Kashfa ya Richmond: The FACTS

Mzee Mwanakijiji said:
Nasikia jamaa wa RDC waliitwa ikulu leo jioni... naona mkataba utavunjwa na jamaa watapigwa persona non grata!!

That's more like what I'm expecting.
 
Najua nini kitafuatia baada ya sakata hili la nishati kati ya Richmond Development Company, Tanesco na Serikali:

a. Serikali/Tanesco itavunja mkataba na RDC
b. Serikali itasema haikuridhishwa na utendaji wa kampuni hiyo.
c. Serikali inafanya juhudi zaidi na makampuni mengine kusaidia kuondoa adha ya kukosa umeme.
d. Waliohusika na mkataba wa RDC na Tanesco, na Wizara wataendelea kutembea vifua mbele bila hatua za kinidhamu dhidi yao kuchukuliwa.
e. Watanzania watapiga makofi, na kumpongeza Kikwete kwa "Kazi nzuri"
f. Watanzania watasahau ya mkataba huu, hadi mwingine utokee tena, na gurudumu la upotovu litaendelea kubingirika!!

Ila kabla ya hayo kutokea sikiliza ukweli kuhusu kampuni hii ni nini?

http://mwanakijiji.podomatic.com
 
nimesha yasoma haya kule kwenye magazeti na sasa nashangaa udhamini wa crdd mwanzoni walisema hakuna maongezi leo imekuwaje kwamba walikubaliana ?
 
Mzee Mwanakijiji said:
Nasikia jamaa wa RDC waliitwa ikulu leo jioni... naona mkataba utavunjwa na jamaa watapigwa persona non grata!!

Inaonyesha na daiy news wameconfirm jamaa kuitwa:

"......When reached for comment, the RDC Country Manager, Mr Naeem Gire, said: “I have not heard anything from the US regarding the gas turbines. I am at the State House. I have been called here. I am with some people. I will call you later. "

http://dailynews-tsn.com/page.php?id=4111
 
Jasusi,
Usiwe na wasiwasi, unajua kinachoendelea ni kama bwanaharusi ana amua kuwa mshenga mwenyewe sasa hapo ni kusubiri songobingo, tangu lini kama ni kweli raisi unaiingilia kila kitu ufanye badala ya kuwaaachia wataalamu??
Wajomba hapa tuka mkao wa kula tu, tusije shangaa kusikia kuwa hao jamaa walipelekwa kwa JK na RA, maana hizi ndo athari ya serikali iliyoundwa kwa kigezo cha urafiki na wala si uwezo.
Hujiuulizi ni kwa nini Mzee Kalala baada ya kuambiwa na dada zake kuwa hatutaki tena kukusikia unaikashfu CCM, kama kweli unampenda dada yako ambaye mwenye nchi anataka amwachie nchi kaa kimia.
Sasa kaa kimia kama sombwozombwi, jiulize saana wapi tunakwenda
 
mzee Kalala yupi mbona habari hii sijaipata ilivyo ? ndugu unaweza kuelezea kidogo maana habari ya kuachiana Nchi inakuwa kidogo kusohoto .tusaidie sisi akina kilaza juu ya swala hili la kalala tafadhali
 
Chingawanji,
Kalala alikuwa kizito mmoja katika mojawapo ya forums ( jina kapuni) Yeye alikuwa CUF dam dam. Lakini baada ya dada zake kushika hatamu za juu katika sirikali ya sasa amekimya. Mkao wa kula huo!
 
Jasusi said:
Chingawanji,
Kalala alikuwa kizito mmoja katika mojawapo ya forums ( jina kapuni) Yeye alikuwa CUF dam dam. Lakini baada ya dada zake kushika hatamu za juu katika sirikali ya sasa amekimya. Mkao wa kula huo!

Jasusi please kuwa wazi kuhusu hiyo forum. Kama forum hiyo ni kama hii, kwa nini usiiseme? Inakuwa kama magazeti ya bongo? Mheshimiwa mmoja (jina kapuni) alishikwa ugoni na mke wa mtu (jina kapuni) katika gesti moja (jina kapuni), wakatoroka na gari la ofisi fulani (jina kapuni) Utakuwa umesoma nini hapa? Heri kukaa kimya tu:)
 
Kwa kusaidia,

Mzee Kalala ni kaka wa Asha "Rose" Migiro na Mwantumu Malale.
Tuendelee na topic.

Mkandara, nimeshikika ndugu yangu inawezekana hii ikawa ni posting pekee leo humu. JK alivyokuja huko kwenu aliunganishwa kwa akina GIRE na Balozi (unamjua), kama unavyomjua JK ni mshkaji na anachukulia watu hivyo. Jamaa wa Richmond baada ya kukutana naye na kuelezea uwezo wao, JK akaonyesha dalili za kuwakubali. Jamaa wa ka tenda. Wakaweka website hewani haraka haraka. Tenda wakapewa.

Inawezekana ni uongo kuwa JK hakuhusika, ila jiulize swali moja kwanini Msabaha ana survive?, na kwanini dakika za mwisho akiulizwa alikuwa anasema wazi JAMANI MI SIHUSIKI. Procedures are always there, a well structured deal should always pass through those bureaucratic procedures!, watu wana akili Bob!

Basi nitachangia tena kesho

FD
 
Tanzania sasa tumefikia mahali pabaya, tinaingia mikataba na hata kampuni za mifukoni. Huu ni ufisadi wa hali ya juu.Wanaona 10% hazitoshi sasa wanakula 70%. Wahuni wawili KIKWETE NA LOWASA sasa wanaongoza nchi kwa micheni town. Enyi watanzania suala la kuitwa waungwana sasa linatakiwa likome, tuamke kutokomeza huu uhuni na ufisadi. Tutaendelea kuwa wapole mpaka lini?Hapa hakuna amani ya kweli, wao wapo ikulu na umeme wanao, pesa wanazo, na sisis wananchi tuna nini? hatuna umeme, rasilimali zetu wanatumia kwa faida zao. wananchi wanawafunika lilemba cha Amani. Nasisitiza hakuna amani ya kweli Tanzania.
 
Hawa Richmond ni wahindi wabongo,at least mmoja wao,wana kaofisi ka secretarial mtaa wa Mkwepu kanaitwa Richmond pia.
 
Zanaki, I'll bet you that office just popped up after these deals were going on.. kabla ya hili dili hiyo ofisi ilikuwa inafanya shughuli gani?
 
mwanakijiji...inafanya kazi za photocopy,typing,kutengeneza business cards etc
 
Umekosea, hata hao Richmond (agent wao wa Tanzania) huingia forum hii na nasikia alichukia kukuta watu wanajadili hili openly akajua deal ndo linayeyuka.

Heri wangepewa hawa Aggreko ambao wamechelewa sawa lakini umeme wa sasa kwa Dar unakuwa na afadhali japo walipewa MW chache nasikia.
 
Kwa mtu makini,website ya hao Jamaa wa Richmond inaacha maswali mengi kuliko majibu.Kwa mfano,wanazungumzia power project ktk mji flani huko Turkey lakini pekuapekua yangu ya haraka haionyeshi mahusiano yoyote kati ya kampuni hiyo na mradi huo.Pia website hiyo haina mwenekano wa kampuni kubwa ya kimataifa,yaani ni kama personal website tu.

Hawa jamaa ni matapeli lakini kwa jinsi nchi yetu ilivyo ni lazima watakuwa na high connections ndio maana JK na mpiga kelele wake Lowassa wako kimya kabisa wala hawawataji jamaa hao.Nashawishika kuamini kuwa JK alihusika kuchonga dili hiyo na ndio maana hata msabaha ameamua kuuchuna tu kwa vile yeye ni mpiga debe tu
 
Zanaki said:
mwanakijiji...inafanya kazi za photocopy,typing,kutengeneza business cards etc

Zanaki, katika kipande changu cha habari ya "Ukweli ni Huu" kampuni hiyo ya RDC inafanya kazi chini ya kampuni halali ya Richmond Printing hivyo sitashangaa hata Bongo wanataka kutumia kivuli hicho hicho!! How does Printing related to Power generation.. bogles my mind!!
 
Back
Top Bottom