Kasi ya utendaji wa Kassim Majaliwa imepungua sana, sio kama wakati wa Hayati Dkt. Magufuli

Wakati wa hayati JPM waziri mkuu Majaliwa alikuwa akifanya ziara mahala watu uharo unawatoka.

Alikuwa akitoa matamko kila mtumishi wa umma anatapika nyongo.

Kwa ufupi naona kama alikuwa ameendana na kasi ya mwendazake. Ndio maana ilikuwa ukisikia rais yupo mahala fulani moto unawaka huku waziri mkuu akikolozea moto. Kwa ujumla waliweka mambo sawa, kuanzia tumbuatumbua, dhibiti rushwa na hata dhibiti uzembe.

Nini kimemsibu sasa hivi mpaka amepunguza kasi aliyokuwa nayo?
Keshaona kuna Rais wa michongo ndo maana kaamua kupunguza kasi
 
Anajua hatakiwi kumzidi kasi bosi wake. Akijaribu atakuwa amejiondoa kwenye ka-mkeka ka kuwania urais 2030.
Bodi ya TPA imevunjwa na Rais sababu ya madudu yaliyogunduliwa na Waziri Mkuu...Kwa kuwa hana Mamlaka ya kuvunja Bodi alikabidhi Taarifa kwa Rais Samia Suluhu Hassan akachukua hatua kwa maslahi mapana ya Nchi yetu
 
Leo tunashuhudia Kakoko akipandishwa mahakamani kwa ubadhirifu. Haya yote aliyagundua PM katika Ziara aliyoifanya bandarini
 
Sijawahi kuwa na mashaka na utendaji Kazi wa Waziri Mkuu toka akiwa Mkuu wa Wilaya yetu pale Rufiji alikuwa Mtumishi kweli kweli... Mkataa Rushwa na ufisadi
 
Wenzako Bado tunamuhita mzee wa speed na viwango..
Kilicho fanyika Bandari umefumba Macho
Kwenye Halmashauri huko wanatumbuliwa umefumba Macho
Migodini huko umefumba Macho

Ila wabongo nimewanyooshea Miko mtu ata afanye Nini Mnapotezea Ila mnasubiri mpake ndio mjee kutoa pongezi zake..

Majaliwa anaupiga Mwingi Sana acheni chuki binafsi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom