Kashfa ya Rushwa: David Kafulila alalamikiwa na Wazabuni kwa TAKUKURU

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
650
1,000
Wakuu,

Wafanyabiashara Mkoa wa Mbeya na Songwe wailalamikia ofisi ya RAS Songwe na moja kwa moja wanamtupia lawama Katibu Tawala Mkoa huo Kafulila kwamba amekuwa akiwaomba Rushwa endapo ukikataa basi kama ulikuwa mzabuni unanyang’anywa tenda.

Inadaiwa hivi Karibuni, Serikali walitangaza Zabuni kusambaza Dawa katika Mikoa mbalimbali nchini mbadala wa MSD na Zabuni ikashindanishwa Team ya wataalam kutoka Tamisemi pamoja Mkoa wa Songwe ikawapitisha washindi.

Lakini baada ya mwaka 1, Bwana Kafulila ameanza kuwatisha wafanyabiashara walioshinda na kuomba rushwa ili kutositisha mkataba ambao huchukua miaka 3

Inadaiwa kwamba Kafulila amegombana na Team ya wataalamu akiwepo Mfamasia na baadhi ya wajumbe na amekuwa akishirikiana na Katibu wa Afya Mkoa Dada Hobokela.

Kuna madai kuwa RAS amepewa kiasi cha Fedha kutoka kwa Mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la Babito anayemiliki hotel za Beaco jijijni Mbeya, amekuwa akifukuza watumishi na wengine kuwahamisha kinyume cha utaratibu.

TAKUKURU fanyieni kazi habari hizi ili ukweli ujulikane.
 
Peter Madukwa

Verified Member
Sep 20, 2012
183
1,000
Oh.. Aseh hatari, kama ni kweli basi kazi hpo, rushwa ni adui wa haki, JPM akijiridhisha atamtumbua.
 
KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,669
2,000
kama ni kweli naamini haki itatendeka kwa yeyote. Mimi uwa najiuliza ni kwa nini mtu analipwa mshahara mzuri na kazi yenye marupurupu ya kutosha anaingia tamaa ya kupokea rushwa. kwa nini?

kwa hali ilivyo, Rais wetu ana kazi ngumu sana kwa kuwa mambo ya rushwa na ufisadi hakubaliani nayo na wanaomkwamisha katika jitihada zake za kupamabana na rushwa ni vigogo. nini kifanyike? hakika inauma na inaumiza
 
infinix

JF-Expert Member
Sep 6, 2018
2,099

Kesi ya tumbili wampelekea nyani weye?
Hao wote wanakula mahindi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom