Kashfa zaidi zaibuka Magereza.........................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,039
728,455
Kashfa zaidi zaibuka Magereza
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 4th December 2010 @ 23:55 Imesomwa na watu: 487


KASHFA nyingine imeibuka ndani ya Jeshi la Magereza baada ya uongozi wa juu wa jeshi kudaiwa kukiuka taratibu za ununuzi na uwekaji wa lifti mbili katika jengo la Makao Makuu ya jeshi hilo lililopo makutano ya mitaa ya Sokoine na Shaaban Robert, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Aidha, imefahamika kuwa uongozi huo umeshindwa kumwajibisha mzabuni huyo anayedaiwa kufunga lifti hizo zisizo na ubora wa kutosha kwani moja iliharibika zaidi ya miaka miwili iliyopita, lakini mpaka sasa haijatengenezwa.

Chanzo chetu kimeliambia gazeti hili kwamba uongozi huo kwa makusudi ulimpitisha mzabuni ambaye kampuni yake imekuwa ikifichwa kwa makusudi ili kujipatia fedha kupitia mradi huo ambao ulisababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni 80 kupitia zabuni hiyo.

Katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Kamishna Mkuu wa Magereza, Augustino Nanyaro alisema kwamba ofisi yake ilifuata taratibu za manunuzi kwani mzabuni alipatikana baada kushinda zabuni, lakini alishindwa kumtaja mzabuni huyo kwa maelezo kwamba anayejua zaidi suala hilo ni msimamizi mkuu wa ukarabati wa jengo hilo, Mhandisi, DCP Edward Kaluvya.

Mwandishi alipowasiliana na Kaluvya ili kujua mzabuni ambapo msimamizi huyo wa mradi aliitaja kampuni ambayo baada ya kuwasiliana nayo ilikana kuhusika katika mradi huo.

Awali katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hii, Kaluvya alisema kwamba baada ya taratibu za zabuni kukamilika kampuni ambayo ilishinda na kupewa kazi hiyo ilikuwa ni East African Elevators Company Ltd, na kudai kwamba ndio inayohusika katika
matengenezo ya lifti mojawapo ambayo iliharibika muda mfupi baada ya kufungwa katika jengo hilo.

Mwandishi alifanya mahojiano na uongozi wa kampuni hiyo wenye ofisi zake Mtaa wa Makung’anya, Dar es Salaam ambapo ulikana kuhusika na ununuzi na ufungaji wa
lifti hizo zisizo na viwango vya ubora wa kutosha.

“Nataka nikuhakikishie kwamba, ni kweli tuliwasilisha zabuni yetu kwa ajili ya kuomba kazi hiyo, lakini katika hali ya kushangaza hatukupewa majibu, lakini tulisikia kuwa kampuni fulani ambayo hatuifahamu inafanya kazi hiyo,” alisema ofisa mmoja katika ofisi hiyo na kuongeza: “Hawa wamekueleza uongo, tena afadhali umekuja kutuuliza…

Kama unaweza kawaulize tena labda wanaweza kukwambia ukweli kuhusu jambo hili.

“Ukitaka kujua tunachozungumza nenda kakague lifti hizo nina uhakika hazina kibao chetu kinachoonesha aina ya lifti, kampuni yetu na anwani yetu kwani huo ni utaratibu wetu kwa kila lifti na mitambo mingine tunayofunga katika majengo ambako tumekuwa tukipata zabuni.”

Mwandishi alitembelea katika jengo hilo ili kuhakikisha maelezo hayo na kukuta sehemu ya vitufe vya kuendeshea lifti hiyo vikiwa na jina la OTIS, lakini hapakuwapo na kibao chenye maelezo yaliyotolewa na kampuni hiyo inayouza, kusambaza kukarabati, na kufunga lifti aina ya OTIS.

Ufuatiliaji zaidi katika kupitia vyanzo kadhaa ndani ya makao makuu ya Magereza ulibaini kwamba, baadhi ya makabrasha yalikuwa yakionesha kuwa kampuni hiyo ndio ilishinda zabuni na kupewa kazi hiyo, lakini ukweli halisi kampuni isiyojulikana jina lake ndio ilifanya kazi hiyo.

Gazeti ili kwa mara nyingine liliwasiliana na Kamishna Nanyaro na Kaluvya ili kupata ufafanuzi kwamba licha ya kuongopa kuhusu kampuni iliyohusika katika mradi huo na ni kwa sababu gani wameshindwa kuiwajibisha baada ya lifti moja kuharibika ambapo
ilidaiwa kwamba kazi ya kufuatilia suala hilo si yao, bali inaihusu Ofisi ya Wakala wa Majengo (TBA), kwani ndio ilikuwa Mshauri Mkuu wa mradi huo.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka TBA zinasema kwamba wanayo taarifa kuhusu kuharibika kwa lifti mojawapo katika jengo hilo, lakini wao kama washauri hawana uwezo wa kumwajibisha mzabuni huyo kwani alichaguliwa na Bodi ya Zabuni hivyo kazi yao ni kushauri tu.

Msimamizi wa mradi, Kaluvya alipoulizwa kwanini imechukua muda mrefu lifti hiyo
kufanyiwa matengenezo, alisema kwamba kampuni hiyo ambayo imemkana imeshindwa kupata kifaa kilichoharibika kwa wakati.

Hata hivyo alishindwa kutaja kifaa hicho ambacho hakijapatikana kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Vyanzo vyetu kutoka Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), vimeliambia gazeti hili kwamba ofisi hiyo inakabiliwa na kashfa kadhaa za ukiukwaji wa taratibu wa manunuzi, na
tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa ikiwamo kutuma timu ya wataalamu kukagua taratibu za manunuzi katika maeneo mbalimbali ikiwamo kashfa ya Mradi wa Kusajili Taarifa za Wafungwa (Offenders Management Information System), ambayo iliandikwa na gazeti hili hivi karibuni.
 

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,466
1,164
Hawa habari leo na daily news lazima kutakuwa na mtu au kikundi cha watu huko magereza wanaowatafuta. Pamoja na kusema hivyo sikubaliani na utaratibu wa kufisadi hela za serikali. Lakini aina hii ya uandishi wa habari imekuwa too common in Tanzania. Hili ndiyo linaloleta shaka. Wakati main issue sasa hivi ni DOWANS, habari leo na Dnews ni kama vile hawapo nchini sijaona wakiripoti ishu hiyo hata siku moja.
 

Dick

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
477
8
Wahusika wote wawajibishwe bila kujali lolote. Naona wengine wanachangia kama vile wanamaslahi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom