Kashfa ya Rushwa: David Kafulila alalamikiwa na Wazabuni kwa TAKUKURU

Unawatuma TAKUKURU si ndio wale wale tu tatizo linaanzia kutoa madaraka kwa vijana ambao ndio kwanza wanatafuta maisha mfano mkuu wa wilaya Dodoma bwana katambi hata miaka kumi hana tangu atoke chuo hivi unategemea kijana kama uyu unampa madaraja atafanyaje kama si kuwanyoosha watu kwaiyo kuomba rushwa nk maana mshahara wake haukizi anachotaka nimetolea mfano tu wa katambi sasa angalia utiriri wa vijana ambao ni wakurugenzi nk

sasa hivi ukienda halmashauri zote ambazo viongozi wake ni vijana ambao wanacheza kwenye umri wa kuanzia miaka 30 mpaka 45 kote suala la rushwa limekuwa kawaida vijana wanataka kujenga magorofa, kununua magari nzuri, kuwa na fenicha nzuri ndani kwao kuwa na ukwasi wa kutosha hapa sasa ndio fujo uanza

Wakurugenzi vijana, makatibu tawala, wakuu wa wilaya vijana na viongozi wa usalama wa taifa kwenye halmashauri, na viongozi wa takukuru wengi wamekuwa kundi moja lao moja inafikia kipindi mpaka wanauliza hakuna deal uko unategemea nini hapo

Kuna baadhi ya halmashauri tenda za serikali zikitangazwa wazabuni hawaombi maana ukiomba tu mkurugenzi ataomba hela mtu wa ugavi ataomba hela mweka hazina ataomba hela yani ni fujo tupu

MY TAKE
Ni vizuri hizi teuzi wapewe watumishi walitumikia serikali mda mwingi ambao njaa njaa hawana kama nyumba washajenga, magari wanayo watoto washasomesha hawa vijana hawa ipo siku mtasikia wametoleana bastora au kuwa na kisa wamedhurumiana

Mfano mzuri morogoro mh waziri mkuu aliona mkuu wa wilaya na mkurugenzi wanavyovimbiana kisa nini pesa kila mtu anataka kupiga dili
 
Back
Top Bottom