Kasi ya kuondoa foleni D'Salaam bado ndogo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara inaendelea nchini kwa sasa. Zipo barabara kuu zinazojengwa kwa kiwango cha lami ili kuhakikisha kwamba makao makuu yote ya mikoa ya Tanzania yameunganishwa kwa barabara za lami.

Hizi ni juhudi za kupongeza na kuomba nguvu zaidi zielekezwe kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Kwa mfano, hivi karibuni mradi wa kujenga barabara ya kiwango cha lami ya kuunganisha mkoa wa Dodoma na Iringa ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete na kwa maana hiyo sasa kuufungua mkoa wa Dodoma kwa barabara kuu nne, inayokwenda Arusha, Morogoro, Singida na sasa Iringa.

Hapana shaka hizi ni juhudi njema ambazo zitaifungua Dodoma siyo tu kama katikati ya nchi bali pia kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma.

Agosti 2, 2011 katika safu hii tuliandika tahariri tukisifia juhudi za ujenzi wa barabara kuu kwa kiwango cha lami; tiligusia kuwa kwa miaka mingi tangu uhuru zimefanyika juhudi kubwa za kujenga barabara kwa kiwango cha lami;

mkakati mkubwa kwanza ulikuwa ni kuunganisha miji mikuu yote ya mikoa kwa barabara ya lami; nia ikiwa ni kurahisisha mawasiliano kwa njia ya barabara kutoka mkoa mmoja hadi mwingine.

Tulisema na leo tunarejea kauli yetu kwamba tunatambua kwamba kazi kubwa imefanyika kwani miji mingi ya mikoa sasa imeunganishwa kwa barabara ya lami, lakini pia kumekuwa na juhudi za kufugua kanda zilizokuwa zimeachwa nyuma kwenye mtandao wa barabara za kitaifa kama vile Mtwara, Lindi, Pwani hadi Dar es Salaam; Mbeya, Rukwa, Kigoma na Tabora hadi Kagera kwa kanda ya magharibi.

Juhudi kama hizo zinaendelea kufungua barabara ya lami kutoka Arusha kupitia Babati, Manyara hadi Dodoma; Dodoma, Singida, Tabora, Sinyanga hadi Mwanza ambayo sasa imekamilika.

Tunatambua kuwa kuna barabara nyingi ambazo wakandarasi kwa sasa hivi wako kazini wakizijenga. Tunajua changamoto ni nyingi pia, kwani mikoa kama Singida - Manyara; Dodoma - Manyara; Rukwa - Mbeya na Dodoma - Iringa bado haijaunganishwa kwa barabara za lami, lakini pia tunatambua miradi ya kuunganisha mikoa hiyo kwa lami iko katika ngazi mbalimbali.

Kila tunapotazama kazi kubwa ya ujenzi wa barabara za lami nchini, hasa tunapotazama eneo lote la nchi, tunaelewa kuwa kuna kazi kubwa ya kufanywa na kwa kweli umma unapaswa kuwa nyuma ya juhudi zote za kubadili hali ya barabara zetu kutoka za kupitika kwa msimu mmoja wa mwaka hadi kupitika misimu yote, kiangazi na masika sawia.

Pamoja na kutambua ukweli huu, kuna changamoto nyingine ambazo katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ni mzigo mkubwa kwa uchumi wa nchi. Hali ya barabara katika miji mikubwa ya nchi hii, hususan Dar es Salaam, Mwanza na Arusha ni tatizo kubwa!

Kwa ujumla hali katika miji ya Arusha na Mwanza inaelekea kwa na nafuu kidogo ingawa si nafuu ya kutia moyo sana, huku Dar es Salaam hali ikiwa ni mbaya kuliko inavyoweza kuelezwa. Utafiti uliofanywa juu ya foleni za magari katika jiji la Dar es Salaam umethibitisha kwamba kiasi cha hasara ya Sh.bilioni nne inapatika kila siku kutokana na msongamano huo.

Kama tulivyosema huko nyuma leo tunasema kuwa ni ukweli usiopingika kwamba msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam kwa sasa ni janga la kiuchumi kwa taifa hili; muda mrefu wa kufanya kazi unapotea barabarani watu wakienda kazini; muda mrefu wa shughuli nyingine za kijamii unapotea kwa kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine kwa kutumia muda mrefu kupita kiasi.

Msongamano huu mkubwa mbali ya kuwa mzigo mkubwa kwa uchumi, pia umeleta athari mbalimbali za kiafya na kimazingira kwa kiwango kikubwa mno.

Foleni hizi zinasababisha maradhi kama ya moyo, shinikizo la damu, na saratani za aina mbalimbali kutokana na kiwango kikubwa cha uchafuzi wa mazingira unaochangiwa na moshi mwingi wa magari yanayokaa kwenye foleni kwa muda mrefu kupita kiasi.

Tangu serikali ya awamu ya nne ilipoingia madarakani mwaka 2005 ilitangaza wazi kuwa imedhamiria kukabiliana na msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam, ilisema kuwa kutakuwa na kazi ya kujenga barabara za kupita juu kwa juu; kufufua usafiri wa treni na boti, lakini kubwa zaidi kujenga kwa kiwango cha lami barabara za mzunguko ili kuepusha kila gari kuingia katikati ya jiji kama linataka kwenda upande wa pili wa mji.

Tunafahamu kwamba katika jiji la Dar es Salaam kuna miradi mikuba ya ujinzi na upanuzi wa barabara unaendelea kama vile kuanzia Mwenge kwenda Tegeta kuwa njia nne, Morogoro kwa njia sita ili kutekelezwa kwa mradi wa mabasi yaendayo kasi (Darts), ni juhudi nzuri, lakini bado tunaona hazitoshi kwa hali halisi ya jiji hilo.

Mathalan, ukitazama kinachoendelea kwenye barabara ya Morogoro kwa sasa unapata picha ambayo kwa hakika haionyeshi kama juhudi hizi zitasaidia kuifungua bandari ya Dar es Salaam kama kitovu kwa usafirishaji kwa nchi za maziwa makuu; Rwanda, Burundi, DRC, Malawi na Uganda.

Bado ujenzi wa barabara za kupita juu kwenye makutano za barabara kuu haujaanza wala hauelekei kuwa utaanza miaka ya hivi karibuni. Msongamano wa malori katiba barabara ya Morogoro unaonyesha wazi kuwa kasi ya kuvunja vunja barabara hizi ni kubwa; reli haijafufuliwa ili kuepusha mizigo mikubwa na mzito kupitia barabarani.

Barabara za mzunguko miaka minane sasa tangu ahadi ya serikali ya nne itangazwe bado ni za udongo. Hali ni mbaya. Tunafikiri wakati wa kupoteza hakuna, tuwekeze katika miondombinu ya kuokoa Dar es Salaam kama tunataka kuokoa uchumi wa Tanzania.






CHANZO: NIPASHE

 
Upo sahihi kabisa mkuu,kuna baadhi ya maeneo hapa jijini unaweza kutumia mbka masaa matatu kwa sababu ya foleni,ilihali kusingekuwa na foleni ungeweza kutumia dakika 15 tu!
 
Kwanza nimeona kabisa wajenzi hawazingatii protocally(itifaki) kwa kutambua kuwa hizi barabara zinahitajika ziishe mara moja ili zitumike

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom