Kashfa ya SAKATEL vs TTCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya SAKATEL vs TTCL

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaa la Moto, Oct 7, 2008.

?

NINI Kifanyike kwa mambo kama haya ili YAISHE?

 1. WACHAGULIWE VIONGOZI WENYE PESA ILI WASIIBE?

  1.7%
 2. WANAOFANYA WIZI WARUDISHE HARAKA?

  8.5%
 3. TAIFISHA MALI NA WAFUNGWE?

  88.1%
 4. WABADILISHWE TU?

  1.7%
 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Jamani katika kupita pita kwangu nimekutana na hii hapa. Wala si mimi muandishi lakini inajieleza wazi. Nikajiuliza hivi kweli makampuni haya ya serikali turuhusu yafe????? Na je yakifa hapo ndiyo tuyaache yale ya mafisadi yachanje mbuga?

   
 2. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi, inakuaje kampuni ZOTE za umma Tanzania zinachukuliwa na foreign investors matapeli? There is something VERY wrong here. Jamani, mnakumbuka ile thread ya "Nigeria's brain gain"? Mnaonaje vijana waTZ tuanze kurudi home? Hela ndogo tu ya huku unaweza fanyia makubwa back home.
  Ni maoni tu.
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  JESUS! inawezekana, TTCL waliingia mkataba na kampuni ya kichina iitwayo huwaei technologies, wajengewe minara ya mawasialiano, wale wachina waliniambia kuwa TTCL hawataki kutekeleza ule mkataba, bali wamezuiwa na wakubwa fulani, nikijumlisha hii habari hapo juu na hili la wachina napata jawabu

  kuna watu itabidi wanyongwe ili haki itendeke, wanaotajwa hapo juu ni chenge wakati huo mwansheria mkuu, mwandosya, na mramba
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Recalling:

  May 23rd, 2007
  Sasktel takes over at TTCL

  Published 10/22/2006
  PSRC yajiosha mikono kuhusu Saskatel International

  Published on 14/02/2007

  Chenge remains mum over privatisation of TTCL

  and so much more...

  And here comes:

  TTCL vs SaskaTel Case Study
  [​IMG]
   

  Attached Files:

 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  invisible printer yangu imekwish a wino mzee

  yaani unajua unavyozitoa on daily basis nashindwa hata kunyambua which is which

  duh!
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Well, if that's the case... Nitaacha for three months... Najipa likizo mkuu!
   
 7. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Inv.

  Naona ndio ukubwa huo likizo unajichotea tu! LOL

  Shukrani sana kwa hii Mkuu!
   
 8. UramboTabora

  UramboTabora Member

  #8
  Oct 24, 2008
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani pia angalieni jinsi CCM wanavyofanya uchafu ndani ya TTCL licha ya ule uchafu wa Richard wa Monduli katika Tanesco. Chadema kwa udhaifu huu wa CCM hakika mtashinda. jipeni moyo pia mtafute point kwa wadau

  Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,

  Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Salaam,


  Mheshimiwa,

  Kwa heshima kubwa napenda kukutarifu kuwa hali ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ni mbaya sana baada ya waendeshaji SAKATEL kutoka nchini CANADA waliopewa kuiongoza Kampuni yetu kuamua kwa makusudi kabisa kuihujumu KAMPUNI hii.

  Mheshimiwa,

  Historia ya kuifisidi TTCL ilianza mwaka 1999 baada ya Serikali ya awamu ya tatu kuanza mchakato wa kuuza 35% ya TTCL kwa wawekezaji wa nje. Katika mchakato huo Serikali iliingizwa mkenge na Watanzania wenzetu walioamua kwa makusudi kujinufaisha kupitia nyadhifa zao. Wahusika wakuu katika mchezo huo walikuwa ni Waziri wa Mipango na Uchumi, Waziri wa Fedha, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi na Mwanasheri Mkuu wa Serikali.


  Katika kutimiza azima yao hiyo, Waheshimiwa hao waliingia Mkataba na MSI na DETACON wa kununua 35% share za TTCL. Wawekezaji hao ambao mwanzo ilidaiwa kuwa wanatoka UHOLANZI, kumbe haikuwa kweli bali ni Wajanja wa Tanzania wakishirikiana na Mfanyabiashara mmoja huko SUDAN alikuja kutambulika baadae kuwa MOHAMED SAID IBRAHIM (MSI) ndio waliohusika na mchezo huo mchafu.


  Baada ya kukamilisha ujanja huo, wawekezaji DETACON wakaondoka kinyemela na kuiacha TTCL kuongozwa na MSI feki.Muda mfupi baadae HESABU za TTCL zikaanza kuhujumiwa na kutoa taarifa za upotoshaji kwamba KAMPUNI ina hasara na hivyo MSI haiwezi kununua hisa hizo kwa bei waliokubaliana na Seikali ya 120 Million US DOLLARS. Badala yake wakatengengeneza Dili na Mawaziri hao tuliowataja hapo nyuma na wakafanikiwa kuishawishi Serikali ya awamu ya tatu kukubali kuuza 35% kwa bei ya US DOLLARA 60 Million. Baada ya hapo ikapokelewa taarifa kuwa mtoto wa Waziri wa Mawasiliano wakati huo alipelekwa kusoma UINGEREZA na hao MSI feki.

  Mheshimiwa Raisi kuanzia hapo TTCL ikawa inaliwa shs 600 Million kila mwezi na jamaa hao wa MSI feki.Piga mahesabu mwenyewe Mheshimiwa Rais, Fedha hizo zimeliwa kwa miaka 4 na hatimae ikaimarishwa CELLTEL.

  Baada ya kukamilika CELLTEL, bwana MOHAMED SAID IBRAHIM akauza Kampuni yake kwa mfanyabiashara mwenzie kwa KUWAIT na kupelekea kubadilshwa jina na kuitwa Celtel International na sasa ZAIN.Hapo serikali machale yakawacheza na kuamua kuzitenganisha Kampuni hizo mbili CELLTEL na TTCL.

  Mheshimiwa Raisi, ulipoingia madarakani, Serikali yako ikatafuta mwendeshaji mwingione wa kuongoza TTCL kutokana na makubaliano yenu na CELTEL INTERNATIONAL.Katika mchakato huo ikapatikana SASKATEL kutoka CANADA.

  Serikali yako iilifikiri imetatua tatizo la TTCL kumbe hao mawaziri waliotajwa hapo juu ndio walioshiriki tena katika mchezo mchafu na kupatikana SASKATEL feki kama ilivyokuwa MSI fake.

  Mheshimiwa Raisi, wanachokifanya SAKATEL hivi sasa ni kuihujumu TTCL kwa lengo la kuijenga Kampuni mpya ya HITS mabayo wenyewe ni hao mawaziri waliohusika kuiteketeza TTCL hulo nyuma.

  Hujuma za moja kwa moja zinazofanywa na SASKATEL kwa maelekezo ya Mawaziri hao ni kuhakikisha TTCL haiendi mbele kwa kufanya yafuatayo:

  1.Wamesimamisha Matangazo yote ya Biashara ya TTCL.

  2.Wamesimamisha Miradi yote ya TTCL.

  3.Wamesimamisha kutafuta Wateja wapya (Marketing) kwa TTCL

  4.Wamesimamisha ununuzi wa spare za mitambo ya TTCL

  5.Wameamua kubana matumizi kwa asilimia 30 ya mapato ya TTCL.

  6.Business Plan ya TTCL iliyotengenezwa na Wazalendo imepelekwa kampuni ya HITS.

  7.Wametengeneza Salary Structure ya kuwa-frustrate Mafundi wa simu TTCL ili waache kazi au wagome.

  Katika Structure hiyo, Wafanyakazi wa Idara ya Biashara wenye Elimu ya Darasa la saba na kumi nambili wanalipwa mshahara wa shs 1,100, 000.

  Wafanyakazi Mafundi wenye Elimu ya Form VI, FTC na Diploma wanalipwa shs 600,000.

  8.Chief wa Mauzo na Masoko Mama Lorein, anaendesha mkakati wa kuwarubuni Wataalamu wote wazuri wa TTCL waende Kampuni ya HITS.

  9.Huu mwezi wa pili hawajapeleka michango ya Wafanyakazi katika mifuko ya Hifadhi ya jamii NSSF na PPF

  10.Huu mwezi wa pili hawajapeleka fedha za michango ya SACOS za Wafanyakazi wa TTCL katika chama chao cha Kuweka na Kukopa


  Mheshimiwa Raisi, jamaa hawa mpaka sasa wameendesha mradi wa kudai madeni ya TTCL yanayofikia shs 65 Billion.Wameshakusanya 15 BILLION LAKINI HAZIONEKANI NDANI YA ACCOUNT ZA TTCL.

  Katika kubana matumizi wameserve 3 Billion kila mwezi kuanzia October 2007 hadi sasa lakini nazo hazimo kwenye account za TTCL.

  Wameleta wataalamu ambao wanalipwa 800 kila mwezi kwa kazi ambazo zinazweza kufanywa na Wazalendo.

  MHESHIMWA RAISI TUNALETA KWAKO UTUSAIDFIE TWAFA.
  Wako,

  Mbwana Muungwana.

  Kwa niaba ya Wafanyakazi TTCL
   
 9. PgSoft2008

  PgSoft2008 JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2008
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  sijui tunaenda wapi ....


   
 10. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  psrc ndio wanahusika na kushughulikia ubinafsiswaji na mikataba ya makampuni ya serikali...chunguzeni huko
   
 11. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2008
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi PSRC bado iko hai?
   
 12. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Aaaah hii kali sasa kama ndo kweli mh, tumegeuzwa wajinga ndani ya nchi yetu na imenifanya nikumbuke ule usemi wa ''wajinga ndo waliwao''
   
 13. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Naona aliyekwapua kilaptop kapata password ya email sasa, keep em coming.Mi naandaa dosier kwa ajili ya kitabu kitakachotoka mwishoni mwa 2009 mahsusi kwa ajili ya kumkataa Kikwete 2010.

  Seriously!
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Kinachosikitisha zaidi ni kwamba pamoja na makosa waliyofanya mara ya kwanza walipoamua kuingia mkataba na wageni, hakuna fundisho lolote walilopata!! Makosa yale yale yamerudiwa tena!!! Watu wanaeleza hivi vitu lakini hakuna hata mmoja anayetaka kukaa chini na kushughulikia!!! :( Huyu daftari anatwambia kwamba uchunguzi unafanywa na serikali bila kutwambia uchunguzi huo umeanza lini na ni akina nani wanaohusika na uchunguzi huo na pia utakamilika lini.

  Date::10/20/2008
  Serikali yaamua kufanyanyia uchunguzi matatizo TTCL
  Na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi

  SERIKALI imeamua kuchunguza tuhuma mbalimbali ndani ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), zikiwemo za nafasi nyeti za menejimenti kushikwa na Kampuni ya SkaskTel International ya Canada na ufisadi.

  Uchunguzi huo unafanywa wakati kidonda cha menejimenti ya kukodi ya awali ya MSI/Detecon, kikiwa bado hakijapona.

  Naibu Waziri Sayansi, Mawasiliano na Teknoloji, Dk Maua Daftari alithibitisha jana kuwa uchunguzi huo unahusu tuhuma zote ndani ya TTCL.

  Kutokana na uchunguzi huo, jana Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilishindwa kukutana na vigogo wa TTCL kama ratiba ilivyoonyesha na serikali kuomba uchunguzi ukamilike kwanza.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Alhaji Mohamed Misanga, alithibitisha hilo alipoulizwa ofisi ndogo za Bunge.

  Wakati mkutano kati ya kamati na vigogo wa TTCL ukiahirishwa, Dk Daftari alisema uamuzi wa serikali kuchunguza tuhuma zote ndani ya kampuni hiyo unalenga kuondoa utata uliopo.

  "Ni kweli serikali inafanya uchunguzi unaohusu mambo yote, ikiwemo ya nafasi za menejimenti, ripoti ikitoka mtapewa," alithibitisha Dk Daftari.

  Dk Daftari alifafanua kwamba, uchunguzi huo ulikuwa ukamilike Oktoba 15, hata hivyo haikuwezekana na kwamba huenda ripoti ikatolewa wiki hii.

  Kwa upande wa Kamati hiyo ya Bunge, mwenyekiti wake Misanga alisema kutokana na ratiba kuvurugika mkutano kati yake na menejimenti ya TTCL huenda ukafanyika Dodoma wakati wa mkutano wa bunge.

  "Ratiba imekwisha vurugika, kama hatutakutana na uongozi hapa (Dar) basi itakuwa Dodoma katika mkutano ujao wa bunge," alisema Misanga.

  Wakati serikali ikichunguza ufisadi huo, duru hizo za kiserikali zinasema nafasi zote nyeti zikiwemo za Afisa Mtendaji Mkuu, Afisa Mtendaji Mkuu Masoko na Afisa Mtendaji wa Mauzo zinashikiliwa na SaskaTel.

  Nafasi nyingine nyeti zinazoshikiliwa na wageni hao ni pamoja na Afisa Mtendaji wa Fedha na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mtandao

  Wakati wageni hao wakishika nafasi hizo nyeti, wazalendo wamebaki na nafasi za wakuu wa vitengo chini ya idara na ngazi ya umeneja.

  Matatizo hayo yanayokumba TTCL kwa sasa, ni sehemu ya matatizo ambayo yaliikumba wakati wa uongozi wa miaka minne chini ya menejimenti ya MSI/Detecon.

  Mkataba kati ya serikali na MSI/ Detecon ambayo iliongoza TTCL kwa miaka minne kutoka Februari 23, 2001 hadi Februari 23, 2005.
   
 15. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kuzimu sidhani kama kuna sehemu nyingine zaidi ya hiyo
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  Natoa pongezi zangu za dhati kwa mwanahabari Ramadhan Semtawa ambaye amezivalia njuga issues za TTCL na kuanika uovu wote. Ila ni huyu huyu Semtawa ndiye aliyekuwa Public Relation Manager wa TTCL enzi hizo za deal chafu. Jee uzalendo tuu ama kuchanganya na hasira za kibarua kuota nyasi?.
  Yote tisa, kumi ya leo kali!.
   
 17. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  EL, RA, watakosa humo kweli? hebu angalieni vizuri kwani hao mawaziri sio think tank wazuri kwenye biashara ya communications
   
 18. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2008
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sio kwenye simu tuu angalieni vizuri from energy, mining , telecommunications, road contruction etc etc..viongozi wa serikalini wanakula shares left right and centre..watu tuling'ang'ani vodacom sasa mmejua kuhusu celtel...jus think about it why would celtel want ttcl mobile to succeed in the market wakati wao pia wanacompete with them ?yani ubinafsishaji umetumaliza... :-(
  Mo Ibrahim mshenzi sana anajifanya anatoa awards to african presidents kumbe ni guilt conscience yake inamsumbua hana peace of mind..he has sold all our telecommunication companies to arabs..he should be investigated!! Serikali could intervene under national security and regain TTCL..IF KIKWETE HAS THE BALLS TO!!
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Oct 25, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana kuna nchi watu wanauana mambo hayahaya..
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Waberoya,
  Nchi hii tumekwisha kabisa. Tumeacha mafisadi wametumaliza kwa visingizio mbali mbali.
  Lakini iko siku tutajilipiza. Wasije tulaumu.
  Maana watanzania ndivyo tulivyo. Badala ya kutafuta tiba leo, tunasubiri tuandamane mwakani. Mhhhhh.
   
Loading...