Kashfa za RCO wa mkoani KILIMANJARO

MR. ABLE

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,480
944
MKUU wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Mkoa wa Kilimanjaro, Ramadhan Ng’anzi, ameingia katika kashfa akihusishwa na tuhuma za kuwalinda na kuwakumbatia wafanyabiashara wanaojihusisha na usafirishaji wa sukari kwenda Kenya kwa njia za magendo maarufu kama njia za panya.

Tuhuma hizo zimo kwenye taarifa ya siri ya kurasa tano iliyotumwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro hivi karibuni na wananchi wanaojipambanua kama raia wema na wazalendo wanaokerwa na ufisadi na kumtaja RCO huyo kuwa ndiye kikwazo katika mapambano dhidi ya biashara za magendo mpakani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ambayo Tanzania Daima imefanikiwa kuipata nakala yake pia imewataja Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mwanga na Rombo pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa Kituo cha Polisi Himo kilichoko wilaya ya Moshi.

Pia wamo maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka ofisi kuu ya mamlaka hiyo na wale walio katika Kituo cha Ushuru na Forodha katika mpaka wa Holili ulioko wilayani Rombo ambao wanatuhumiwa kufumbia macho magari ya sukari yanayopita karibu na kituo hicho.

Taarifa hiyo imefichua kuwa wafanyabaishara hao wamekuwa na mahusiano ya karibu na RCO huyo na humpigia simu pindi wanapokamatwa na askari wa ngazi ya chini ambapo inadaiwa amekuwa akiwakaripia askari hao na kuwaamuru waondoke mara moja katika maeneo yanakopita magari hayo.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini wastani wa magari makubwa aina ya Fuso 12 hadi 15 yaliyosheheni sukari yamekuwa yakivuka mpaka na kuingia Kenya huku polisi na TRA wakidaiwa kuwa vinara wa kupokea rushwa na kuyaachia magari hayo yapite machoni mwao.

Njia zinazotumiwa na wasafrishaji hao ambao kwa sasa wamejijengea mtandao mkubwa ndani ya TRA na polisi ni kutoka mji wa Himo kupitia Barabara ya Lower Road hadi yalipo machimbo ya mchanga aina ya pozolana na kuingia Kenya sehemu inayojulikana kwa jina la Kwa Mandara ambapo ni mita chache kutoka kituo cha forodha cha Holili.

Njia nyingine ni kutoka katika mji huo wa Himo kupitia Marangu, Mwika, Mamsera, Ibukoni wilayani Rombo na kuingia katika kijiji cha Munga kilichoko mpakani mwa Tanzania na Kenya ambako magari hayo hupata urahisi wa kuingia Kenya eneo linalofahamika na polisi wa Rombo liitwalo Chumvini.

Kwa wilaya ya Mwanga magari yaliyosheheni sukari ya magendo huanzia safari zake katika eneo maarufu la Njiapanda ya Himo baada ya kupakia sukari mjini Moshi na kuelekea vijiji vya Kileo na Mnoa kabla ya kuingia Kenya eneo maarufu la Madarasani au Kitobo ambako hushusha sukari hiyo na kupakiwa kwenya magari ya Kenya.
 
RPC na RC watakuwa na muamala wao wanapewa ndio maana hawajachukua hatua...
serikali hii hatuna watendaji tuna wababaishaji tu pamoja na waziri mkuu kuchimba bit bado wanamwona mluga mluga tu wanaendelea na magendo kama kawaida.
hii ndio serikali ya ccm zaidi ya uijuavyo.....
 
swala la magendo mkoani KLM lipo kabla ya uhuru na wala haliwez kuisha manake wanaotakiwa kuikemea ndio wanaofaidika nayo.

nakumbuka miaka ile Jiwe ama Asprin wanaweza thibitisha ilikuwa bia zinasafirishwa kwa viroba toka kenya kuja tz na zilikuwa bia za tusker ama plisner nakumbuka, pia mafuta ya taa na mafuta ya kupikia imagine hao polis walifanya ndo mtaji na uzuri enzi zile Mahita alikuwa anajali chake ukimpooza unatoka kimaisha lol!

kimsingi mm biashara ya magendo niliifagilia kwa sababu kuu moja, kama njia za uchumi kwetu hazijafunguka watu wafanye nn?? waache waende kenya walete kappa oil, na kasuku watuuzie wapate hela wasomeshe watoto. sasa hivi ukienda mkuu sekondatri bila malaki ya pesa mtoto hapokelewi, KNCU haifanyi kazi useme utauza mazao huko, mahindi mvua ndo hizo watu wafanyeje?? serikali irasimishe tu hii biashara basi wananchi wafanye biashara hivi wafikiri wananchi wa mipakan wataish vipi??

moshi hakuna ardhi ya kulima kote ni nyumba, kilimo chenyewe cha mvua, ufugaji hakuna mahali pa kulishia mfugo viwanda hakuna watu wafanyeje??
 
Last edited by a moderator:

moshi hakuna ardhi ya kulima kote ni nyumba, kilimo chenyewe cha mvua, ufugaji hakuna mahali pa kulishia mfugo viwanda hakuna watu wafanyeje??[/QUOTE]

"thought takes man out of servitude into freedom"....naona hata jinsi biashara inavyoenda mambo yanabadilika...doing that thing is not sustainable. Tuanze kutengeneza entrepreneurs waweze kuenda sambamba na uchumi wetu wa sasa unavyokwenda. Magendo mhhhh! Don't get me wrong...I like that place called Moshi
 
Ndahani tatizo sio wananchi kwenye biashara ya magendo bali ni serikali. wananchi wanaoish mpakani wanapata tabu sana, hawawekewi njia nzuri za wao kufanya biashara wakati wanataka pesa sasa wafanyeje?? serikali ingekuwa makin ingejiuliza inapoteza sh ngapi kwa biashara za magendo kisha itengeneze njia ambayo mfanyabiashara ataifanya iwe na tija kwa taifa sasa wao wanakuwa loose na wapenda rushwa tutegemee nini??

binafsi hata mm ikiwezekana na kama inalipa ni bora kuleta sukari toka kenya kuja kuuza tz nipate pesa kuliko kubaki nalia kila siku sina hela swala la nchi inafaidika nini litajibiwa kwenye leseni ya biashara dukan kwangu na kwenye kodi ya mapato.
 
Last edited by a moderator:
swala la magendo mkoani KLM lipo kabla ya uhuru na wala haliwez kuisha manake wanaotakiwa kuikemea ndio wanaofaidika nayo.

nakumbuka miaka ile Jiwe ama Asprin wanaweza thibitisha ilikuwa bia zinasafirishwa kwa viroba toka kenya kuja tz na zilikuwa bia za tusker ama plisner nakumbuka, pia mafuta ya taa na mafuta ya kupikia imagine hao polis walifanya ndo mtaji na uzuri enzi zile Mahita alikuwa anajali chake ukimpooza unatoka kimaisha lol!

kimsingi mm biashara ya magendo niliifagilia kwa sababu kuu moja, kama njia za uchumi kwetu hazijafunguka watu wafanye nn?? waache waende kenya walete kappa oil, na kasuku watuuzie wapate hela wasomeshe watoto. sasa hivi ukienda mkuu sekondatri bila malaki ya pesa mtoto hapokelewi, KNCU haifanyi kazi useme utauza mazao huko, mahindi mvua ndo hizo watu wafanyeje?? serikali irasimishe tu hii biashara basi wananchi wafanye biashara hivi wafikiri wananchi wa mipakan wataish vipi??

moshi hakuna ardhi ya kulima kote ni nyumba, kilimo chenyewe cha mvua, ufugaji hakuna mahali pa kulishia mfugo viwanda hakuna watu wafanyeje??
Umenikumbusha mjombangu alikuwa dereva wa treni enzi hizo. Basi kwenye kichwa cha treni tulikuwa tunajaza mikreti ya Pilsner kama hatuna akili timamu. Tukiishusha Dar, wanywaji wa Temeke walikuwa wanapiga foleni kwenye grosare yake bubu. Bia zilikuwa hazikatiki pale. RIP Uncle
 
hii story imejaa majungu. nashauri serikali iangalie kama kuna uhitaji mkubwa wa sukari ya Tanzania nchini Kenya basi wavishawishi viwanda vyetu viongeze uzalishaji na wafanyabiashara wapeleke sukari kwa wingi kiwanda kiajiri wafanyakazi zaidi, wafanyabiashara waneemeke na taifa lipate kodi na majungu yaishe. tuna nini? watanzania sukari toka malawi ikiingia nchini inakamatwa, sukari yetu ikiingia kenya inasindikizwa tubadilike.majungu si mtaji kalamu zenu zitoe ufumbuzi.
 
Unajua hata mimi nashangaa kwanini hili halifanyiki? Au labda sababu ni kwamba sukari inayozalishwa haitoshelezi hata kwa watanzania wenyewe?
 
mkuu siyo huko tu, hata karagwe , kahawa yetu inasoko zuri tu, nchini uganda ambao nao bila shaka wanasafirisha nje ya nchi , lkn mkulima anavyosumbuliwa kuipeleka huko huwezi amini,sasa waandishi badala ya kuendekeza majungu ni vyema wakatumia kalamu zao , kushauri na kutoa ufumbuzi, kwanini? tung'ang'ane kupeleka sukari/kahawa Uingereza wakati Uganda/kenya wanazihitaji bidhaa hizo basi uwekwe utaratibu wa malipo ya USD kama tatizo ndo hilo.mkuuu amini usiamini viwanda vyetu vinauwezo mkubwa wa kuzalisha sukari nyingi ya kutosheleza nchini na kuuza kenya hii hali ya kuzalisha / kutoa stock kidogo ili soko liendelee kuwa na uhitaji na sukari ya nje iweze kuingizwa nchini na sukari hiyo inaagizwa na hao hao wamiliki wa viwanda vya sukari kwakuwa kwa kuagiza faida ni kubwa mno.
 
Back
Top Bottom