KASI YA JK:NBC Mwaka wa pili Muungwana hajateua Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
156
Wakuu Heshima Mbele,

Wakati JK anaingia madarakani alikuja na kasi mpya na ari mpya,ila ari na kasi sijui iko katika safari na katika mambo mengine muhimi ya nchi kasi haionekani.katika suala la kufanya uteuzi Mheshimiwa rais amekuwa anachukua muda mrefu,sijajua ni kwasababu gani.

Huu ni mwaka wa pili bado hajateua mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NBC,alishapelekewa majina na jina mojawapo lilikuwa la Dr. Mussa J Assad ambaye mwaka jana alimchagua kuwa Mwenyekiti wa bodi Ya wahasibu na wakaguzi.hii imesababisha ABSA kuteua mwenyekiti wao baada ya kuona Muugwana kakaa kimya,wakamteua Balozi Ami Mpungwe.ila katika hadidu rejea Rais ndiye anatakiwa kuteua Mwenyekiti wa Bodi.sasa sijui ni uzembe wa Mkuu wa kaya au watendaji wake.

Huu ni uzembe mmojawapo.Naomba Mmmkumbushe Mkuu ateua Mwenyeliti wa Bodi ya NBC.na sio kumpangia safari za nje kila siku.
 
Inaonekana kutokana na kusafiri sana nyumba yake hajaijua vizuri,kona zote yeye anajua sebuleni,msalani,ofisini na chumbani tu. Hajui kama kuna varandar,jiko n.k. ndio maana baadhi ya majukumu ameyasahau. sidhani kama anakumbuka presidential duties zote manaake ili uzijue unapaswa kuwa na muda wa kutulia chini na kusoma baadhi ya makabrasha ofisini.
 
Pilot hajatulia tangu aingie ikulu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom