nyakahanga
JF-Expert Member
- Mar 7, 2013
- 240
- 65
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe, Joseph Mkirikiti, alisema baada ya halmashauri hiyo kufanya uhakiki wa watumishi hewa kuanzia Machi 19 hadi Machi 25, mwaka huu, walibaini madudu hayo.
Mkirikiti alisema watumishi ‘hewa’ hao walikuwa wakilipwa mishahara kupitia akaunti zao, lakini hatua zimechukuliwa za kuzuia akaunti hizo na kuokolewa kiasi hicho cha fedha.
Alisema kutokana na hali hiyo, Katibu wa Idara ya Utumishi wa Walimu, Hamis Machele na Sweet Sudi, ambaye ni wa idara ya utawala wa rasilimali watu, ameagiza wakamatwe kwa kujihusisha kutenda makosa ya jinai na kinidhamu.
“Naagiza watumishi hawa wakamatwe mara moja kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wakiwa wamesimamishwa,” alisema Mikirikiti.
Aidha, alisema katika uhakiki wa watumishi hewa, 36 walibainika ni watoro, wastaafu walikuwa saba na marehemu wawili.
Credit to: NIPASHE