Kashfa ya Richmond: The FACTS

Site yao ni hii, a very very shady website. Lets just say, this is not the type of company a country should do business with. Look through for yourself.

Hata ka sehemu ka ku apply kazi hamna :D

http://www.rdevco.com/
 
sidhani kama mabadiliko ya kweli yatatoka CCM, ila CCM italazimishwa ibadilike!! chama cha Mapinduzi cha Mexico kilitawala mfululizo kwa miaka 70 huko lakini kikaja angushwa na Vicente fox. CCM haitabadilika itaangushwa. Kama ni miaka kumi kuanzia sasa au thelathini ijayo.. CCM itaondoshwa madarakani!!!!!
 
Hiyo used Generator haina thamani ya hizo pesa na umaweza ukapiga sime GE ukauliza ni uizi tu huu!!!!, ni kwanini wananunua hizo machine kwa pesa nyingi hivyo kutoka kwa watu?? wakati wanaweza kupiga simu GE wakauziwa direct?? huyo jamaa anautalaamu gani wakati biashara yake ni ya printing na kampuni imeanzishwa miaka mitatu 2003!!!

Tunaweza kutafuta price quotes kutoka makampuni mbalimbali yanayohusiana na magenerator hayo; huwezi kupata generator la MW100 kwa zaidi ya $40m.
 
Richmond development company
Habari za saizi ndugu zangu, mimi naomba niwaelimishe kidogo kuhusu hiyo kampuni ya richmond development company. Hizi ndiyo ukweli.

1. Kampuni hiyo ipo hapa Texas, lakini siyo corporation ni personal business hivyo haihitaji kuwa register Austin makao makuu.Hii ni jinsi ya kuiangalia
a) paste hii link http://www.cclerk.hctx.net/
b) Go to - Search Databases
c)Go to- Asumed Names
d) Enter Name - Richmond Development Company

2. Nimeenda kwenye hiyo adress na huu ndiyo ukweli
a) hiyo small building imeandikwa Richmond printing na sijaona kitu chochote kuhusu richmond development. Ni ka warehouse fulani hivi na inaonyesha wanafanya biashara ya printing.
b)Nimeulizii owner na nimekutana na watu wanaomfahamu anasema ni Mtanzania aliye na hasili ya kiasia aliamia huku miaka ya 80's na anafanya biashara ya printing. Kwa jinsi nilivyo angalia record za nyumba huyo jamaa ni tajiri kwani nyumba yake inathamani zaidi ya $1m .
c) Huyu jamaa wakati waziri mkuu sumay alivyo kuja hapa Houston alifanya private meeting na tunaona matunda yake.
d)Biashara yake imeanzishwa mwaka 2003
c) Hana specific office ya hiyo biashara ni pale pale iliko biashara nyingine.
Reply With Quote

Asante kwa data.

Kazi ya Sumaye na Mkapa inaonekana. Inelekea Kikwete anaendeleza wembe ule ule.
Mwaka 2004, anasemekana huyu jamaa wa Richmond alimkalisha Balozi Daraja pale Houston kwa siku kama tatu hivi, watanzania wengine wote hawakupata nafasi ya kuonana na Daraja ambaye alikuwa amekuja hapo Houston kuwatembelea watanzania, je hiyo stori ni ya kweli ndugu yetu kamundu?
 
Majambazi makubwa baada ya kuona watanzania wanapiga kelele sana kuhusu ujambazi wa IPTL!!

Ikabidi majambazi wakae chini na kusema inabidi sasa tutoke na Richayamondi!!

ili aipil ife!

inauma!!
 
Waziri aitetea Richmond si ya kigogo

Na Abdallah Bawazir

WAZIRI wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, amesema hakuna kigogo wala mtoto wa kigogo mwenye maslahi katika kampuni ya Richmond iliyopewa jukumu na serikali la kuleta mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura nchini .

Karamagi aliitisha mkutano wa waandishi wa habari jana kutoa maelezo hayo na kufafanua masuala mbalimbali yanayohusiana na kampuni hiyo, pamoja na mikakati ya serikali ya kukabiliana na tatizo la umeme nchini.

"Napenda kuwahakikishia kuwa hakuna kigogo wala mtoto wa kigogo kwenye kampuni ya Richmond," alisema Waziri huyo mwenye dhamana na masuala ya umeme, ambao kwa miezi takriban sita sasa unapatikana kwa mgawo.

Akielezea jinsi kampuni hiyo ilivyopata zabuni ya kuleta mitambo ya kufua megawati 100 za umeme, waziri huyo alisema ilipatikana kwa njia ya zabuni iliyotangazwa duniani kote.

Alisema makampuni manane ya ndani na nje ya nchi yalijitokeza kuwania zabuni hiyo na kampuni hiyo ilifanikiwa kushinda zabuni hiyo kutokana na kutimiza masharti na vigezo vilivyokuwa vimewekwa.

Alivitaja vigezo hivyo kuwa ni unafuu wa bei ya umeme na upatikanaji wa haraka wa vifaa.

Alisema baada ya makampuni hayo kujitokeza, serikali iliunda kamati ya kupitia na kuchambua maombi hayo kwa kila kampuni kabla ya kumtangaza mshindi.

Karamagi alisema katika makampuni yote manane yaliyojitokeza, Richmond ndiyo iliyofikia vigezo hivyo na kupewa zabuni ya kuleta mitambo hiyo.

Aliyataja makampuni mengine yaliyoomba zabuni hiyo na bei zake kwa dola za Marekani kuwa ni Upagum (senti 4.5), Aggreko (senti 6.79), Globalake (senti 5.8), Richmond (senti 4.99), Renko (senti 10), Onetus (dola 1.11), Reo Ernegy ya Kenya na Gapco ya Tanzania.

Alisema kutokana na Richmond kuonekana kuwa na umeme wa bei na nafuu, ilichaguliwa kutoka miongoni mwa makampuni hayo. Alisema wakati ikiomba zabuni hiyo, ilikuwa ikishirikiana na kampuni nyingine kubwa ya kutengeneza injini za ndege, jambo ambalo pia liliisaidia kushinda zabuni hiyo.

Kwa upande mwingine Karamagi alisema kampuni hiyo ya Richmond tayari imeshapata mitambo mingine iliyobaki, yenye uwezo wa kuzalishamegawati 80 za umeme.

Alisema mitambo hiyo imepatikana nchini Afrika Kusini na kwamba kutokana na nchi hiyo kutokuwa mbali sana na Tanzania, inatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kwa ajili ya kufungwa na kuzalisha umeme kabla mwisho wa Desemba.

Hata hivyo, alisema mitambo hiyo inaweza isiletwe yote kwa mkupuo bali kwa awamu, lakini akasisitiza kuwa hadi mwishoni mwa Desemba itakuwa yote imeshawasili na kuanza kuzalisha umeme kama ilivyokusudiwa.

Waziri huyo aliongeza kuwa makampuni yote yaliyopewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura nchini, yamepewa mikataba ya miaka miwili na baada ya hapo serikali itakuwa imeshajiweka tayari kwa ajili ya kuwa na vyanzo vyake yenyewe vya kuzalisha nishati hiyo.

Pamoja na Richmond, kampuni nyingine iliyopewa zabuni hiyo ya miaka miwili ni ya Aggreko ambayo inazalisha wamegawati 40 za umeme. Kampuni hizo zimepewa mkataba wa miaka miwili, lakini haikuelezwa bayana baada ya muda huo mitambo hiyo itapelekwa wapi.

Akieleza mipango ya muda mrefu ya serikaliya kuwa na mitambo yake yenyewe ya kuzalisha umeme, Karamagi alisema ni pamoja na kununua mitambo aina ya Wartsilla yenye uwezo wa kuzalisha megawati 100.

Alisema mitambo hiyo yenye thamani ya Euro 58.2 milioni itafungwa eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam na hadi kufikia Agosti mwakani itakuwa tayari imeanza kuzalisha umeme.

Alisema mikakati mingine ni kufunga mtambo mwingine aina ya Oret katika eneo la Tegeta ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 45 na kwamba mtambo huo utakuwa tayari kwa matumizi mwishoni mwa mwaka 2007 au mwanzoni mwa 2008.

Alisema pia kuna mkakati wa kuingia mkataba wa kuzalisha umeme wa megawati 200 ambao mitambo yake itajengwa katika awamu tatu, ya kwanza ikianza Julai mwakani kwa kuzalisha megawati 50. Aliongeza kuwa mtambo mwingine wa kuzalisha megawati 100 utafungwa mwishoni mwa mwaka huo na uliobaki wa megawati 50 utafungwa mwanzoni mwa mwaka 2008.

Alisema mitambo yote hiyo itakapofungwa, itakuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 475 za umeme ambazo zitatosheleza na kumaliza kabisa tatizo la mgao wa umeme nchini.

http://www.mwananchi.co.tz/mwananchisite/Mwananchi/Habari/Habari0.asp
 
EVENTS


Richmond Development Company of Houston (RDC) which is developing several projects in the East African nation of Tanzania hosted The Tanzanian Ambassador to USA, The Honorable Andrew M. Daraja to Houston, Texas, from July 20 through to July 22, 2003.

During his visit, Ambassador Daraja was introduced to the leaders of the business community of Houston, which also included alliance partner companies of RDC.

Ambassador Daraja acknowledged that the African region is becoming prominent with regard to the economic and strategic interests of United States as evidenced by President Bush's recent trip to the region.

"With some of our Tanzanian projects approaching financial close, RDC will add new high caliber jobs in Houston" said Dr. Huque, a principal at RDC.

"The fact that Ambassador Daraja came to Houston demonstrates the commitment of The Government of Tanzania to extend business cooperation of Houston based companies" added Mr. Gire, another principal at RDC.


PRINCIPLES


Mohamed A. Gire EMAIL
Mr. Gire is a prominent businessman and an active private investor in emerging high-tech companies and offshore real estate and Infrastructure sectors.
Mr. Gire brings a unique blend of talent and over 20 years of business acumen into growing strategic companies.
Mr. Gire serves on numerous boards and commissions including a Houston's Mayoral Advisory Board for International Affairs and Development.
Energy/Refinary companies that are interested in forming business alliance with us, are welcomed.

Mohammed S. Huque, Ph. D EMAIL
Dr. Huque has over 25 years experience in the energy/infrastructure sector. For the last seven years he has been a successful developer of infrastructure projects totaling $U.S. $500 million.
He is a specialist in project financing and has worked extensively with multi-lateral financing agencies (World Bank Group, Asian Development Bank) and export credit agencies.
Dr. Huque has served as senior executive with multi nationals such as Westinghouse Electric Corporation and Marathon Oil/Duquesne Light, to name a few. He has lived and worked in Europe, Middle East, Asia and Japan.
Dr. Huque earned a Ph. D in economics from the University of Manchester, United Kingdom and is a past fellow of the the Leadership Institute, Duquesne University, Pittsburgh, Pennsylvania.



ACCOMPLISHMENTS & NEW PROJECTS


Financially Closed Projects
130 MW Power Generation Station in Gaziantep, Turkey. Project Value: $117 million.
Upstream Oil & Gas in collaboration with Major Oil Company in The Balkans. Project Value: $150 million.
Leveraged Buy Out (LBO) of an Infrastructure Development Company in The State of Michigan, USA.

Projects Currently Under Development
National Sports Stadium with seating capacity of Sixty Thousand Spectators.
1,150 km of Petroleum Product Pipeline plus Five Terminals.
Redevelopment of Multiple Civil Airports.



HOW LOW CAN LOWASA & HIS SON GO BY DEALING WITH THESE GUYS?

PILI HAWA JAA WALIFANYIWA VETTING? THEY COULD HAVE LINKS WITH TERRORISTS...AFTER ALL I ASSUME SIO WATANZANIA HAWA
 
Karamagi alisema katika makampuni yote manane yaliyojitokeza, Richmond ndiyo iliyofikia vigezo hivyo na kupewa zabuni ya kuleta mitambo hiyo.

Aliyataja makampuni mengine yaliyoomba zabuni hiyo na bei zake kwa dola za Marekani kuwa ni Upagum (senti 4.5), Aggreko (senti 6.79), Globalake (senti 5.8), Richmond (senti 4.99), Renko (senti 10), Onetus (dola 1.11), Reo Ernegy ya Kenya na Gapco ya Tanzania.

Alisema kutokana na Richmond kuonekana kuwa na umeme wa bei na nafuu, ilichaguliwa kutoka miongoni mwa makampuni hayo. Alisema wakati ikiomba zabuni hiyo, ilikuwa ikishirikiana na kampuni nyingine kubwa ya kutengeneza injini za ndege, jambo ambalo pia liliisaidia kushinda zabuni hiyo.

Kwa upande mwingine Karamagi alisema kampuni hiyo ya Richmond tayari imeshapata mitambo mingine iliyobaki, yenye uwezo wa kuzalishamegawati 80 za umeme.

Alisema mitambo hiyo imepatikana nchini Afrika Kusini na kwamba kutokana na nchi hiyo kutokuwa mbali sana na Tanzania, inatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kwa ajili ya kufungwa na kuzalisha umeme kabla mwisho wa Desemba.

(1) Zabuni hiyo ilitangazwa wapi? Aseme medium ilyotumika. Kwa nini imechukua muda mrefu sana kutuambia kama kweli tenda ilitangazwa. Halafu inakweaje tenda za Serikali ya Tanzania zinagombewa na makumpuni uchwala tu kama haya: Upagum, Aggreko, Globalake, Richmond, Renko, Onetus.


(2) Hawa jamaa wanababaisha mambo; mara ya kwanza walisema kuwa walileta consignement ya kwanza kulingana na uwezo wa ndege ya Urusi waliyokuwa wametumia, na kwamba sehemu nyingine ingefikla baada ya muda si mrefgu. Sasa wanadai wamepata generator nyingine South Africa. Hapa inaelekea kama wanacheza danadana.

(3) Ni vizuri details za contract zijulikane wazi wazi. Hii ni contract inayohusu public funds, kwa hiyo siyo siri hata kidogo. Wananchi wana hakio ya kujua pesa yao inatumiakje.
 
Kichuguu,
You are right. Wanacheza danadana.Unakumbuka ile mitambo ilikuwa inaletwa kutoka Marekani? Sasa kivipi ghafla bin vuu mitambo inanunuliwa Afrika kusini?
Nasikia huyu Gire alichangia sana kwenye kampeni za Kikwete, sasa sishangai kama ni pay back kwa kutumia migongo ya Watanzania. Matatizo ya umeme yataendelea hata baada ya December. Mark my words.
 
Hey guys hiyo website ina wiki mbili au tatu tu kwasababu nilijaribu kuitafuta bila ja majibu mwezi uliopita!! na hizo deal ni za wongo maana hawa jamaa hawana hata office na wameifungua 2003. Kitu kingine ni kwamba kuna kampuni nyingine mbine za U.AE zimepata contract lakini hatuziongelei hivyo mwizi si richmond peke yake kuna wezi wengine wawili!!
 
Ukweli ni kwamba mosi, hawa jamaa wa Richmomd wameshindwa kutimiza ahadi walizoziweka wao wenyewe wakati wanasaini mkataba na serikali pili, kuweka habari za miradi ya uongo kwenye tovuti yao, kwamba wao ndio wasimamizi wakati sio kweli tatu, creditworthiness yao hailingani na mkataba waliopewa ambao hawakusema ukweli tokea mwanzo. Ofcourse vitu kama hivi vikitokea na kuwa wazi halafu hauoni Rais wala waziri wake mkuu anafanya chochote au anawahamisha watu wizara tu, basi lazima ujue kwamba kuna kuleana kwa aina fulani. Mbona jengo lilivyoporomoka huko Chang'ombe waziri mkuu alitoa miongozi waziwazi?

Mimi kwa mtazamo wangu, ukiondoa nani kafanya nini katika mjadala mzima wa Richmond, lawama zangu zote zinaenda kwa Rais wa nchi kwamba anatuonyesha wazi kabisa kwamba ni dhaifu katika uongozi na labda anachoweza ni porojo na safari. Unavutia vipi wawekezaji wakati hata sera zako za umeme zimejawa na rushwa na mizengwe na bado haufanyi maamuzi yanayoelekeza kuwapa watendaji fundisho? Nani atawekeza kwenye nchi ambayo hata umeme hauna uhakika? Kazi watafukuzwa wahandisi wa halmashauri, wakuu wa wilaya, lakini mbona hao wala rushwa wakubwa hakuna hata mmoja ambaye ameshakamatwa na kushitakiwa wakati kipo chombo kinachoendeshwa kwa mamilioni ya fedha za walipa kodi kila mwaka?

Hata mtu ambaye ushahidi wa kumshitaki uko wazi kabisa kama Profesa Mahalu, wanashindwa kumpeleka mahakamani? Balozi wa Tanzania nchini zambia/malawi amekula fedha waziwazi kabisa wanamsubiri astaafu halafu zile alizoiba zikatwe kutoka kwenye pension yake, lakini mhasibu wake aliyeshirikiana nae amefukuzwa kazi!?! uliiona wapi hiyo?

NAfikiri nikiangalia baada ya miaka mitano nchi hii itakuwa kwenye hali mbaya kiuchumi kama aliyoiacha mwinyi. Kitu cha maana kimoja alichofanya na kiongozi wetu mpya huyu labda ni kuwakaripia na kuwatishia viongozi wa chini hasa wa serikali kuhusu uhudumiaji wao kwa wanachi, ambayo ni nguvu ya soda na itaisha tu.

Mungu irehemu Tanzania na uiepushe na majanga yaliyo mbele yake........
 
Hawa jamaa wa awamu ya nne wanatuyeyusha. Wanaendesha nchi kisanii, huyu JK si alituahidi mambo ya mgao yataisha hivi karibuni?,sasa kila siku wanatujia na jipya. Mzee Ben yeye alakuwa kimya,ila mambo yakawa yanaenda, hawa jamaa kila siku kelele nyingi, mambo hayaendi. Huo ndio usanii wenyewe.Na hii ishu ya Richmond, kuna nyepesi mtaani zinazosema Mtoto wa Lowassa anahusika,ila ni nyepesi tu, hazina uthubitisho. Ila mambo yanayosemwa semwa mtaani huwa yana ukweli wake.Kwahiyo mimi naona ingawa wananchi wanamategemeo makubwa sana na huyu JK na wenzake,na wao maneno yamekuwa mengi, ahadi nyingi ila hakuna kitu,watu watakuja kumkumbuka mzee Ben tu.
 
Dr Idrisa hana mchezo atawanyosha watu pale lakini hataweza kubadilisha mikataba ya rushwa.
 
Mmesikia Tanesco wako mbioni kuongeza bei ya umeme kutokana na gharama za uendeshaji kuongezeka!! Hivi kwanini watu wanafikiri Watanzania ni wajinga sana!!... Mr. President livunje hili shirika and spare us the misery please!!
 
Hapo ndio WaTz watakapolia na kusaga meno, kwa nini walioleta hii fracas wasiadhibiwe? hii itaathiri sana uchumi, kweli maisha bora tutapata kwa mwendo huu?
 
Mmesikia Tanesco wako mbioni kuongeza bei ya umeme kutokana na gharama za uendeshaji kuongezeka!! Hivi kwanini watu wanafikiri Watanzania ni wajinga sana!!... Mr. President livunje hili shirika and spare us the misery please!!

Mwankijiji nafikiri swali lako lingekuwa "Hivi kwa nini Watanzania ni wajinga sana?' Sababu ingekuwa kama swali lako lilivyo originally tungetarajia wangeutumia werevu huo unaodhani wanao kufanya kitu. Wacha watulize mpira hii ndiyo ari,kasi na nguvu mpya kuelekea kwenye Tanzania yenye neema. Kajisemea alles au qarz? kisichowezekana duniani kote kinawezekana Tanzania


_________________________________________________
Ni afadhali kuishi siku moja kama simba kuliko siku mia kama nzi (Nietche)
 
Back
Top Bottom