Kasi ya maambukizi ya VVU ni kubwa asema Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kasi ya maambukizi ya VVU ni kubwa asema Pinda

Discussion in 'JF Doctor' started by fangfangjt, Apr 5, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Hussein Issa na Fidelis Butahe
  Mwananchi

  WAKATI safari za wananchi kwenda katika Kijiji cha Samunge, Loliondo kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila, kupata tiba ya magonjwa sugu,ukiwemo Ukimwi zikizidi kuongezeka, imeelezwa kuwa Watanzania milioni moja na nusu huambukizwa virusi vya ugonjwa Ukimwi kila mwaka.

  Takwimu za serikali kuhusu maambukizi ya virusi vya Ukimwi, zinaonyesha kuwa mwaka 2003/2004 maabukizi yalikuwa asilimia saba wakati mwaka 2007/2008 yakishuka hadi kufikia asilimia 5.7.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana wakati wa uzinduzi wa mkakati Kitaifa wa kudhibiti maambukizi ya Ukimwi,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema asilimia 10 ya watoto wanaozaliwa na asilimia 8.2 na wanawake wajawazito wanaambukizwa virusi.

  Alisema katika maeneo ya mijini, kiwango cha maambukizo kimefikia zaidi ya asilimia tisa wakati katika maeneo ya vijijini, kimefikia asilimia tano.

  "Zaidi ya asilimia 80 ya maambukizo yanatokana na kujamiana, asilimia 18 yanatoka kwa mama kwenda kwa mtoto na asilimia 1.8 yanatokana na njia nyingine," alisema Pinda.

  Alisema zaidi ya nusu ya Watanzania hawajapima afya zao ambapo asilimia 11 ya watoto wa chini ya miaka 15 wameshaanza ngono hali ambayo ni hatari kwa nchi.

  Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk AshaRose Migiro, alisema hali ya ukimwi duniani inatisha na kwamba wanaoathirika ni pamoja na viongozi.

  Alielezea kusikitishwa kwake kuhusu matukio ya viongozi wa nchi kupoteza maisha kwa ugonjwa huo.

  Aliisifu Tanzania kwa kuwa na mpango kabambe wa kudhibiti maambukizi, jambo jambo ambalo kwa kiasi fulani limesaidia kupunguza maambukizi.

  Alisema kinachotakiwa ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu maabukizi ya ugonjwa huo, unaoangamiza wanawake wengi na watoto.
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  aisifuye mvua imemnyea
   
Loading...