Kashfa ya Rushwa inayomkabili Mgombea Udiwani Frank Mang'ati

Gini

JF-Expert Member
Oct 11, 2018
398
385
*BARUA YA WAZI KWA KATIBU MKUU CCM, Dkt Bashiru Ally.*

Katibu Mkuu,
Chama Cha Mapinduzi ,
S.L.P 50,
Dodoma.
21.07.2020.

Ndugu Katibu Mkuu Chama cha Mapinduzi (Ccm) Dkt, Bashiru Ally.

*YAH: KASHFA YA RUSHWA INAYOMKABILI MGOMBEA U-DIWANI FRANK MANG'ATI KATA YA PUGU WILAYA YA ILALA.*

Husika na somo tajwa hapo juu.
Ndugu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally, kwanza nianze kwa kukupongeza kwa hatua nzuri na ya kizalendo unayoifanya katika utendaji wako kwa Chama chetu kiasi cha kukifanya kizidi kuwa imara kwa kushirikiana na Mwenyekiti wetu Ndugu *Dkt. John Pombe Magufuli.* Ndugu Katibu Mkuu pamoja na Viongozi wetu waandamizi wa Chama, mmekipa heshima kubwa sana Chama chetu kiasi kwamba wananchi wanaomuunga mkono Rais Magufuli kutokana na ukweli wa namna CCM inavyoendesha chaguzi zake kwa uhuru na uwazi wamezidi kuongezeka siku hadi siku.

Lakini ndugu Katibu, pamoja na jitihada za makusudi za kukijenga chama chetu cha CCM, bado kumeendelea kuwepo watu wanaokichafua na kukipaka matope chama kwa kuiweka taswira ya Chama hatarini hali inayopelekea wapinzani kututusi kwa kusema kuwa Ccm ni Chama cha wala rushwa. Mtajwa hapo juu Frank Mang'ati ni miongoni mwa wagombea Udiwani katika Kata ya Pugu Wilaya ya Ilala ambaye alikamatwa pamoja na wenzake watatu na Maofisa wa TAKUKURU wakiomba kupewa rushwa huku wakijua wazi kuwa ni kinyume na Katiba ya CCM.

Kwanza, Machi 21, 2019 aliyekuwa Katibu Uhamasishaji Mkoa wa Dar es Salaam, Frank Mang'ati na wenzake watatu, Katibu wa CCM tawi la Amana, Jenifer Mushi, Katibu Kata Ilala, Devotha Batulake katika klabu ya wazee Amana walishawishi rushwa ya shilingi milioni tano (5) kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya Daluni East Africa Transport, Daud Kalaghe ili waweze kumpatia kiwanja namba 41 Y kinachomilikiwa na CCM kwa shughuli ya biashara.

Inadaiwa kuwa Machi 22, 2019 katika eneo la Msimbazi Sekondari washtakiwa hao walijipatia rushwa ya shilingi milioni tatu (3) kutoka kwa Kalaghe ili waweze kumpatia kiwanja namba 41 Y kinachomilikiwa na CCM kwa shughuli ya biashara.

Taarifa hizo zilithibitishwa na Christopher Myava, Mkuu wa Ofisi ya Takukuru Mkoa wa Ilala ambapo akihojiwa na televisheni ya mtandaoni (YouTube Channel) inayojulikana kwa jina la Millard Ayo iliyoweka video hiyo mtandaoni Machi 25, 2019 yenye kichwa cha habari kilichoandikwa kwa herufi kubwa na kinachosomeka *MCHANA KWEUPE: VIGOGO WA CCM WALIVYONASWA KWA RUSHWA YA MIL 5* , ikiwa ni video yenye urefu wa dakika 1 na sekunde 53 (1:53). Ndugu Katibu Mkuu chapisho lingine linaloelezea kutiwa hatiani na kupelekewa Mahakamani kwa mgombea huyo wa kiti cha Udiwani kata ya Pugu Wilaya ya Ilala Frank Mang'ati na wenzake waliotajwa hapo awali ni wavuti (website) ya kampuni ya gazeti la Mwananchi ikiweka taarifa hiyo mtandaoni Julai 4, 2019 yenye kichwa cha habari kinachoselomeka *“Kesi viongozi CCM kuomba rushwa kuanza kusikilizwa Julai 22".*

Pili, baada ya kutoa vielelezo vinavyoonesha ushiriki wa Frank Mang'ati (Mgombea Udiwani) kuomba na kupokea rushwa hapo mwaka jana, naomba nijikite katika dhamira iliyopelekea kuandika barua hii ili haki ipatikane kutokana na ukweli kwamba kosa la rushwa ni kinyume na haki na Mh Rais amekuwa akilikemea hili ili kuweka usawa katika jamii na kwamba rushwa inapotendeka basi haki za wananchi wanyonge hupotea kama sio kukosekana kabisa. Mpaka sasa bado Frank Mang'ati ameendelea kuonesha vitendo vya kutoa rushwa kwa wajumbe ili kumpigia kura katika uchaguzi wa madiwani Kata ya Pugu unaoyarajiwa kufanyika tarehe 27.07.2020 katika ukumbi wa Checkpoint Pugu Kajiungeni.

Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2017, Sehemu ya Kwanza ibara ya 4 ibara ndogo ya 1 inasema “Binadamu wote ni sawa”. Lakini kwa viashiria vya rushwa vinavyonekana kufanyika na Frank Mang'ati ni wazi vinaondoa haki kwa wagombea wengine. Ni haki ya kila mwana CCM aliyekidhi vigezo kupiga kura ama kupigiwa kura ya kuwa kiongozi inayobainishwa Sehemu ya Pili ya Katiba ya CCM ibara ya 14(3).

Aidha, ibara ya 18(2) ya Katiba ya CCM inakataza kiongozi kutoa au kupockea rushwa. Lakini pia katika Ahadi za Wanachama wa Chama cha Mapinduzi ahadi namba 4 inayosema “Rushwa ni adui wa haki, sitopokea wala kutoa rushwa.

Sisi wananchi wa Kata ya Pugu na Mitaa yake tumeamua kukuandikia barua hii ili Chama kifanye uteuzi kwa kuzingatia uhalisia wa kiongozi atakayeweza kushirikiana na sisi Wananchi pamoja na Rais Magufulii na viongozi wengine kututumikia. Kiongozi mwenye makando kando kama haya ya Frank ni wazi anaenda kuwagawa wananchi na kusababisha mpasuko ndani ya chama. Katika uchaguzi Mkuu uliopita wa mwaka 2015 CCM tulipoteza Kata ya Pugu kwa kuletewa kiongozi asiyekubalika na hatma yake mpasuko ukatamalaki na wana CCM wakampigia kura mgombea wa CHADEMA kwa kukerwa na kitendo cha viongozi wanaulohusika katika nafasi ya uteuzi kumleta mtu tuliyemkataa, ambaye alikuwa diwani wakati wa nyuma.

Sisi wananchi wa Kata ya Pugu na viunga vyake tunaamini kuwa Chama kitayatazama hayo yote na kuamua kutuletea mgombea wa Udiwani anayekubalika na anayejitolea kutusaidia wananchi. Ndugu Katibu Mkuu tunaomba uwaelekeze viongozi katika nafasi za uteuzi walione hili na kwamba Frank Mang'ati kutokana na kushiriki katika rushwa na kupelekea kupoteza nafasi yake ya Katibu Hamasa Mkoa wa Dar es Salaam, na endapo juhudi za Makusudi hazitachukuliwa mpasuko uliotokea mwaka 2015 ndiyo nauona unaenda kutokea mwaka huu hali itakayopelekea kukosa uwakilishi unaostahili.

Tunakutakia kila la kheri katika utumishi wako. Wananchi wa Kata ya Pugu.
 
Back
Top Bottom