Kasi ya Mwigulu, Nape itakiangamiza CCM

bullet proof

Member
Sep 19, 2012
57
35
Kwanza kabisa nieleze tu kwamba mimi ni mpenzi na mwanachama wa CCM, ila nashitushwa sana na kasi ya viongozi hawa wa chama, Mwigulu (naibu katibu mkuu) na Nape (katibu mwenezi).

Viongozi hawa ni ukweli uliowazi kuwa wameshindwa kabisa kukiongoza chama kwa imani na itikadi za CCM. Wanatumia muda mwingi kushindana/kugombana na Chadema badala ya kuwa na mipango thabiti ya kukiimarisha chama. Matokeo ya aina ya siasa zao ni:

Kwanza, wanazidisha mpasuko wa kisiasa ndani ya chama cha mapinduzi. Hii ni kwa namna wanavyopitiwa na vuguvugu la kisiasa nchini linaloongozwa na CHADEMA kwa 'lebo' ya ufisadi. Hili liliwafanya waje na kauli mbiu ya kujivua gamba kwa wanaCCM 'wanaotuhumiwa' (kwa sababu za kisiasa) bila kujua kwamba kwa kufanya hivi wanakiongezea nguvu CHADEMA.

Pili, siasa zao za mabavu na ubabe zinaamsha chuki za wananchi dhidi ya CCM. Vyovyote inavyokuwa, watz hubaki kuwa wapenda amani tu. Matukio ya hv karibuni yanavyofanywa na viongozi hawa, hasa Nchemba, yanafanya CCM kichukiwe 7ana
 
Back
Top Bottom