Kasi ya kupeleka umeme vijijini imepungua sana, kulikoni?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
8,128
2,000
Ni vigumu kusafiri kwenda mbali kusema habari za mazingira kama wananchi bado wanawasha moto wa Kuni ili TU kupata mwanga wa kumulikia usiku kusoma na kupika jikoni.

Kama Mtu hana njia nyingine ya kupika chakula chake lazima awashe moto wa Kuni au mkaa hayo mazingira yatatunzwa namna gani, tunaenda kufanya nini kwenye mkutano wa mazingira wakati gesi yetu asili hatujaielekeza kwenye kupunguza matumizi ya Kuni, mkaa na petroli kwa watu wetu.

Nani ameturoga?
 
Tui

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
1,281
2,000
Mkuu reasoning yako ni kwamba tusiende kwenye mkutano wa Mazingira kwa sababu hatujatimiza malengo yanayohitajika?

Mkutano ungekuwa na faida gani kama Nchi zote zingekuwa zimetatua changamoto za mazingira? Lengo la mkutano ni kutatua changamoto za tabianchi na mazingira.

Hakuna Nchi yeyote iliyofikia malengo yaliyowekwa. Nchi zilizoendelea ndio polluters wakubwa kwa asilimia.

Mikutano hii ni kubadilishana mawazo na uwezo wa kutatua changamoto hii ambayo ni tishio kwetu na kwa vizazi vijavyo.
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
8,128
2,000
Mkuu reasoning yako ni kwamba tusiende kwenye mkutano wa Mazingira kwa sababu hatujatimiza malengo yanayohitajika?
Mkutano ungekuwa na faida gani kama Nchi zote zingekuwa zimetatua changamoto za mazingira?...
Charity begins at home, unapomulika (mtafuta) nyoka anzia miguuni mwako. Safari moja ya kwenda kwenye mkutano inagharimu nguzo ngapi za kusambaza umeme vijijini ili watu wapunguze kukata misitu?

Kwani pale kwenye mkutano tumekwenda kusema na kufanya kitu gani ambacho hakifahamiki? Nani hajui kuwa Marekani, China, India na Ulaya ndiyo wachafuzi wakubwa wa mazingira? Nani amekwenda kutaja jambo jipya pale?

Sisi tunapaswa kufanya kila kitu kwenye uwezo wetu (play our part) kuhakikisha kuwa umeme unawaka nchi nzima, gesi yetu inatumika majumbani na kwenye magari na mashine, bei ya saruji inashuka bei ili watu waache kujenga kuta za nyumba za miti, bei ya umeme inashuka ili watu wapike kwa kutumia umeme badala ya Kuni na mkaa na kupanda miti.

Sasa tunakwenda kunyooshea wengine kidole kimoja wakati vidole 3 vimeelekea kwetu.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,626
2,000
Na pesa ya REA ipo maana kuna tozo kwaajili yao. Watupe majibu kuwa pesa za REA wanapeleka wapi.
 
Tui

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
1,281
2,000
Kwenda kwenye mikutano haitunyimi kufanya yote hayo uliyoyaorodhesha.Ukiwa signatory wa hiyo mikataba huwezi kuacha kwenda kwenye mikutano kwa kusingizia priorities zingine.Faida ya mikutano hiyo diplomasia ni kubwa .
 
Kwani mkutano mmoja kama huu unatugharimu sh. ngapi? Labda tuanzie hapo. Hela hizo zingetosha kupanda miti mingapi inayoweza kunyonya gesi chafu?

Ndugu zangu we have to think globally and act locally, na sio to think locally and and act globally.
 
gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,072
2,000
Kichwa cha habari hakina uhusiano kabisa na kilichoandikwa ndani.Tujifunze uandishi mzuri sio ilimradi tu.
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
8,128
2,000
Kichwa cha habari hakina uhusiano kabisa na kilichoandikwa ndani.Tujifunze uandishi mzuri sio ilimradi tu.
Hii inaonyesha namna kusambaza umeme vijijini inavyopaswa kuwa kipaumbele Cha kupambana na uharibifu wa mazingira. Umeme unachochea Kasi ya maendeleo ya kiuchumi, kielimu, kiafya, kijamii na kimazingira pia. Tuache kutumia hela kwenye sherehe, safari na misamaha ili tumalize kwanza kero za maji, umeme, elimu, na afya ambazo zimewaganda wanyonge kama fulana kwa miaka 60 Sasa hata baada ya Uhuru.
Miaka 60 bro ni mingi sana kwa watu kukosa umeme na maji. Miti mingi sana imepotea kwa kosa hili.

Tumeambiwa Kuna Kodi kwenye mafuta na miamala ya simu ili kumaliza shida hizi kwa Kasi, lakini sioni idadi ya vijiji vinavyopata umeme ikiongezeka kwa kasi, badala yake tunaona Kasi ya safari TU.

Tungesifiwa na kupigiwa makofi mengi sana na dunia nzima kwenye mikutano kama hii kama kiongozi wetu angesimama na kusema Tanzania katika kupambana na uharibifu wa mazingira Tanzania imefanya yafuatayo:

1. Imesambaza umeme vijiji vyote (100%) ili kuepusha miti kukatwa kwaajili ya kupata nishati.
2. Inajenga bwawa la umeme wa kutumia maji (hydro power) huko Rufiji na kusimika mitambo ya kuvfua umeme wa upepo huko singinda.
3. inasambaza maji nchi nzima ili kuepusha watu kuhamahama kutafuta maji ya malisho na majumbani.
4. Nimeshusha bei za umeme na saluji ili kupunguza idadi ya watu wanaojenga nyumba za miti.
5. Nimesambaza gesi yetu itumike majumbani, mashuleni, magerezani na majeshini badala ya kutumia mkaa na Kuni kupikia.

6. Tubabadilisha magari yooote madogo yatumie gesi badala ya mafuta ya diseli na petroli.
7. Tumepiga marufuku matumizi ya vifungaahio vya plastic nchi nzima.
8. Tumeshusha bei ya umeme na gesi ya kupikia ili kuepusha matumizi ya Kuni na mkaa.
9. Tumewapatia pembejeo za kilimo na ufugaji wananchi ili kuepuka kilimo na ufugaji wa kuhamahama.
10. Tumepanda miti hekta kadhaa kurudishia zile zilizoharibiwa na wananchi waliokuwa wakikata Kuni, mkaa, mijengo, kilimo na ufugaji wa kuhamahama.

Hotuba zetu kwenye mikutano zingekuwa kama hivi watu wote wangeduaa na kupiga makofi hadi mikono Yao ipate malengelenge. Lakini unaposema tunapanda miti mingi wakati huohuo wananchi wanakata miti mingi zaidi kuliko uliyopata kwaajili ya kupata mkaa, Kuni, jengo, kilimo na ufugaji wa kuhamahama na mwanga wa kumulikia watu wanakushangaa kwelikweli. Utadhani umeupiga mwingi lakini wanakucheka TU.

Unapanda miti 3 lakini hapohapo wananchi wamekata miti 33 kwa kuni, kuchoma mkaa, kujenga nyumba zao na kutafuta mashamba.
 
luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
4,332
2,000
Ni vigumu kusafiri kwenda mbali kusema habari za mazingira kama wananchi bado wanawasha moto wa Kuni ili TU kupata mwanga wa kumulikia usiku kusoma na kupika jikoni.

Kama Mtu hana njia nyingine ya kupika chakula chake lazima awashe moto wa Kuni au mkaa hayo mazingira yatatunzwa namna gani, tunaenda kufanya nini kwenye mkutano wa mazingira wakati gesi yetu asili hatujaielekeza kwenye kupunguza matumizi ya Kuni, mkaa na petroli kwa watu wetu.

Nani ameturoga?
Mkuu toa takwimu ndio itapendeza zaidi
 
PETER THE ROCK

Senior Member
Feb 17, 2014
163
500
Hii inaonyesha namna kusambaza umeme vijijini inavyopaswa kuwa kipaumbele Cha kupambana na uharibifu wa mazingira. Umeme unachochea Kasi ya maendeleo ya kiuchumi, kielimu, kiafya, kijamii na kimazingira pia. Tuache kutumia hela kwenye sherehe, safari na misamaha ili tumalize kwanza kero za maji, umeme, elimu, na afya ambazo zimewaganda wanyonge kama fulana kwa miaka 60 Sasa hata baada ya Uhuru.

Tumeambiwa Kuna Kodi kwenye mafuta na miamala ya simu ili kumaliza shida hizi kwa Kasi lakini sioni idadi ya vijiji vinavyopata umeme ikiongezeka kwa kasi, badala yake tunaona Kasi ya safari TU.
Swali hapa ni kama kasi ya kupeleka umeme vijijini imepungua? Kwa nini wengi mnapenda kushambulia mada na kuelekeza kwenye siasa za ajabu badala ya kujibu suali kwa data kwamba kasi iko pale pale, imeongezeka au sababu za kasi kupungua!?
 
Ridomil gold

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
1,535
2,000
Swali hapa ni kama kasi ya kupeleka umeme vijijini imepungua? Kwa nini wengi mnapenda kushambulia mada na kuelekeza kwenye siasa za ajabu badala ya kujibu suali kwa data kwamba kasi iko pale pale, imeongezeka au sababu za kasi kupungua!?
Wanamuta eti Mama wanasema Anaupiga mwingi sana
 
gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,072
2,000
Hii inaonyesha namna kusambaza umeme vijijini inavyopaswa kuwa kipaumbele Cha kupambana na uharibifu wa mazingira. Umeme unachochea Kasi ya maendeleo ya kiuchumi, kielimu, kiafya, kijamii na kimazingira pia. Tuache kutumia hela kwenye sherehe, safari na misamaha ili tumalize kwanza kero za maji, umeme, elimu, na afya ambazo zimewaganda wanyonge kama fulana kwa miaka 60 Sasa hata baada ya Uhuru. Miaka 60 bro ni mingi sana kwa watu kukosa umeme na maji. Miti mingi sana imepotea kwa kosa hili.

Tumeambiwa Kuna Kodi kwenye mafuta na miamala ya simu ili kumaliza shida hizi kwa Kasi lakini sioni idadi ya vijiji vinavyopata umeme ikiongezeka kwa kasi, badala yake tunaona Kasi ya safari TU.

Tungesifiwa na kupigiwa makofi mengi sana na dunia nzima kwenye mikutano kama kiongozi wetu atasimama na kusema ili kupambana na uharibifu wa mazingira Tanzania imefanya yafuatayo:

1. Imesamba umeme vijiji vyote (100%) ili kuepusha miti kukatwa kwaajili ya nishati.
2. Inajenga bwawa la umeme wa kutumia maji (hydro power)
3. Nisambaza maji nchi nzima ili kuepusha watu kuhamahama kutafuta maji ya malisho na majumbani.
4. Nimeshusha bei za umeme na saluji ili kupunguza idadi ya watu wanaojenga nyumba za miti.
5. Nimesambaza gesi yetu itumike majumbani, mashuleni, magerezani na makeshini badala ya kutumia mkaa na Kuni kupikia.

5. Tubabadilisha magari yooote madogo yatumie gesi badala ya mafuta ya diseli na petroli.
6. Tumepiga marufuku matumizi ya vifungaahio vya plastic nchi nzima.
7. Tumeshusha bei ya umeme na gesi ya kupikia ili kuepusha matumizi ya Kuni na mkaa.
8. Tumewapatia pembejeo za kilimo na ufugaji wananchi ili kuepuka kilimo na ufugaji wa kuhamahama.
9. Tumepanda miti hekta kadhaa kurudishia zile zilizoharibiwa na wananchi waliokuwa wakikata Kuni, mkaa, mijengo, kilimo na ufugaji wa kuhamahama.

Hotuba zetu kwenye mikutano zingekuwa kama hivi watu wote wangeduaa na kupiga makofi hadi mikono Yao ipate malengelenge. Lakini unaposema tunapanda miti mingi wakati huohuo wananchi wanakata miti mingi zaidi kuliko uliyopata kwaajili ya kupata mkaa, Kuni, jengo, kilimo na ufugaji wa kuhamahama na mwanga wa kumulikia watu wanakushangaa kwelikweli. Utadhani umeupiga mwingi lakini wanakucheka TU.
Heading na content ni mbingu na ardhi jifunze,
halafu unaposema kasi ya usambazaji umeme vijijini imepungua bila data utakuwa ni wendawazimu,
Eleza mfano mwaka jana umeme ulisambazwa vijiji vingapi na mwaka huu vingapi,
Toa data sio tu kwasababu una mb unapost tu!
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
8,128
2,000
Heading na content ni mbingu na ardhi jifunze,
halafu unaposema kasi ya usambazaji umeme vijijini imepungua bila data utakuwa ni wendawazimu,
Eleza mfano mwaka jana umeme ulisambazwa vijiji vingapi na mwaka huu vingapi,
Toa data sio tu kwasababu una mb unapost tu!
Kwani tuliambiwa umeme utafika kila Kijiji ifikapo lini? Wewe ndio ulete takwimu Mimi ninachofahamu ni kata yangu yooooote hakuna kijiji chenye umeme, shule, hospitali na wananchi wote wako gizani. Usifikirie Mimi nitahangaika na takwimu za vijiji vingine. Miaka 60 sina umeme Wala maji.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
11,854
2,000
Nchi lazima iwe na madaraja (classes) ya wanaolala hai na wanaolala hoi.

Kupeleka umeme vijijini ni upotevu wa rasilimali fedha. Tuna mqmbo mengi ya kufanya.

Unapeleka umeme kijijini halafu watu wanabaki kuutizama tu. Hakuna hata mmoja anayechangamkia kuungqnisha nyumbani kwake.
 
Umeupiga mwingi bro
 
thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
7,585
2,000
Ni vigumu kusafiri kwenda mbali kusema habari za mazingira kama wananchi bado wanawasha moto wa Kuni ili TU kupata mwanga wa kumulikia usiku kusoma na kupika jikoni.

Kama Mtu hana njia nyingine ya kupika chakula chake lazima awashe moto wa Kuni au mkaa hayo mazingira yatatunzwa namna gani, tunaenda kufanya nini kwenye mkutano wa mazingira wakati gesi yetu asili hatujaielekeza kwenye kupunguza matumizi ya Kuni, mkaa na petroli kwa watu wetu.

Nani ameturoga?
Kasi imeondoka na hayati Magufuli,muda wa magoigoi huu
 
thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
7,585
2,000
Charity begins at home, unapomulika (mtafuta) nyoka anzia miguuni mwako. Safari moja ya kwenda kwenye mkutano inagharimu nguzo ngapi za kusambaza umeme vijijini ili watu wapunguze kukata misitu?

Kwani pale kwenye mkutano tumekwenda kusema na kufanya kitu gani ambacho hakifahamiki? Nani hajui kuwa Marekani, China, India na Ulaya ndiyo wachafuzi wakubwa wa mazingira? Nani amekwenda kutaja jambo jipya pale?

Sisi tunapaswa kufanya kila kitu kwenye uwezo wetu (play our part) kuhakikisha kuwa umeme unawaka nchi nzima, gesi yetu inatumika majumbani na kwenye magari na mashine, bei ya saruji inashuka bei ili watu waache kujenga kuta za nyumba za miti, bei ya umeme inashuka ili watu wapike kwa kutumia umeme badala ya Kuni na mkaa na kupanda miti.

Sasa tunakwenda kunyooshea wengine kidole kimoja wakati vidole 3 vimeelekea kwetu.
Well said
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom