Kashfa ya Richmond: The FACTS

Kichuguu,
wakati tunapata uhuru mengi yalisemwa na kweli tulikuwa hatupo tayari kwa sababu waafrika wengi tulikuwa hatufahamu nini maana ya Uhuru.. leo hii inaonyesha wazi. Nyerere aliyajua yote haya na ndio maana ilipovumbuliwa gas na mafuta miaka ya 70's na mwanzo 80's Nyerere alidai ziachwe huko chini ardhini kwa sababu watu wangu hawana elimu wala uwezo wa ku-deal na mali kama hiyo. Wote wataacha kufanya kazi kwa sababu utajiri umepatikana!...Kwa mwafrika utajiri ndio maendeleo yenyewe.
TZ tunayo mafuta na wala msije danganywa!
Nyerere hakufahamu tu kuwa mbali na elimu tulikuwa bado na akili za kitumwa na hadi leo bado hatujaelemika zaidi ya elimu ya kitumwa!...Sasa Tazara nayo itauzwa kwa mpango gani hali ni mali ya jumuiya?... Zambia wapo radhi?... jamani mweee!...mimi nipeni hiyo Tazara club tosha kabisa nitafunga domo langu.kwi..kwi...kwi...
Kichuguu sii Mlima, nenda kwenye mada ya Idriss Rashid, leo nimeweka orodha ya viongozi walioshiriki kuipitisha IPTL kisha nambie kabaki nani?... na list itaendelea kesho. Kila unayemfikiria kuwa msomi mzuri utamshangaa ktk maamuzi.. JK, Mwinyi na Mkapa ndani mshikaji sasa hapa kweli tutafika?
 
Mzee Es said:
Ndio maana mzee wa usalama wa DC, yuko kwenye maji ya moto over the Richmond ameulizwa alikuwa wapi?

Yeah Yeah huyu Station Chief wa DC ameshindwa kazi!
Ameshatulostisha vya kutosha!
 
Mkandara said:
Kichuguu,
wakati tunapata uhuru mengi yalisemwa na kweli tulikuwa hatupo tayari kwa sababu waafrika wengi tulikuwa hatufahamu nini maana ya Uhuru.. leo hii inaonyesha wazi. Nyerere aliyajua yote haya na ndio maana ilipovumbuliwa gas na mafuta miaka ya 70's na mwanzo 80's Nyerere alidai ziachwe huko chini ardhini kwa sababu watu wangu hawana elimu wala uwezo wa ku-deal na mali kama hiyo. Wote wataacha kufanya kazi kwa sababu utajiri umepatikana!...Kwa mwafrika utajiri ndio maendeleo yenyewe.
TZ tunayo mafuta na wala msije danganywa!
Nyerere hakufahamu tu kuwa mbali na elimu tulikuwa bado na akili za kitumwa na hadi leo bado hatujaelemika zaidi ya elimu ya kitumwa!...Sasa Tazara nayo itauzwa kwa mpango gani hali ni mali ya jumuiya?... Zambia wapo radhi?... jamani mweee!...mimi nipeni hiyo Tazara club tosha kabisa nitafunga domo langu.kwi..kwi...kwi...
Kichuguu sii Mlima, nenda kwenye mada ya Idriss Rashid, leo nimeweka orodha ya viongozi walioshiriki kuipitisha IPTL kisha nambie kabaki nani?... na list itaendelea kesho. Kila unayemfikiria kuwa msomi mzuri utamshangaa ktk maamuzi.. JK, Mwinyi na Mkapa ndani mshikaji sasa hapa kweli tutafika?


Mkuu nimekusikia,
 
kichuguu said:
Nasikia kuwa wakati tunaelekea kupata Uhuru, kuna wazungu walimwambia Nyerere kuwa nchi yetu ilikuwa haijawa tayari kwa uhuru. Lakini Nyerere aliwashinda kwa hoja na mwishoni tukapata uhuru huo kabla ya nchi zote za afrika ya mashariki. .......

Si wazungu tu, kama sikosei hata Mtemi (Chifu?) Mareale, alisema hivyo hivyo, na nifahamuvyo miye (ki historia) ni kuwa yeye alifunga safari hadi UN kumchalenge Mchonga kuwa TZ bado saana, tunahitaji miaka mingine kadhaa kabla hata hatujafikiria huo uhuru. Of course Blah blah za mchongo zilimsaidia na uhuru fake ukapatikana. Pia historia inasema ati Machief wengi waliomba uongozi uwe based ki aina aina ya uchief, yaani kama kule Iringa badala ya kuokota jamaa yeyote tu na kumpa uongozi, apatiwe mtu ambae eshawahi ongoza, au aliekuwa recommended na ma Chiefs kama mkwawa, na machief wengine wa maeneo hayo, nk. Kule moshi vivyo hivyo, mwanza, kagera nk. Of course mchonga tena akakataa katakata.

Sasa hivi sote ni watumwa nchini mwetu, na hakuna anayejua pesa zetu, madini yetu, mbuga zetu, bahari na beach zetu, v zinamnufaisha nane.... Miaka 45 baada ya uhuru tushaanza kuwa na viongozi limbukeni ambao wanajiona ni miungu watu watu wanatembeza ubabe bila hata ya aibu!

Tukirudi kwenye hiyo jenerata nikumbukavyo mimi ni kuwa imeazimwa tu!, yaani biashara kichaa tu, hapo tumenunua mbuzi kwenye gunia...Cha ajabu ni kuwa kwenye baraza la mawaziri ma PhD, Masters etc kibao, sijui hao jamaa elimu yao inawasidia vipi...kwani maamuzi yao hata ngumbaro ana nafuu!
 
taarifa nyepesinyepesi zimezagaa mjini kuwa mtoto wa EL na jk wana interest kwenye kampuni ya richmond ,one of them is director,na pia wanaagiza majenereta yanayouzwa kama njugu jijini na kuwapa wahindi wauze.
inaelezwa zaidi kuwa hata pesa ya kukodi cargo plane richmond hawakua nayo ,imebidi serikali ilipe ,pia genereta hizo wamehike bei kutoka bei yake ya halali ya 40m usd na wame quote 180m usd.
tunaomba msajili wa makampuni atupe details na kujua pia kama kampuni ni halali marekani na inalipa kodi,uzoefu na list ya wateja wake wakubwa for reference.

kama kuna mwana forum an taarifa zaidi tushirikiane....kwa manufaa ya tanganyika yetu[tanzania]
 
Bro Phil,hizi news mbona hazina moto tena...sijui,labda kuna wageni watakuja na mpya
 
Kwa habari nzito kama hiyo tunategemea more credible evidence kuliko hiyo ya kusema habari nyepesinyepesi!
 
msaidieni kijana huyo.. mbona watu wanaelewa hayo yote....ila hilo la watoto wakubwa kuhusika.. maneno matupu hayatoshi.. tupe details..
 
nashukuru sana for some response,but si unajua hata mkuu alisema kuwa ushahidi wa haya mambo under cover ni mgumu kupatikana na akasema utawala wake pia atakubali cicumstatial evidemnce kuamua mambo corrupt.ni kama mtu akuambie utafute ushahidi katika mambo ya adultery,utabaki kuwa crcumstatial.
sasa kweli kama kampuni haijasajiliwa marekani ,hailipi kodi huko,haijawahi kuwa na historia ya relevant service,haina finatial stability hadi serikali imewapa pesa ya kusafirishia na awali walitaka kuiingiza mjini crdb ili iwape guaramtee,bei wamehike mara nne ,hiyo kwangu ndio circumstance inayofanya niweze kaamini kuna grift act.
haya mambo ya uhujumu ni ngumu kupata link ya moja kwa moja ndio maana pcb hadi leo wameshindwa kumfikisha costa mahakamani.rais alisema hatangojea ushahidi wa kimazingira ,,je na hapa hajaona???
tuendelee hivi????????????
 
kadiri hii mada inavyoendelea watatokea watu wamaowajua hawa washkaji ,[wATOTO] na watasema wanavyotuasha gap,,,hapa tumeshokoza mada tu.!!!!!!
 
Phillemon,

Ulichosema ni kweli. Haiwezekani serikali iingie mkataba kama huu na kutoa fedha nyingi kiasi hicho bila viongozi kujua. Nilifuatilia kwenye website ya huyu bwana Gere na kugundua kuwa biashara yake ni ya printing; hajwahi kufanya biashara yoyote ya mejenereta na wala hana hata ujuzi wa mambo ya majenereta. Kwa bahati nzuri mekuwa na uhusiano wa karibu sana na balozi wa Tanzania hapo Washington DC bwana Daraja. Makampuni yanayoshughulikia mambo ya powere yapo mengi sana. Kitendo cha serikali kutoyaona makampuni hayo na badala yake kutoa tenda kubwa hivyo bila kutangazwa kwa kampuni ambayo siyo credible ni jambo linaloashiria kuwa kuwa rushwa imfenayika hapa.

Kwa sasa tunajua kuwa genereta iliyoletwa ni ya MW22 kwa na wala siyo MW 100 kama tulivyoambiwa na bei yake ni $175m. Inajulikana kuwa genereta mpya kabisa ya MW100 inauzwa kwa bei isiyozidi $38m, kwa hiyo hiyo tofauti ya bei kati ya genereta ya MW22 na ile ya MW 100 ni jambo ambalo linaashiria rushwa, tena rushwa kubwa kabisa. Kwanza kabisa hatujui kuwa genereta lililoletwa ni jipya au limeshatumika. Sasa hivi kuna tetesi kuwa jenereta lenyewe ni la kukodi. Kama siyo rushwa kweli itakuwa nini ati. Ina maana viongozi wetu ni wapumbavu kiasi kuwa wanaweza kufanya jambo kama hili bila wao kunufuaika kweli.
 
Tunataka data tu...na si vinginevyo, la sivyo kila mtu atakuwa anakuja na nyepesi nyepesi tu.
 
bw mafuchila ,,shamba la babu linaliwa..naamini watu wanaochangia huku hawana sababu ya kutoa tuhuma baseless ,hatuna muda huo,wenye interest na kulipua mabomu ni wale wa jukwaani,,.,tuna uchungu mkubwa na nchi yetu na hatuwezi kuamua ,hili ndio jukwaa letu ,,,sehemu wanapoulizana ushahidi ni dodoma na kama mtu hana anafukuzwa barazani..

hii mambo ya kutaka ushahidi wa kisheria ndio imefikisha nchi yetu hapa ,,hutakaa upate data za kumtia mtu hatiani tanzania,,labda marekani ambapo hata rais ameshawahi ku resign kashfa ya watergate...

hali halisi ndio hiyo hizo cicumstance zilizopelekea kampuni ya printing kupewa tenda ya nishati zinaashiria nini,..

tusiwe kama tomaso hakutaka kuamini hadi ashike tundu za misumari!! sisi kama wazalendo tuanzie kwenye hizi tuhuma na tuzifanyie kazi siriaz,,
hatuko hapa kumuonea mtu .,.we are here to debate fairly on the future of our offsprings!!! watakuta nini,,au watakua manamba at the expense ya wachache ,,,tatizo la corruption zetu ni cheap,,

nyrere alisema rushwa ya asia inaliwa,kazi inafanyika below standard,ulaya wanakula na kazi inafanyika vilivyo,,kwetu tunakula rushwa na kazi haifanyiki ,,kwa maana nyingine tunakula hadi MTAJI
 
Mzee P,

Sikupingi lakini kama kweli unayosema basi Jk asingewashukia kina Masha, na Msabaha kama alivyofanya, nasikia Msabaha alikuwa akimdanganya Jk kuhusu hiyo kampuni, ninachojua so far ni kwamba Msabaha, Daraja, na Syskes ndio waliohusika na mchezo mzima wa Richmond, na hasa Syskes as a front!

Lakini lisemwalo linaweza kuwa lipo, na hasa hizi siasa zetu za bongo anything is possible!
 
Mzee ES, hata mimi hainingii akili mwangu eti JK ana hisa katika hilo kampuni! Ili iweje?

kama ni hela JK sasa anazo itakuwaje awe na tamaa ya aina hiyo. Na kama ni kweli basi dunia hii kweli imekwisha!

watoto wake wame mfano wa kigwa wapate mali zao kwa uhalali. Wana shida gani ya kuanza tamaa ya hela? Kama ni ajira nzuri watapata kama wamesoma.

Hii habari ninadhani ina walakini au ni uchavuzi tu! But kila kitu kinawezekana!
 
Nani aliwalazimisha?

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE 'mail box' story of Messrs Richmond Development Company is getting sexier: the bedfellows are now disowning it, THISDAY can report.

The Tanzania Electric Supply Company, the country's only utility firm ? has come in the open to say it never negotiated the 100MW contract for the gas generators with the make-believe US firm.

Tanesco's general manager for distribution and customer services, Anton Booyzen, now says his firm was 'instructed' to sign the deal by some top official of the ministry of energy and minerals, then headed by Dr Ibrahim Msabaha.

''NetGroup staff were not involved in any of the negotiations with Richmond, so this thing placed us in a very difficult position when the contracts had to be signed,'' Mr Booyzen says in a written statement in response to questions from THISDAY.

He adds: ''Any professional person would be hesitant to enter into any arrangement and then to be held responsible for the execution of such arrangement, if he or she was not part of it in the first place.''

The RDC has twice failed to deliver on gas turbines since last September, and is still struggling to assemble the first consignment. Even then, the RDC has promised to start power generation by the end of this year
Currently, there is a power purchase agreement of sorts between Tanesco and Songas, which determines the performance level, including blackouts, which Songas must maintain, with clauses on penalties to be applied when the company fails to achieve those minimum performance levels.

Songas supplies 140 MW of gas-fired turbines power to Tanesco from natural gas extracted at the Songo Songo islands of Kilwa District. Two of the 40MW turbines have broken down this year, causing the unpredictable power blackouts, euphemistically known locally as 'power rationing.'

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) national chairman Freeman Mbowe recently claimed that a son of a senior government official is one of the directors of the RDC, a fact that paints the firm in favourable light with senior government functionaries despite its dismal performance.

The RDC was awarded a controversial $172m (206.4bn/-) for the supply of generators despite the fact that it is not known in the State of Texas, where officials said it was 'a mailbox' company
 
guys this thing is very serious!!
unajua kuna siri moja kubwa ya matatizo ya tanzania nayo ni ujinga.
ujinga wenyewe unatokana na ubinafsi,kutokuwa makini, na kutokuona mbali.
unajua nchi za ulaya,marekani zinaendelea sio kwasababu wananchi au raia wote wanahusika bali kuna watu wachache wenye akili sana wamewekwa zile sehemu nyeti zote na ndio hao wanafanya decition making and all the planning.

lakini ukija sisi watanzania zile sehemu nyeti zote watu wamewakana pale kwa kujuana,urafiki,undugu..nk
KUANZIA BENKI KUU,TRA,WIZARA ZOTE MUHIMU,UBALOZINI,KWENYE MABENKI,TANESCO,BANDARI etc utaona wengi wanaofanya kazi huko waliwekwa tu, kwasababu walipigiwa cross na jamaa zao au ndugu zao.

sasa matokeo yake nini.
tuna vijana wengi wenye uwezo mkubwa kiakili lakini matokeo yake vijana hawa wanaajiriwa na makampuni binasfi au wengine wanatokomea ulaya na marekani na wanaishia huko.
huku nje wapo watanzania ambao wanafanya mambo makubwa kwenye sekta mbalimbali lakini serikali yetu inashindwa kuwathamini watu kama hawa na matokeo yake ndio haya tunayoyapata.
 
Back
Top Bottom