Kasi ya kuuza viwanja awamu hii inaongezeka

Senior Boss

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
3,405
3,685
Salaam wandugu,

Well in my unofficial independent study nimekuja gundua awamu hii ya 5 watu wameanza kupigika mbayaa mzunguko wa hela ki ukweli umekua utata mtupu...kasi ya kukopa bank imepungua, turnover zime drop yet standards of living remain the same.

Hii imesababisha watu kadhaa kama sio wengi ninao wafahamu kuuza maeneo yao so as kufukia mashimo i.e. life expenses, loans, family needs etc. Jamani kama ulipiga hela awamu iliyopita plz use ur money wisely...unaweza kuja nunua ma viwanja bei chee tu kila siku tunaona. Watu hela hamna. Lol

Watu wanapigwa mikopo binafsi hawachomoi....kiwanja/nyumba hyo imeenda. Patience is the talent. Just stay calm & watch.
 
Hata mimi nina mpango wa kuuza kiwanja changu ile niweze kumalizia nyumba yangu nihamie. Kwa huyu Pombe sidhani kama nitaweza kupata hela ya pango/rent, maana posho iliyokuwa inanipa jeuri imeondolewa.

Lakini Pombe ajue morali ya kazi itapungua sana kwa watumishi wa umma. Yeye na aendelee kula maugali ya bure huko Ikulu, wenzie huku kila kitu tunanunua.
 
Aisee ni shida sanaa. Yan at some point we all need to re-organise our finances. Otherwise tutaangamia.
 
Ni kweli kabisa maisha yamebana sana,hata mimi nauza viwanja vyangu hapa MOSHONO,Arusha jirani na kambi ya JWTZ.
Kama mtu hukujenga miaka iliyopita,subiri awamu ya tano ipite ndio ujenge.
Yaani sasa hivi hata michepuko haipati wateja wa kuwapangishia self contained house/apartment.

Salaam wandugu,

Well in my unofficial independent study nimekuja gundua awamu hii ya 5 watu wameanza kupigika mbayaa mzunguko wa hela ki ukweli umekua utata mtupu...kasi ya kukopa bank imepungua, turnover zime drop yet standards of living remain the same.

Hii imesababisha watu kadhaa kama sio wengi ninao wafahanu kuuza maeneo yao so as kufukia mashimo i.e. life expenses, loans, family needs etc. Jamani kama ulipiga hela awamu iliyopita plz use ur money wisely...unaweza kuja nunua ma viwanja bei chee tu kila siku tunaona. Watu hela hamna. Lol

Watu wanapigwa mikopo binafsi hawachomoi....kiwanja/nyumba hyo imeenda. Patience is the talent. Just stay calm & watch.
 
Ni kweli kabisa maisha yamebana sana,hata mimi nauza viwanja vyangu hapa MOSHONO,Arusha jirani na kambi ya JWTZ.
Kama mtu hukujenga miaka iliyopita,subiri awamu ya tano ipite ndio ujenge.
Yaani sasa hivi hata michepuko haipati wateja wa kuwapangishia self contained house/apartment.
Yan man hustles ni nyingi but low money circulation kwa system. Yan mtu unapigana ila hela haiji. Otherwise ni vile tu channel out tuuze masoko ya nnje.
 
Wenye malori ya mizigo walokuwa wanategemea kubeba contena na mizigo ya dili nao wamefulia kuna jamaa kauza masemi trela sita kwa mkupuo..kwa bei cheee ukiuliza nini alikopa bank so kaona apunguze malori yake
Ni kweli. Hata mimi kuna watu nawafahamu walikuwa na semi trailers kadhaa lakini wameuza baadhi na pia kupunguza wafanyakazi.
 
Study yako umefanyia maeneo gani ili tuje tujizolee viwanja vya bei nafuu? Nakwambia wale waliojiwekea hazina kwenye land and other assets watapata unafuu ktk kipindi hiki. Shida kwetu sie 'Makapuku forum' ambao hatuna assets...
 
Kweli kabisa kiongozi mana hata hi biashara mpaka sometime naona kama nawafanyia watu mzunguko mdogo raia wanalia hali ngumu wanataka kukopa afu tatizo kulipa bado anadaiwa pango+ada+hela ya msosi kwa familia daily+vocha+bili za maji,umeme na nk...Watu wanadata na maisha haya kwanza. Siku hizi kama una girlfriend/boyfriend ukimkaribisha kwako jiangalie unaweza pigwa tukio usiamini
 
Hata mwaka haujaisha tayari tushaisoma namba. JPM kanikatia mrija wa ulaji, sina hamu nae
 
Study yako umefanyia maeneo gani ili tuje tujizolee viwanja vya bei nafuu? Nakwambia wale waliojiwekea hazina kwenye land and other assets watapata unafuu ktk kipindi hiki. Shida kwetu sie 'Makapuku forum' ambao hatuna assets...
Ila pia kuna uwezekano wa kuuza kwa bei ya hasara kwa vile wanunuzi hawana hela. Mfano kama mtu ulikuwa umenunua kiwanja miaka mitatu iliyopita kwa milioni 10 kama ungeuza hicho kiwanja mwaka jana ungeweza kupata mteja wa milioni 20. Lakini kama ukikiuza leo utaishia kukiuza kwa milioni 15 au chini zaidi ya hapo.
 
Acheni kujidanganya eti ardhi itashuka bei,walipotoka waliokuwepo ndipo wanapoingia wasiokuwepo!channel zimebadili tu watu,wasiokuwanacho juzi na jana wanapata leo.
Tayari majina mapya yameshaanza kuibuka mjini.
 
Sasa hivi kuna kina Papaa nani au Mapedeshee gani wapya ambao wamenufaika na utawala mpya? Lete majina yao hapa...
 
Back
Top Bottom