Kasi ya JPM yaanza kulipa

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,224
1,676
Magufuli+Photo.jpg

Dar es Salaam. Mtindo wa utawala wa Rais wa awamu ya Tano, Dk John Magufuli wa kudhibiti matumizi ya fedha za umma, kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na kupambana na ufisadi, sasa zimeanza kurudisha majibu, Mwananchi inaweza kukuthibitishia.

Kudhibiti safari za nje, kupambana na wafanyabiashara wanaopitisha makontena bandarini bila ya kulipa kodi, kusimamisha watendaji wa Serikali kwa kutosimamia vizuri mapato, wanaotuhumiwa kwa wizi na matumizi mabaya ya fedha za umma, ni shughuli ambazo Serikali ya Awamu ya Tano imezipa kipaumbele kwa kipindi cha takriban miezi minne sasa.

Shughuli hizo zimekuwa zikionekana kuwa hazimsaidii mwananchi wa chini, lakini hatua za hivi karibuni za kuelekeza fedha zilizokusanywa kwenye miradi mikubwa ambayo baadhi inazalisha ajira na nyingine kuwezesha shughuli za Serikali na za kijamii kuendelea, zinaonyesha umuhimu wa udhibiti wa mali za umma. Kabla ya kuingia madarakani, wizara nyingi zilikuwa hazipati fedha zilizopangiwa kwenye bajeti kutokana na Serikali kukosa uwezo uliotokana na kushindwa kukusanya fedha ipasavyo, misamaha ya kodi, ukwepaji kodi na ubadhirifu, lakini hali sasa imebadilika.

Ubanaji matumizi

Rais alianza kazi kwa kudhibiti safari za nje kwa watumishi wa umma isipokuwa kwa kibali cha Ikulu na kudhibiti semina na mikutano inayofanyika kwenye hoteli za kitalii, na kudhibiti posho zilizokuwa zinalipwa kiholela.

Pia, Rais alipunguza bajeti ya awali ya Sh250 milioni iliyokuwa imetengewa sherehe za kupongeza wabunge walioshinda uchaguzi hadi kufikia Sh15 milioni.

Rais pia aliamua kutokuwa na semina elekezi kwa ajili ya mawaziri ambayo alisema kama ingefanyika, ingetumia Sh2 bilioni.

Mbali na kudhibiti safari za nje isipokuwa kwa kibali cha Ikulu, Rais pia amepiga marufuku semina na mikutano ya Serikali na taasisi zake kufanywa kwenye hoteli za kifahari, huku watumishi wakijilipa posho kiholela.

Shughuli hizo sasa zinafanywa kwenye majengo yanayomilikiwa na Serikali au taasisi zake.

Rais Magufuli alipunguza ujumbe wa Tanzania kwenye kongamano la maendeleo kutoka watu 34 hadi wanne na kuokoa Sh700 milioni ambazo zingetumiwa na ujumbe huo mzito.

Rais Magufuli pia alifuta sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru Desemba 9 kwa ajili ya kuokoa fedha zilizotengwa kwa ajili ya shughuli hizo.

Rais pia aliagiza wafanyabiashara ambao walipitisha makontena 349 bila ya kulipa kodi na kusababisha Serikali kukosa Sh80 bilioni, walipe ndani ya siku saba na taarifa zinasema wengi walijitokeza kufanya hivyo.

Katika kuhakikisha fedha za Serikali zinakusanywa ipasavyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amebaini mbinu iliyokuwa inatumiwa na wajanja kupitisha mafuta kiholela bandarini baada ya kutembelea na kukuta mita inayotumika kupima kiwango cha nishati hiyo ilizimwa kwa takriban miaka mitano.

Mambo sasa yanakwenda

Lakini katika siku za karibuni, Rais ameanza kutekeleza kwa vitendo jinsi ambavyo fedha hizo zinazopatikana zinaelekezwa kwenye shughuli za maendeleo na hasa miradi mikubwa ambayo ina uwezo wa kuajiri idadi kubwa ya watu kama mradi wa Kinyerezi ll, bomba la mafuta kutoka Kampala nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na ujenzi wa barabara ya njia sita.

Pia fedha hizo zimeelekezwa hospitalini, kwenye sekta ya elimu na Idara ya Mahakama.

Akizungumza kwenye mkutano na wazee wa Dar es Salaam, Rais alisema fedha ambazo zilikwamisha kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha umeme cha Kinyerezi ll, Dola 52 bilioni sawa na asilimia 15 ya fedha zilizotakiwa kuchangiwa na Serikali, wameshazilipa na hivyo kituo hicho kitaanza kuzalisha umeme. Magufuli alizindua ujenzi huo juzi.

Siku hiyo, Rais Magufuli pia alitangaza kuwa Serikali iko tayari kulipa fedha ambazo zitatakiwa kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Chalinze hadi Dar es Salaam, ambao utagharimu mamilioni ya fedha.

Juzi wakati akizindua mradi wa Kinyerezi ll, Rais alisema atahakikisha anapata Dola milioni 20 kwa ajili ya upanuzi wa mradi wa Kinyerezi l ili uzalishe umeme zaidi.

Pia alitumia fedha ambazo zilipangwa kwa ajili ya sherehe za kuwapongeza wabunge, kununua magodoro na vitanda 300 kwa ajili ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Alifanya hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini humo na kukuta wagonjwa wanalala chini kutokana na ukosefu wa vitanda na wengine kukosa huduma kutokana na ukosefu wa mashine ya vipimo ya CT Scan.

Pia siku mbili baada ya ziara yake kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alitoa Sh3 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa mashine hiyo ya CT Scan ambayo haikuwa ikifanya kazi kwa muda mrefu.

Katika sekta ya elimu, Serikali imetenga zaidi ya Sh137 bilioni kila mwezi ambazo zinapelekwa kwenye shule za msingi na sekondari kufanikisha mpango wa kutoa elimu bure.

“Hatuhitaji mwanafunzi achangishwe hela ya mitihani. Na zile Sh10,000 kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma sekondari nazo pia tutazipeleka,” alisema Magufuli.

“Na huu ni mpango wa dharura ambao haukuwemo katika bajeti ya mwaka 2015/2016, kwa hiyo tutalazimika kuziombea kibali.”

Hali kadhalika, Serikali yake imetangaza kuboresha utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambako pia amefanya mabadiliko makubwa kutokana na tuhuma za ubadhirifu.

Fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za Uhuru, Rais aliagiza zilimike kwa ujenzi wa Barabara ya Mwenge-Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3.

Katika siku ya Mahakama, Rais aliahidi kuipa idara hiyo Sh12.5 bilioni kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao, fedha ambazo zimeshalipwa.

Akizungumzia mwenedo huo wa Serikali kuanza kuelekeza fedha kwenye miradi na shughuli za kijamii, Profesa Wineaster Anderson, ambaye ni mhadhiri wa Shule ya Biashara wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kitendo cha kubana matumizi na kuweka wazi kiasi kinachopatikana na kisha kuzielekeza katika miradi ya maendeleo ni ni dalili ya kuutunza uchumi kwa watu wengi zaidi.

Alisema wananchi wa kawaida ndio wanaofaidika na miradi hiyo ya maendeleo. Alisema ilivyokuwa inaonekana ni kuwa fedha hizo zinazobanwa na Rais zilikuwa zikiwanufaisha watu wachache na kwamba kitendo cha kuzielekeza kwenye miradi ya maendeleo kitawanufaisha wananchi wengi, jambo alisema linachangia kukuza uchumi wan chi.

Alisema endapo Rais ataelekeza nguvu zake katika kufufua viwanda vilivyokufa, kasi ya uchumi kukua itaongezeka na vijana wengi watapata ajira, huku thamani ya fedha ikipanda.

“Mkiona viwanda vinafufuliwa, wengi watanufaika. Wakulima watauza mazao yao, wafugaji vile vile, tutatengeneza vitu vyetu na kuviuza nje ya nchi ambavyo huku tutakuwa tunaongeza Pato la Taifa sambamba na kupandisha thamani ya shilingi,” alisema.

Mtaalamu wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Humphrey Mushi alisema mwenendo wa utendaji kazi wa Rais Magufuli utawezesha uchumi wa nchi kukua kwa kasi katika kipindi kifupi kijacho.

Alisema awali, ni asilimia 15 pekee ya bajeti ya serikali iliyokuwa ikielekezwa kwenye miradi ya wananchi jambo alilosema lilikwamisha kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi.

Alisema hiyo ina maana kuwa kasi ya kupunguza umasikini itaongezeka, huku maendeleo ya wananchi yakikua kwa kasi kubwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Wewe hauna akili kwa maana kama ungekuwa nazo hata kidogo tu ungetambua ya kwamba huwezi kufufua/kujenga viwanda kama hauna umeme wa uhakika na ndiyo maana Kinyerezei III tayari Ujenzi umeanza na Kinyerezei I pia itajengwa!
Hizo zako we mwenye akili ni story, alivyosema vijana wasicheze pool alikuwa hajui kuwa hajafufua viwanda na vijana hawana ajira? Acha wacheze pool mpaka umeme wa uhakika utakapo patikana basi.
 
Safi sana mheshimiwa Rais. Dhibiti ufisadi na matumizi yasiyo ya lazima. Hata tuwe na viwanda kama nchi tajiri lakini tukiwa na mafisadi makubwa makubwa nchi haiwezi enda popote. Fundisha kwanza watu adabu, ebo
 
Hizo zako we mwenye akili ni story, alivyosema vijana wasicheze pool alikuwa hajui kuwa hajafufua viwanda na vijana hawna ajira? Acha wache pool mpaka umeme wa uhakika utakapo patikana basi.
Mkuu mwasu wewe ni miongoni mwa wale vijana mnaoshinda shinda kwenye pool mnapiga viloba na kupiga stick...nasikia mkuu wa nchi,atawatia bakora mkalime!
 
Roma haiwezi kujengwa kwa siku moja, ila ni kweli kwamba kwa sasa Serikali ya awamu hii inaelekeza mapato yake ya nchi katika miradi inayowagusa wananchi! ila bado kuna tatizo dogo la uelewa kwa baadhi ya wananchi, wanatamani sana kila kitu kitimie siku moja ama siku chache zijazo!
Wananchi tutoeni ushirikiano kwa awamu hii kwani mapato yetu yatatunufaisha wengi kuliko awamu zilizopita!
 
Inatakiwa afufue viwanda sio mipasho na wapinzani, dira inakwama anazunguka mbuyu.
We kiazi kweli hata humitambui kweli unaweza kuanza na viwanda kabla ya kuwa na umeme imara watu wengine hasara kabisa.
 
Mkuu mwasu wewe ni miongoni mwa wale vijana mnaoshinda shinda kwenye pool mnapiga viloba na kupiga stick...nasikia mkuu wa nchi,atawatia bakora mkalime!
Tunalima sana mkuu, lakini hakuna soko la mazao, mwambie apite masokoni aone jinsi matunda yanavyo haribika, watanzania hawana kipato cha kula mboga mboga na matunda mwambieni afufue viwanda ajira zipatikane mazao yasindikwe mengine yote yatajisawazisha yenyewe aache kutumia nguvu panapohitaji busara.
 
We kiazi kweli hata humitambui kweli unaweza kuanza na viwanda kabla ya kuwa na umeme imara watu wengine hasara kabisa.
Alivyosema watu wasicheze pool table alitegemea wakalime lami? Aliahidi ajira hayo mengine ni yaleyale, agawe mashamba aone kama kuna atakae kataa kama ajira imekuwa kikwazo, sio kila mtu ana shamba hapa Tanzania.
 
Magufuli+Photo.jpg

Dar es Salaam. Mtindo wa utawala wa Rais wa awamu ya Tano, Dk John Magufuli wa kudhibiti matumizi ya fedha za umma, kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na kupambana na ufisadi, sasa zimeanza kurudisha majibu, Mwananchi inaweza kukuthibitishia.

Kudhibiti safari za nje, kupambana na wafanyabiashara wanaopitisha makontena bandarini bila ya kulipa kodi, kusimamisha watendaji wa Serikali kwa kutosimamia vizuri mapato, wanaotuhumiwa kwa wizi na matumizi mabaya ya fedha za umma, ni shughuli ambazo Serikali ya Awamu ya Tano imezipa kipaumbele kwa kipindi cha takriban miezi minne sasa.

Shughuli hizo zimekuwa zikionekana kuwa hazimsaidii mwananchi wa chini, lakini hatua za hivi karibuni za kuelekeza fedha zilizokusanywa kwenye miradi mikubwa ambayo baadhi inazalisha ajira na nyingine kuwezesha shughuli za Serikali na za kijamii kuendelea, zinaonyesha umuhimu wa udhibiti wa mali za umma. Kabla ya kuingia madarakani, wizara nyingi zilikuwa hazipati fedha zilizopangiwa kwenye bajeti kutokana na Serikali kukosa uwezo uliotokana na kushindwa kukusanya fedha ipasavyo, misamaha ya kodi, ukwepaji kodi na ubadhirifu, lakini hali sasa imebadilika.

Ubanaji matumizi

Rais alianza kazi kwa kudhibiti safari za nje kwa watumishi wa umma isipokuwa kwa kibali cha Ikulu na kudhibiti semina na mikutano inayofanyika kwenye hoteli za kitalii, na kudhibiti posho zilizokuwa zinalipwa kiholela.

Pia, Rais alipunguza bajeti ya awali ya Sh250 milioni iliyokuwa imetengewa sherehe za kupongeza wabunge walioshinda uchaguzi hadi kufikia Sh15 milioni.

Rais pia aliamua kutokuwa na semina elekezi kwa ajili ya mawaziri ambayo alisema kama ingefanyika, ingetumia Sh2 bilioni.

Mbali na kudhibiti safari za nje isipokuwa kwa kibali cha Ikulu, Rais pia amepiga marufuku semina na mikutano ya Serikali na taasisi zake kufanywa kwenye hoteli za kifahari, huku watumishi wakijilipa posho kiholela.

Shughuli hizo sasa zinafanywa kwenye majengo yanayomilikiwa na Serikali au taasisi zake.

Rais Magufuli alipunguza ujumbe wa Tanzania kwenye kongamano la maendeleo kutoka watu 34 hadi wanne na kuokoa Sh700 milioni ambazo zingetumiwa na ujumbe huo mzito.

Rais Magufuli pia alifuta sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru Desemba 9 kwa ajili ya kuokoa fedha zilizotengwa kwa ajili ya shughuli hizo.

Rais pia aliagiza wafanyabiashara ambao walipitisha makontena 349 bila ya kulipa kodi na kusababisha Serikali kukosa Sh80 bilioni, walipe ndani ya siku saba na taarifa zinasema wengi walijitokeza kufanya hivyo.

Katika kuhakikisha fedha za Serikali zinakusanywa ipasavyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amebaini mbinu iliyokuwa inatumiwa na wajanja kupitisha mafuta kiholela bandarini baada ya kutembelea na kukuta mita inayotumika kupima kiwango cha nishati hiyo ilizimwa kwa takriban miaka mitano.

Mambo sasa yanakwenda

Lakini katika siku za karibuni, Rais ameanza kutekeleza kwa vitendo jinsi ambavyo fedha hizo zinazopatikana zinaelekezwa kwenye shughuli za maendeleo na hasa miradi mikubwa ambayo ina uwezo wa kuajiri idadi kubwa ya watu kama mradi wa Kinyerezi ll, bomba la mafuta kutoka Kampala nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na ujenzi wa barabara ya njia sita.

Pia fedha hizo zimeelekezwa hospitalini, kwenye sekta ya elimu na Idara ya Mahakama.

Akizungumza kwenye mkutano na wazee wa Dar es Salaam, Rais alisema fedha ambazo zilikwamisha kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha umeme cha Kinyerezi ll, Dola 52 bilioni sawa na asilimia 15 ya fedha zilizotakiwa kuchangiwa na Serikali, wameshazilipa na hivyo kituo hicho kitaanza kuzalisha umeme. Magufuli alizindua ujenzi huo juzi.

Siku hiyo, Rais Magufuli pia alitangaza kuwa Serikali iko tayari kulipa fedha ambazo zitatakiwa kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Chalinze hadi Dar es Salaam, ambao utagharimu mamilioni ya fedha.

Juzi wakati akizindua mradi wa Kinyerezi ll, Rais alisema atahakikisha anapata Dola milioni 20 kwa ajili ya upanuzi wa mradi wa Kinyerezi l ili uzalishe umeme zaidi.

Pia alitumia fedha ambazo zilipangwa kwa ajili ya sherehe za kuwapongeza wabunge, kununua magodoro na vitanda 300 kwa ajili ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Alifanya hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini humo na kukuta wagonjwa wanalala chini kutokana na ukosefu wa vitanda na wengine kukosa huduma kutokana na ukosefu wa mashine ya vipimo ya CT Scan.

Pia siku mbili baada ya ziara yake kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alitoa Sh3 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa mashine hiyo ya CT Scan ambayo haikuwa ikifanya kazi kwa muda mrefu.

Katika sekta ya elimu, Serikali imetenga zaidi ya Sh137 bilioni kila mwezi ambazo zinapelekwa kwenye shule za msingi na sekondari kufanikisha mpango wa kutoa elimu bure.

“Hatuhitaji mwanafunzi achangishwe hela ya mitihani. Na zile Sh10,000 kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma sekondari nazo pia tutazipeleka,” alisema Magufuli.

“Na huu ni mpango wa dharura ambao haukuwemo katika bajeti ya mwaka 2015/2016, kwa hiyo tutalazimika kuziombea kibali.”

Hali kadhalika, Serikali yake imetangaza kuboresha utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambako pia amefanya mabadiliko makubwa kutokana na tuhuma za ubadhirifu.

Fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za Uhuru, Rais aliagiza zilimike kwa ujenzi wa Barabara ya Mwenge-Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3.

Katika siku ya Mahakama, Rais aliahidi kuipa idara hiyo Sh12.5 bilioni kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao, fedha ambazo zimeshalipwa.

Akizungumzia mwenedo huo wa Serikali kuanza kuelekeza fedha kwenye miradi na shughuli za kijamii, Profesa Wineaster Anderson, ambaye ni mhadhiri wa Shule ya Biashara wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kitendo cha kubana matumizi na kuweka wazi kiasi kinachopatikana na kisha kuzielekeza katika miradi ya maendeleo ni ni dalili ya kuutunza uchumi kwa watu wengi zaidi.

Alisema wananchi wa kawaida ndio wanaofaidika na miradi hiyo ya maendeleo. Alisema ilivyokuwa inaonekana ni kuwa fedha hizo zinazobanwa na Rais zilikuwa zikiwanufaisha watu wachache na kwamba kitendo cha kuzielekeza kwenye miradi ya maendeleo kitawanufaisha wananchi wengi, jambo alisema linachangia kukuza uchumi wan chi.

Alisema endapo Rais ataelekeza nguvu zake katika kufufua viwanda vilivyokufa, kasi ya uchumi kukua itaongezeka na vijana wengi watapata ajira, huku thamani ya fedha ikipanda.

“Mkiona viwanda vinafufuliwa, wengi watanufaika. Wakulima watauza mazao yao, wafugaji vile vile, tutatengeneza vitu vyetu na kuviuza nje ya nchi ambavyo huku tutakuwa tunaongeza Pato la Taifa sambamba na kupandisha thamani ya shilingi,” alisema.

Mtaalamu wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Humphrey Mushi alisema mwenendo wa utendaji kazi wa Rais Magufuli utawezesha uchumi wa nchi kukua kwa kasi katika kipindi kifupi kijacho.

Alisema awali, ni asilimia 15 pekee ya bajeti ya serikali iliyokuwa ikielekezwa kwenye miradi ya wananchi jambo alilosema lilikwamisha kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi.

Alisema hiyo ina maana kuwa kasi ya kupunguza umasikini itaongezeka, huku maendeleo ya wananchi yakikua kwa kasi kubwa.

Chanzo: Mwananchi
Imelipa nini/vipi?
Usiwe santuri.
 
Viwanda ndo vinafufuliwa ndani ya miezi 5 subiri muda utafika.
Acha akili za mgando, kwahyo mikakati ya kuanzisha hvo viwanda imefikia wap. Au hamna uhakika na plan zenu mnasubiri pesa ndo muanze mipango
STUKA HAMNA CHA VIWANDA WALA MAMA AKE KIWANDA, ILE ULIKUWA KICK YA KAMPENI TU.
Hv mshindwe vitu vidogo kama kudhibiti mfumko wa bei unaotutesa kila sehem, Et ndo mjenge viwanda daah.. Au viwanda vya midoli
 
Kunyamaza nalo ni jibu zuri kwa mpumbavu
 
Dola billion 52 kwa hako kamradi ka kinyerezi!!!!!!hili gazeti la Mwananchi watakuwa wanavuta bangi,Africa nzima hakuna mradi wenye thamani ya hiyo hela.
 
Back
Top Bottom