Kashfa za Rushwa zatinga UVCCM, Wagombea wafuatao kukiona cha moto

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,395
Baadhi ya wagombea wa UVCCM Taifa wameendelea kukumbana na mkono wa dola baada ya taarifa zao kufika TAKUKURU wakiwa katika harakati za kutoa rushwa kwa Makatibu wa UVCCM mikoa... baadhi ya wagombea hao ni kama ifuatavyoooo

1. Ayoub Tesha: Mara baada ya usahili uliofanyika Dodoma nusra akamatwe na TAKUKURU akiwa katika mikoa ya Arusha na Singida akigawa fedha kwa wajumbe hususani makatibu wa mikoa... Mratibu wa kundi hili ni moja wa makatibu anayetoka kanda ya Kaskazini (Jina tumehifadhi kwa sasa), na kila mjumbe alipewe laki 4 taslimu. Tarehe 13/07/20017 akiwa katika hoteli ya Royal Hotel mhusika alifanya kikao na makatibu wa mikoa 11 na kila katibu alipewa kiasi cha shillingi laki tano kwa kila moja. Nyuma ya mgombea huyu inasemekana yupo Sadifa (Mkt wa Sasa)..

2. Jackson Kangoye: Huyu ni moja wa wagombea walioanza kugawa pesa za rushwa tokea 2015 akiwa anajipanga kugombea uenyekiti wa UVCCM Taifa. Kangoye amekuwa na shutuma mbalimbali na mwezi wa jana aliitwa TAKUKURU mkoa wa Mwanza kwa mahojiano baada taarifa zake kusambaa kuwa yuko Mwanza hoteli na baadhi ya makatibu akigawa rushwa. Kangowe amezunguka mikoa yote Tanzania bara na Zanzibar akigawa rushwa kwa wajumbe na ilifikia mahali akijigamba hata kamati ya utekelezaji ya UVCCM kaiweka mfukoni. Fedha nyingi amekuwa akitoa kwa mzazi wake ambaye alikuwa ni mtumishi wa TRA na baadaye Mkuu wa Wilaya, mstafu kwa sasa na pia kwa shemeji yake ambaye ni mbunge wa kundi la Vijana.

3. Abdul Van Mohamed: Timu yake inaratibiwa vyema na mke wake ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Pangani. rushwa zake anagawa kupitia kwa baadhi ya MADAS akiwemo DAS wa Iringa mjini Chitinka. Tarehe 2.10.2017 Abdul Van aliwaita Makatibu wa mikoa 17 nyumbani kwake Pangani na kufanya nao kikao ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati. Abdul Van aliwapa rushwa kiasi cha shillingi millioni 1 kwa kila katibu aliyehudhuria. Tarehe 15.10.2017 katika hoteli ya Morena, Dodoma mhusika alifanya kikao na makatibu 8 ambao waliweka mikakati ya kuendelea kufanya kampeni kwa ajili ya uchaguzi ujao. haijajulikana katika kikao hicho ni kiasi gani cha fedha kiligawiwa kama rushwa.

4. James Mwakibinga: Ikisemekana kuwa ni moja wa mgombea wa moja wa mkuu wa mkoa moja wa sasa, Mwakibinga mpaka muda huu uzi unashushwa yupo mkoa wa Ruvuma akiwa katika harakati za kampeni. Mwakibinga amekuwa mgawaji mzuri wa rushwa tokea 2015, na kutokana na fedha ambazo amechangisha kwa wadau mbalimbali ni moja wa wagombea wenye fedha ndani ya UVCCM. Mwezi wa pili alianzisha group la Whattasp lenye jina la "JMK 2017" dhamira likiwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni. jumla ya wanagroup wapo 81.

5. Kheri James: Mpaka muda huu Kheri James ana kesi ya Forgery polisi Mwanza, na TAKUKURU Mwanza. Kheri James anashutumiwa kwa kufoji vyeti vya shule kitendo kilichopelekea kufukuzwa kazi na Rais Magufuli. Ikumbukwe kuwa Kheri James aliteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa DAS ila baada ya kugundulika kuwa hakuwa na vyeti halali Mh. Rais alitengua uteuzi wake. kuwa kwake katibu wa mbunge wa Ilemela na naibu waziri wa Ardhi kwa namna moja au nyingine imeuwa shutuma hizo kuendelea. Pili, Kheri James akiwa na ufahamu wa anachokitenda amedhubutu kufoji cheti cha kuzaliwa na kuonyesha kuwa ana miaka 30 wakati ukweli ni kwamba ana miaka 32.. Amekuwa akisemekana kuwa ndio mgombea anayebebwa kutoka kanda ya ziwa na baadhi ya wabunge na wakuu wa mikoa kutoka kanda hiyo ya ziwa

6. Mathias Kipara: Inasemekana ndio mgombea wa moja wa very powerful Mkuu wa mkoa wa moja la jiji. Mathias amekuwa na shutuma nyingi za kugawa rushwa kupitia kwa marafiki wa huyo mkuu wa mkoa. Mathias ana umri wa miaka 34 ila cha kushangaza katika vikao vya awali vya UVCCM kapendekeza licha ya kutokuwa na sifa za kikanuni hasa linapokuja suala la umri. kanuni za UVCCM zinasema mgombea anapogombea sharti awe na umri usiozidi 30 ili atakapomaliza muda wake awe na umri usiozidi 35...

Itaendelea....
 
Huo ni utamaduni wa ccm kwenye chaguzi zao za ndani, rushwa ni sehemu ya taratibu zao wao wanaita takrima
 
Mtoa post umejitahidi sana kuwafuatilia wagombea unao dai wanatoa Rushwa bahati mbaya hujatuambia wewe binafsi mgombea wako anatoa kiasi gani ! Uvccm ninayoifamu mie inao utaratibu wa kuchuja wagombea kwa kila nafasi lakini pia kuwashughulikia wote wenye mapungufu kama watakuwepo kwa mujibu wa vikao husika wala si humu mitandaoni ! Uvccm ipo imara ikiwa na viongozi mahiri chini ya Shaka Hamdu Shaka ambaye kupitia yeye Uvccm imesimama Imara kuiboresha na kuiimarisha jumuiya, hizo kampeni za kuchafuana mitandaoni hazina tija wala hazitapewa nafasi
Viva Vijana Vivaaaaa
 
Ni lazima nae awe na Mgombea?
Hizo tuhuma alizotoa umezichunguza ukaona kua hazina ukweli bali kuchafuana tu mitandaoni kama unavyodai??
 
Fact. tatizo vijana siku hizi hawataki ukweli. ama ukweli wako usiguse maslahi yao. Hapo unaweza kukuta uozo wa mgombea wake umeanikwa sasa anahaha?..... Anasema sijui Shaka yuko imara and all that..... Sasa Shaka hata akiwa imara ataweza kucontrol rushwa as an individual?...
 
Mtoa post umejitahidi sana kuwafuatilia wagombea unao dai wanatoa Rushwa bahati mbaya hujatuambia wewe binafsi mgombea wako anatoa kiasi gani ! Uvccm ninayoifamu mie inao utaratibu wa kuchuja wagombea kwa kila nafasi lakini pia kuwashughulikia wote wenye mapungufu kama watakuwepo kwa mujibu wa vikao husika wala si humu mitandaoni ! Uvccm ipo imara ikiwa na viongozi mahiri chini ya Shaka Hamdu Shaka ambaye kupitia yeye Uvccm imesimama Imara kuiboresha na kuiimarisha jumuiya, hizo kampeni za kuchafuana mitandaoni hazina tija wala hazitapewa nafasi
Viva Vijana Vivaaaaa
Hakuna positive correlation kati ya uimara wa individual katika taasisi na udhibiti wa rushwa. Achievement will be seen if mfumo wa kucontrol rushwa ikiwa in place... By the way, Shaka mwenyewe muulize zile millioni 70 zilizochotwa CRDB zimeenda wapi?, Muulize 10% ya ununuzi wa magari mawili Prado anayotumia na anayotumia Sadifa alikula ngapi?...

Anyway tusifike huko kwa Shaka. I have just touched some tips za wagombea wa sasa
 
Bila Shaka wewe ni mgombea au mgombea wako kazidiwa maarifa . Acha SIASA za kitoto hizo. Wote uliowataja hao hakuna mwenye uwezo wa kuhonga hata elfu 50, labda Kipara ambaye simjui. James Mwakibinga hata nauli ya kwenda Dodoma kwenye usaili alikuwa anaokoteza. Na huko Ruvuma amenda saa ngapi wakati asubuhi alikuwa DSM?

Tuache tabia ya kutengenezeana kashifa. Wewe ni kada sikutegemea Kama unaweza kuwazushia marafiki zako hivi. Acha Vikao viangalie nani anateuliwa na sisi Kama wajumbe tutaamua. Wewe pambana na Chama huko , UVCCM haikuhusu kwa sasa.
 
Fact. tatizo vijana siku hizi hawataki ukweli. ama ukweli wako usiguse maslahi yao. Hapo unaweza kukuta uozo wa mgombea wake umeanikwa sasa anahaha?..... Anasema sijui Shaka yuko imara and all that..... Sasa Shaka hata akiwa imara ataweza kucontrol rushwa as an individual?...
Nilifikiri angekuja na fact kua Jamaa hakufoji cheti cha Shule au yule mwengine hajazidi umri.
Otherwise aseme kua kigezo cha umri kimefutwa so hata kama amezidi 30 anaruhusiwa ningemuelewa
 
Bila Shaka wewe ni mgombea au mgombea wako kazidiwa maarifa . Acha SIASA za kitoto hizo. Wote uliowataja hao hakuna mwenye uwezo wa kuhonga hata elfu 50, labda Kipara ambaye simjui. James Mwakibinga hata nauli ya kwenda Dodoma kwenye usaili alikuwa anaokoteza. Na huko Ruvuma amenda saa ngapi wakati asubuhi alikuwa DSM?

Tuache tabia ya kutengenezeana kashifa. Wewe ni kada sikutegemea Kama unaweza kuwazushia marafiki zako hivi. Acha Vikao viangalie nani anateuliwa na sisi Kama wajumbe tutaamua. Wewe pambana na Chama huko , UVCCM haikuhusu kwa sasa.
Njoo na fact. Hahahaha eti nauli Mwakibinga alikuwa anaookoteza.... Ebu muulize gari aina ya IST aliyokuja nayo Dodoma imesajiliwa jina la nani?... Sitaki kufika huko. But ikibidi tutafika
 
Akili za CCM ni ngumu sana kuzielewa. Ikitokea mkubwa wao kama wa Arusha kanunua political figures from opposition wanabishaaaa na mapovu juu. Sasa ngoja mtu atoe rusha kwenye vipost vyao utaona wanavyokiri chama kuoza. But mkuu [HASHTAG]#PaganAmum[/HASHTAG] kwa kuwa na wewe ni mgombea nakushauri utoboke mfuko tu ili tuweze kukomesha udouble standard wenu. CHAGUA FUNGU ANALOPENDA KIONGOZI WENU
 
Pagan Amum ,

Mkuu, sasa kama utaendelea kutoa majina mengine mbona basi wagombea wote wa UVCCM ni watoa Rushwa, au mimi ndiyo sijaelewa!??

Mmmmmmmmmmh, kazi ipo Tanzania na siasa zake.
 
Back
Top Bottom