Kashfa za wagombea zimetosha, sasa tujadili sifa walizonazo

Baba Kiki

JF-Expert Member
May 31, 2012
1,544
940
Ni matarajio ya wengi kama sio wote kuwa Rais ajaye aweza kuwa Edward Ngoyai Lowassa au John Pombe Magufuli.
Kwa muda mwingi tumejadili kuhusu kashfa zao, familia zao, sera zao, vyama vyao n.k. Ni wakati sasa wa kufanya mjumuisho ili tarehe hiyo 25/10/2015 tufanye kile kinachoitwa informed decision. Hadi sasa kuna watu hawajaamua wampe nani kura zao, na hivyo tuwasaidie wafanye maamuzi

Kwa kuzingatia hili hebu naomba tuwapime katika maeneo haya 4, ambayo ni sifa muhimu za Rais au kiongozi tumtakaye katika nchi. Sifa hizi ni muhtasari wa sifa muhimu za kiongozi bora yeyote anazopaswa kuwa nazo, hasa anapokuwa ni ni mwamuzi au sauti ya mwisho. Hili litasaidia wale ambao hawajaamua wamchague nani wafanye uamuzi sahihi.


1. Rais apaswa kuwa mwenye uono mpana na uelewa wa kutosha wa mambo (mfano: nchi, siasa, mahusiano ya kitaifa na kimataifa, uchumi, utamaduni, harakati za kimaendeleo, nk.

2. Rais anapaswa kuwa mwenye dhamira safi na ya kweli sikuzote yaani mkweli, muwazi, tabia njema ambazo zinafaa kuigwa na anaowaongoza.

3. Rais kama kiongozi anapaswa kuamini, kujali na kuheshimu watu. Kuthamini uwezo wa wengine, kujenga moyo wa ushirikiano (teamwork), uwezo wa kuchochea kila mtu kufanya kazi kwa bidii na ku-excel. Anayejua hawezi kujenga nchi peke yake ila ni kwa ushrikiano na kila mtu mwenye dhamira njema.

4. Mwenye uwezo wa kuchukua hatua na ujasiri wa kufanya maamuzi SAHIHI na kwa wakati sahihi.

Ni nani kati ya watajwa hapo juu ana sifa za uongozi zaidi ya mwenzake?
 
Back
Top Bottom