Kashfa ya Stanbic: Serikali inaweza kutuambia ni kwanini waliotajwa na SFO hawajakamatwa?

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,862
Mi sipendi tabia za watanzania kusifia sifia tu kwamba mtu anatumbua majipu kumbe anahangaika na vipere tu! Hivi leo hii serikali inaweza kutoa jibu gani kwa nini watu waliotajwa kwenye kashfa ya stanbic ya ule mkopo dola mil 600 hawajakamatwa achia mbali kuhojiwa?

SFO walifanya kila kitu na kututajia waliohusika katika wizi huo akiwemo Godfrey Mgimwa na Mustafa Mkulo, lakini serikali iko kimya lakini sisi tunaendelea na nyimbo za sifa tu. Serikali hii ina tofauti gani na zile zilizopita ambazo SFO ilipowataja akina Chenge hawakuguswa bali wakaishia kusimanga watanzania kwamba bilioni moja ni vijisenti?

Na haya tumeyaona ktk kukamata walioruhusu makontena kupita bila kulipa kodi lakini wenye makontena wakaambiwa walipe yaishe! (Ina tofauti gani na EPA?) Wale ambao walipewa siku 7 wawe wamelipa zimepita siku ngapi mpaka sasa?
 
Last edited by a moderator:
Hakuna mwanasiasa yeyote atakayekamatwa.

Ndio maana unamuona Chenge, Tibaijuka, Ngeleja wakipeta na sakata lao la Escrow.

Ndio maana unamuona aliyebeba mabilioni ya pesa za Escrow kwenye Lumbesa, mabegi, sandarusi na mifuko ya rambo, (Mnamjua) kinyume na sheria, kanuni na taratibu za kibenki, akiendelea kuzunguka dunia nzima bila kukamatwa.

Ndio maana unamuona Waziri wa Fedha na Waziri wa Uchukuzi awamu ya nne na manaibu wao wakiendelea kupeta na Sakata la makontena.

Usitegemee Mwanasiasa yeyote kukamatwa.

Kwa kifupi hawezi kuwashughulikia wana ccm waliompa Urais

Labda aone aibu baada ya thread hii.
 
Hawajiamini kabisa ndio maana wanawazuia wapinzani kufanya mikutano nguvu ya soda tuwape miezi mitano mtaniambia
 
Magufuli ilikuwa "gear' ya kuiponya ccm. Wengi walinijua kuwa mpizani na aliyeichukia ccm. Uzuri wamekili kwa vinywa vyao kuwa wameoza kwa majipu....sasa wanatumbuana.. .Swali moja naulizwa mitaani..."sasa umemkubali magufuli"? Jibu ni "No"...nasubili miaka 2 nitatoa jibu sahihi....Ila ninamwombea....
 
Hakuna mwanasiasa yeyote atakayekamatwa.

Ndio maana unamuona Chenge, Tibaijuka, Ngeleja wakipeta na sakata lao la Escrow.

Ndio maana unamuona aliyebeba pesa za Escrow kwenye Lumbesa, mabegi, sandarusi na Rambo (Mnamjua) akiendelea kuzunguka dunia nzima bila kukamatwa.

Ndio maana unamuona Waziri wa Fedha na Waziri wa Uchukuzi awamu ya nne na manaibu wao wakiendelea kupeta na Sakata la makontena.

Usitegemee Mwanasiasa yeyote kukamatwa.

Kwa kifupi hawezi kuwashughulikia wana ccm waliompa Urais

Labda aone aibu baada ya thread hii.

Issue ya Escrow ni bomu, tunasubiri bunge liwabane watekeleze maazimio ya bunge.
 
Mi sipendi tabia za watanzania kusifia sifia tu kwamba mtu anatumbua majipu kumbe anahangaika na vipere tu! Hivi leo hii serikali inaweza kutoa jibu gani kwa nini watu waliotajwa kwenye kashfa ya Stambic ya ule mkopo dola mil 600 hawajakamatwa achia mbali kuhojiwa?

SFO walifanya kila kitu na kututajia waliohusika katika wizi huo, lakini serikali iko kimya lakini sisi tunaendelea na nyimbo za sifa tu. Serikali hii ina tofauti gani na zile zilizopita ambazo SFO ilipowataja akina Chenge hawakuguswa bali wakaishia kusimanga watanzania kwamba bilioni moja ni vijisenti?

Na haya tumeyaona ktk kukamata walioruhusu makontena kupita bila kulipa kodi lakini wenye makontena wakaambiwa walipe yaishe! (Ina tofauti gani na EPA?) Wale ambao walipewa siku 7 wawe wamelipa zimepita siku ngapi mpaka sasa?

ww subiri utasikia wamepelekwa mahakamani masuala ya kuhojiwa sio kazi yako
 
We Ulitaka Ndani Ya Mwezi Mmoja Magufuli Awe Amefanya Kila Kitu, Mpe Mda Atatenda

Siyo kweli ndg, na ninyi mnaosifia mtakuja kulia nawaambia. Magufuli aliposema majipu nilamini ni majipu kweli kumbe majipu ni watumishi na siyo wanasiasa mabosi wao?
 
Mi sipendi tabia za watanzania kusifia sifia tu kwamba mtu anatumbua majipu kumbe anahangaika na vipere tu! Hivi leo hii serikali inaweza kutoa jibu gani kwa nini watu waliotajwa kwenye kashfa ya Stambic ya ule mkopo dola mil 600 hawajakamatwa achia mbali kuhojiwa?

SFO walifanya kila kitu na kututajia waliohusika katika wizi huo, lakini serikali iko kimya lakini sisi tunaendelea na nyimbo za sifa tu. Serikali hii ina tofauti gani na zile zilizopita ambazo SFO ilipowataja akina Chenge hawakuguswa bali wakaishia kusimanga watanzania kwamba bilioni moja ni vijisenti?

Na haya tumeyaona ktk kukamata walioruhusu makontena kupita bila kulipa kodi lakini wenye makontena wakaambiwa walipe yaishe! (Ina tofauti gani na EPA?) Wale ambao walipewa siku 7 wawe wamelipa zimepita siku ngapi mpaka sasa?
sema tu unakerwa na mafanikio na sifa aliyopa magufuli kwa muda mfupi. vigogo haswaaa ndio wanaotumbuliwa siku hizi za magufuli. tra bandari etc.
 
Issue ya Escrow ni bomu, tunasubiri bunge liwabane watekeleze maazimio ya bunge.

Mkuu tusitegemee jipya kutoka kwenye Bunge lililojaa majipu ya ccm.

Hivi unadhani Dungai ana uwezo wa kumshughulia Chenge, mthuhumiwa wa escrow, ambaye bila aibu alipitishwa na CCM kugombea Ubunge kisha kupewa Uenyekiti wa Bunge siku ile Dungai anapigiwa kura awe Spika!!!????

In these kind of things CCM will remain the same ever, na tusitegemee anything new under ccm regime.
 
Back
Top Bottom