fikra Pevu
Wacha watu wazaliane .Tumeona kuna watu wana watoto mmoja au watatu wana maisha magumu sana.pia hata huko ulaya hawana nguvu kazi tena wamebaki wazee tu.Tanzania tunaenda uchumi wa viwanda nani atafanya hizo kazi.china kwenyewe wameongeza kutoka mtoto mmoja hadi wawili.
 
Isitungwe sheria bali kasi ya elimu ya uzazi wa mpango iongezwe.
 
Back
Top Bottom