Kashfa ya Vigogo Serikalini kujimilikisha hifadhi yenye madini Handeni

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Jumla ya hekta 749.5 za msitu wa taifa wa Magambazi uliopo katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga eneo lenye utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu linadaiwa kuuzwa kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo. Hifadhi hiyo ilitangazwa katika Gazeti la Serikali mwaka 1912 kabla ya uhuru na taarifa zake kuhifadhiwa katika Jalada Namba 658 Wizara ya Maliasili na Utalii. Kashfa hii imekuja siku chache baada ya NIPASHE kuripoti kuwa baadhi ya vigogo wa Idara ya Maliasili walishiriki pia kuvusha wanyama pori Hai bila ya kulipa kodi na kusababisha serikali kupata hasara zaidi ya Sh. milioni 170 katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA). Hata hivyo, kesi hiyo iko mahakamani Moshi. NIPASHE iliyotembelea eneo hilo, imeshuhudia mitambo mikubwa ya uchimbaji dhababu na usafishaji dhababu ikiwa inafanya kazi usiku na mchana kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Wanaodaiwa kumiliki eneo hilo la hifadhi ni vigogo wa serikali na viongozi wa Idara ya Maliasili na Utalii. Na walipoulizwa na NIPASHE baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Handeni kwamba kwanini hawachukui hatua, kwa nyakati tofauti walijibu kuwa `waulizwe wakubwa' wao. Baadhi ya viongozi walioulizwa kuhusiana na suala hilo ni Kamanda wa Kikosi Maalum cha Maliasili Kanda ya Kaskazini, Halifa Munisi, Afisa Maliasili Wilaya hiyo, Hilbert Temu, Mhifadhi Misitu Asili wilaya hiyo, Anatory Masaka, Afisa Maliasili mkoa wa Tanga, Jonas Mialla na Mkuu wa wilaya hiyo, Seif Mpembenwe.

Hata hivyo, walisema wanayo dhamana ya kusimamia misitu na hifadhi za Taifa lakini Hifadhi ya Magambazi, walimtupia lawama Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Dk. Felician Kilahama na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige. “Naomba suala la Magambazi usiniulize…naelekea kustaafu," alisema kwa kifupi Mkuu wa Wilaya, Mpembenwe. Kwa upande wake, Munisi alisema si msemaji na Mialla alidai wakubwa wake wanajua suala hilo na kutaka tuachane nalo huku Temu akisema ameshaandika barua nyingi hazijibiwi. NIPASHE ilimtafuta Waziri Maige ofisini kwake bila mafanikio lakini alipohojiwa Dk. Felician Kilahama alisema alipata taarifa za uharibifu huo. Hata hivyo, alisema ametuma watu kutoka wizarani waje kupima eneo lililoharibiwa kufahamu mipaka yake.

Habari kutoka kwa baadhi ya wachimbaji hao wa dhahabu zilidai kuwa viongozi hao wa maliasili wamepewa kazi ya kutokuwakamata wachimbaji hao na mitambo yao ikiwemo kudhoofisha juhudi za Mkurugenzi wa Maliasili na Nyuki. Dk. Kilahama, ili asichukue hatua haraka kwa kumuogopesha kuwa wanaochimba hapo ni vigogo wa serikali. Viongozi hao wamepewa utetezi kuwa endapo itatokea wakahojiwa waseme hawajui mipaka ya hifadhi hiyo jambo ambalo limepingwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana, kuwa utetezi huo ni dhaifu kwani hata anayekata mti nje ya hifadhi bila ya leseni, ana hatia.

Maligana alisema hata yeye anashangaa kuletewa wakulima kila siku na maliasili wakidaiwa wamekata miti bila ya leseni huku makatapila yakiwa ndani ya hifadhi ya Taifa yakiangusha miti. Alisema hali hiyo imejenga chuki baina ya mahakama na wananchi Handeni wakiwatuhumu mahakimu kuwa wanahusika. "Sheria za maliasili ziko wazi. Ukikutwa ndani ya hifadhi au ukiwa na kesi ya maliasili, wewe mshtakiwa ndio wa kutoa ushahidi kuwa hukuhusika…yale magreda wakiyaleta hapa na wahalifu wao ndiyo wathibitishe kuwa ile sio hifadhi ni mashamba yao,”alisema.

Uchunguzi wa NIPASHE ambao pia umethibitishwa na Afisa Madini Mkazi Mfawidhi wa kanda hiyo, Philip Ngeleja, kampuni iliyopewa leseni ambayo iko kisheria ndani ya hifadhi hiyo kwa utafiti ni ya Midlands Minerals Tanzania Ltd Novemba 7, mwaka 2007 ambapo leseni hiyo inaishia Novemba 22, mwaka huu. Hata hivyo, wachimbaji wengine wako kinyume cha sheria.
 
MMh Mmh haya hiki kizazi cha huu utawala ni mchwa wakimaliza dhahabu na almasi,mafuta na gesi wataanza kututafuna sisi,inauma sana kuona wale waliopewa dhamana wanajinufaisha wenyewe utafikiri serikali imegeuka NGO duh hatari sana
 
Hakuna rais mbaya ambaye atatokea kuwa mhuni,mnafiki,mwizi na kigeugeu kama Kikwete...namchukia zaidi ya shetani mkuu aliyemuasi Mungu,Kikwete ametumwa kuiua Tanzania na vizazi vyake,alaaniwe JK.
 
nchi ya kitu kidogooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Ukitaka leseni ya kuchimba madini piga watu offfa za Suti kutoka wool worth
 
Hakuna rais mbaya ambaye atatokea kuwa mhuni,mnafiki,mwizi na kigeugeu kama Kikwete...namchukia zaidi ya shetani mkuu aliyemuasi Mungu,Kikwete ametumwa kuiua Tanzania na vizazi vyake,alaaniwe JK.

Kabisa ndugu yangu.ila naamini siku moja tutawawajibisha.yuko wapi gadafi?tailor?kitajulikana tu.
 
bora wamiliki hao watanzania kuliko barick na GGM... au dowans, wezi watupu

Mpare akiwekeza basi atajenga kwetu na ndugu zake watapaka kazi hata ya kuosha vyombo...
 
Hakuna rais mbaya ambaye atatokea kuwa mhuni,mnafiki,mwizi na kigeugeu kama Kikwete...namchukia zaidi ya shetani mkuu aliyemuasi Mungu,Kikwete ametumwa kuiua Tanzania na vizazi vyake,alaaniwe JK.

Uvumilivu una kikomo chake, na iposiku tutajutia ubinafsi wa viongozi wetu kwani yatakayojilia wote tutaathirika. Kwa haya sasa ni dhahiri sikio la kufa halisikii dawa, na wanachoendelea kuimba wanasiasa wa upinzani kinazidi kuingia akilini mwa watanzania wengi sasa maana jitihada hizi za kupotosha ukweli kwa malengo ya kujaza matumbo ya wachache inazidi kutufanya serikali ya sasa tuikinai.
 
Back
Top Bottom