Kasi ya Rais Magufuli yawavuruga Chadema waona ni heri muasisi mtendaji pekee mzee Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,765
Kasi ya Rais Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo imewavuruga kabisa wafuasi wa Chadema kiasi cha kushindwa kumuona mbadala wa Mbowe katika nafasi ya Mwenyekiti.

Kwa sasa kila anayetamani kuchukua fomu anaonekana ana mahaba na CCM isipokuwa Freeman pekee ambaye yuko Chadema tokea mwaka 1992 wakati chama hicho kinaasisiwa. Kinachosahaulika hapa ni kuwa mzee Mbowe alikuwa mwanaccm kabla Chadema haijazaliwa.

Tatizo la Chadema siyo Mbowe bali ni tishio la chama hicho kumezwa na CCM na nafasi yake kama chama kikuu cha Upinzani kuchukuliwa na ACT wazalendo ambayo ina uhakika wa kupata wabunge kutoka Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Tayari Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru ameshasema ana barua lukuki kutoka kwa wabunge na madiwani wa Chadema wanaoomba kujiunga CCM.

Kiuhalisia kilichomkimbiza mzee Sumaye pale Ufipa siyo " kuonja sumu kwa kulamba " bali kaisoma kasi ya Magufuli na kugundua kuwa Chadema inaelekea kibra na wengi watamfuata Sumaye kabla ya Krismas na mwaka mpya.

Maendeleo hayana vyama!
 
John Mbatizaji umeandika nini hasa main topic nini??
Mara Sumai mara Mbowe hueleweki, sema point yako!!
 
Ni aibu kwa mtu "anayedhaniwa" kuwa na akili timamu kudai "kuletewa" maendeleo! Magufuli anamletea nani maendeleo???/ Subiri uletewe kila kitu hadi msosi!
 
Sawa ila kasi ya kuisambaratisha CHADEMA imemchanganya maana mawakala wake wanarudi nyumbani kuliko noga bila CHADEMA kusambaratika. Bado wachache waliobaki wanasubiri behewa lirudi kuwachukua.
 
Watanzania siku tutakayo acha unafiki na njaa zetu ndiyo siku tutakayolikomboa Taifa hili, otherwise tutakesha!! Inaweza ukakuta aliyeandika hiyo post ni mtu msomi ameenda shule kapata elimu!! Kabisa kweli mtu anashabikia kinafiki mambo yanayoendelea nchini!! Democracy iko wapi, Uhuru uko wapi, siasa za mizani ziko wapi!!!? Najionea huruma!! Tutaangamia kwa kukosa maarifa kwa huu unafiki na uzandiki!! Acha tukipate cha mtema kuni, uzuri ni kwamba mapigo yanapokuja hayachagui mnafiki, adha tunaipata wote!! Tuendelee tu!!
 
Wewe jamaa nimekuwa nakufuatilia muda mrefu sana humu kwenye jukwaa nimegundua una IQ ndogo mno since then nimekuwa nakupuuza sana kila post yako huwa nai ignore then naendelea na mambo yangu
 
Kutegemea CDM ya Mbowe ina future na huu mtindo wa "susasusa" ni zaidi ya ukichaa.

2020 siyo mbali!
 
Umewahi fikiria ccm kuendelea kubaki madarakani ni sababu ya Mbowe.Iko hivo busara za mbowe ndizo zimeshikilia amani yetu,mfano akipewa mwingine asiyekubali kuonewa vipi akimwaga vijana mtaani kudai haki zao huo ndo itakuwa mwisho Wa ccm na ccm ikifa na buku saba zitakufa
 
Kaka usijitoe ufahamu kama huishi Tanzania.. Yanayoendelea nadhani unayajua sana na hata andiko lako ni kinyume chake.. Waachie wajinga kama Kawe Alumni na The State Agent ndo akili kama hizi zinawatosha.. Wenye uelewa na wanaofahamu hujuma zinazofanywa zikiwemo kuua, kuteka, kuhujumu kila juhudi njema za chama, kuharibu mali, kubambikia kesi, kunyima mikutato, kutesa, kutumi polisi, mahakama, msajili wa vyama, tume ya uchaguzi, TISS, mamluki, vyombo vya habari, kudhuru na mengine mengi ya kutisha kwa WANACHADEMA. Hata kama ni wafia chama CCM hawasemi zaidi ya kuowanea huruma Wapinzani.. usijitoe ufahamu bali waza out of CCM na Ushabiki usiobalance mambo kiuhlisia.. Mngehangaika na kina Lipumba na Mrema TLP plus Mbatia.. Waache chadem kama watakufa iwe furaha yenu..Unafiki ni chukizo..
 
Back
Top Bottom